Napenda niukuu ile slogan ya Nyani Ngabu na kuurudisha mjadala ambao ulishafungwa na labda tukipata wakti kuuangalia upya tunaweza kubadili fikira zetu na kuulizana jee sisi ndivyo tulivyo? matendo yetu, tabia zetu, fikira zetu, hulza zetu, utamaduni wetu, kufanya kazi kwetu, kuridhika kwetu, kulalamika kwetu, utegemezi wetu, uvivu wetu?
Jambo lililonisukuma kuanza jiuliza swali hili tena ingawa sikushiriki mjadala uliopita au kupitia kitabu cha Bundala kama kilivyoletwa na Zanaki wa Radio Butiama ni mambo kadhaa na tabia za "kawaida" katika jamii yetu na hata hapa kijiweni.
Wenzetu wazungu, ugumu wa maisha kutokana na hali yeyote, milele umekuwa ni kichocheo cha wao kuwa wachapa kazi, wavumbuzi, watafiti na kuendelea kutafuta suluhisho la matatizo yao au kuongeza ufanisi kupunguza ugumu na makali ya maisha au uchapa kazi. Mafanikio yao si kabisa au kamili (absolute/perfect), lakini husaidia sana kuleta mabadiliko na maendleo katika maisha na jamii zao na hivyo kuendelea kuwa na hali nzuri za maendeleo mpaka tunawanyeyekea na kuwaita "Nchi Matajiri".
Sisi tumedumaa, je ndivyo tulivyo?
Sasa hivi tumeletewa Mjapani yupo Ikulu kutushauri na kutufundisha jinsi ya kuachana na jembe la mkono, je Aisco, UFi, Ushirika, SUA, TFA, Kilimo wako wapi? je hawaoni umuhimu wa kuleta maendeleo na kuleta zana mpya za kuongeza ufanisi na uzalishaji mali mpaka tuletemwe taarishi kutoka Ajemi au Mashariki ya mbali? je sisi ni wavivu wa ubunifu na hatuna wataalamu wa kutosha au ndivyo tulivyo twashukuru kusaidiwa mpaka Chandarua?
Hujuma; ATC, BOT, Richmond, TISCAN na sehemu nyingine, jami tunapiga kelele na kushindana kutoa mapovu, lakini hakuna hata mmoja wetu ambaye yupo tayari kusema ngoja niende mahakamani na kudai haki kama Katiba inavyosema. Tumeachia Serikali "ifanye kazi huku tukiendelea kufaidi kupiga kelele na kutoa matusi na kashfa, "Chenge fisadi, Lowassa mhujumu, Screw Muungwana, Riziwani, Manji, Rostam, Othman, Bangusilo" na majina kibao kulia hujuma, ufisadi, Sisiemu, je hii ndio tabia yetu kuishia kulalama na kuendelea kunyanyaswa? je ni hali yetu ya ndivyo tulivyo inayofanya tuendelee kuhujumiwa?
Wakati wa sakata la maji Chuo Kikuu, niliuliza kwa nini Idara ya Uhandisi pale Chuo isiwe ya kimapinduzi na kufanya utafiti wa kina (utumike kama somo kwa wanafunzi na wapeme maksi kwa kushiriki) na kutafuta suluhisho la uhaba wa maji ambalo limetawala Chuo Kikuu kwa miaka mingi? Majibu yakaja Sisiemu, UDSM sio chuo tafiti, ooh Msola na lawama kibao! Je ndivyo tulivyo?
I would have thought kwamba Idara na wanafunzi wa Uhandisi wangekutana na Chuo cha maji, chuo cha ardhi na idara ya Jiolojia pale UDMS na kusema, jamani tutumie "talanta" (kama in Maryam anavyosema) tutafute mbinu za kuleta maji, iwe ni kuchimba visima, kuweka mabomba ya kiwango fulani, kutengeneza pampu au hata kutumia nyezno zote kutafuta namna ya kutumia lita 10 kupata mafanikio ya kutumia lita 30 za maji(efficiency)! Lakini kama Tulivyo, tunailaumu Dawasco, Azimio, CCM na Mafisadi!
NI lini basi tutaacha kuwa "ndivyo tulivyo"? Je tuna hata nia ya kuachana na dhana na fikira hizo za "Ndivyo Tulivyo"? maana ni mentality ya namna hii imetufanya tuendeleel kuwa tegemezi, kuhitimu katika uvivu, kuendelea kunyonywa na kupunjwa na mwishowe tumeanza kudhulumiana na kutafuna njia panya na za haraka kujipatia marudufu.
Huu Ufisadi, Uhujumu, Uzembe na Kunyonywa kungeendelea kutoea kama tungeamka na kusema "hivi sivyo tulivyo" na kuanza kufanya mambo kwa njia za maendeleo kama Wazungu, Waasia na Wamarekani kusini?
"Ndivyo Tulivyo" wikiendi njema kwenye kupata Kilauri, nyama choma, Ikibinda nkoi na Poozeo la kugombea baa (bamedi kama si changudoa)! Ndivyo tulivyo!