Jaji Mfawidhi
JF-Expert Member
- Feb 20, 2016
- 14,047
- 20,411
Maswali chechefu:
1. Je, gazeti la "Mwanahabari" ni la nani?
2. Je, mwandishi aliyemtaja Naibu Waziri Mkuu, Mhe Dotto Biteko, kama "BITOKE" alikuwa anamuwaza muigizaji EBITOKE?
3. Je, gazeti hili halina Mhariri?
4. Je, gazeti hili linajua kuwa linapaswa kumuomba radhi Mhe Biteko & "Bongolanderz" kwa ujumla ?
NB:
(a) Rais Mkapa:
"Huwa sipendi kuhojiwa na waandishi wa hapa nchini kwavile hawafanyi utafiti na wanauliza maswali ya hovyo yasiyo na msingi"
(b) Rais Kikwete:
"Waandishi wengi wa Tanzania ni makanjanja. Wapo ambao hawajasomea na wengine hawana weledi. Siku hizi mtoto akimaliza "Form 4" akakosa kazi kote, mzazi wake anamwambia "Huna namna, inabidi tu uwe Mwandishi wa habari". Hii si sahihi kwani uandishi wa habari ni "fourth estate". Ni kitu cha muhimu sana kwa maendeleo ya Taifa"
(c) CJ Nyalali
"Waandishi wengi wanakosea sana uandikaji wa masuala ya kesi mahakamani na mara nyingi wanapotosha. Wahariri wahakikishe wanaleta mahakamani waandishi wenye uelewa kwani magazeti yao yanaweza kuchukuliwa hatua".
(d) Samwel Sitta
"Waandishi wawe makini kufuatilia Bunge. Uandishi wa upotoshaji habari za Bunge huko mbeleni unaweza kupelekea Wenye magazeti kuitwa na kuchukuliwa hatua na Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge".
(e) Prof. Kabudi
"Mimi niliwahi kuwa Mwandishi wa habari. Waandishi wa enzi zetu ni tofauti kabisa na waandishi wa sasa. Waandishi wengi siku hizi wana uwezo mdogo. Siwabagazi kwani huo ndio ukweli. Kiongozi ukiongea leo, utashangaa kesho magazeti manne yana kichwa cha habari kinachofanana! Wanadeseana! Enzi zetu, Mhariri alikuwa anakuna kichwa kuwaza atokee "angle" gani. Aidha, siku hizi Kiongozi akitoa mada, waandishi hawawezi kabisa kuandika "Summary". Wanasubiri Kiongozi akiwa anatoka ukumbini kwenda kwenye gari lake na kuanza kumkibilia kama kibaka kisha wanamwambia "Mzee, Umesahau kutupa "Press Release". Hii si sawa. Tubadilike"