Who said it was based off of some study...? I was just generally speaking...geeez. Why are you so ornery today?
oh.. ok naogopa you might be able to convince me kuwa ndivyo tulivyo!! LoLest!
Katika kuperuze hii mada ninaona kuna kutofautiana kimaana kwenye hii hoja
'NDIVYO TULIVYO' tunamaanisha nini hasa.....kama watanzania, kama waafrika, watu weusi....katika 'abstract' level, ndivyo tulivyo haipaswi kuwa na mtizamo hasi wowote ule. Kwa nini nasema hivo? kwa sababu pia hata yaho 'maendeleo' ambayo sisi tunaoan wengine 'wameendelea', nini maana yake? tunakubaliana kuhusu maana ya maendeleo?
Walioendelea, walau katika maana ya kawaida tunategemea wawe na maisha flani ya kuwa na furaha, etc, lakini labda tujiulize, je wenzetu pamoja na kuendelea, are they 'warm' au 'cold'?
Ni kitu gani kinatufanya sisi tutake kuwa 'kama walivyo' na sio kama 'tulivyo', nikistick kwenye dhana kuwa 'ndivyo tulivyo' haina mtizamo hasi?
Nasema hivi kwa sababu naona tatizo linakuja pale tunapoichukulia hii 'ndivyo tulivyo' kwa mtizamo hasi. Naweza kuona kuwa hoja za Mzee Mwanakijiji zinaanzia hapa, na Nyani Ngabu akimaanisha kinyume chake.
Hivi tumeshawahi kujiuliza, kama kusingekuwa na mwingiliano na jamii nyingine, sisi kama waafrika tungekuwa wapi na tungekuwa na 'matatizo' yepi? Tungekuwa tunajiuliza kama hivi 'ndivyo tulivyo'?
Bubu ataka kusema,
Maelezo yako mazuri sana lakini kidogo unakosea kuitazama hiyo shilingi.
Umezungumzia swala la Waamerika weusi, hapa mkuu unaondoa Uraia wao na kuichukua rangi yao - meaning weusi. Hivyo unajaribu kuipanua hoja ama Mada ya Nnyani Ngabu kuwa ni swala la rangi sio tena Waafrika - I mean Watanzania ndivyo tulivyo.
Sasa ukisha vuka mipaka ya ramani na kuwa rangi hii inatuweka ktk nafasi ngumu zaidi kwani tutazungumzia tofauti kati ya minority na wapi wameendelea zaidi ya wenzao. Tofauti kama hizo tunaweza zipata hata ndani ya Watanzania, Mchagga anaweza sema hivyo hivyo lakini haiondowi ukweli kuwa sisi Wadanganyika pamoja na Wachagga Ndivyo tulivyo.
Mkuu population ya weusi US ni kitu kama 10% ambayo inaweza lingana na population nzima ya Tanzania. Lakini lazima ukubali kuna wasomi wengi weusi US kuliko TZ na uwezo wa mwafrika mweusi Marekani ni mkubwa kuliko mwafrika wa Afrika-Tanzania kwa kila sekta unayofikiria wewe. Na pengine margin ya Utajiri, middle class na umaskini kwa watu weusi Marekani ni 10-40-50 wakati hapa kwetu tunazungumzia 5 -15-80, hapa mkuu unapima mbingu na ardhi. Na ni ktk kuitukuza historia yao imeweza kuwakumbusha kule walikotoka hivyo kuongeza struggle zaidi kuhakikisha yale yaliyowakuta babu zao hayatarudiwa tena...Sisi na elimu zetu tunaishi ktk utumwa tena tunatawaliwa na ndugu zetu wenyewe.
Pili, umezungumzia swala la Nyerere kukumbukwa.. Mkuu wangu Nyerere anakumbukwa kwa sababu ailikuwa akisisitiza kuiweka Identity yetu mbele, nafasi ya Tamaduni zetu, lugha na Utanzania mbele ya kuiga. Ni ktk kumkumbusha Mtanzania kila siku kulinda hadi yake ndiko kulikompa sifa Nyerere na hata kina Nkurumah, Mandela na kadhalika hawa ndio madereva.
Kina Mwinyi na Mkapa ni viongozi madereva wa treni wanaofuata reli ya uongozi hivyo hakuna jipya ambalo wananchi wanaweza kuliwekea kumbukumbu kwani watu kama hawa wapo dunia nzima. Marais madereva wa reni yaani hawana kazi kubwa zaidi ya ku keep time, huko tuendako wameisha jengewa reli.
Could be both...
If I say Africans are more gregarious than whites because that is just the way they are....is that a good or bad thing?
Watanzania ndio tulivyo! maybe some of you ndivyo mlivyo, but I know that majority of Tanzanians are not happy about the direction of our beloved country and they would like to do something to bring a positive change, because THEY DO CARE ABOUT TANZANIA.
Bubu,
Kiteto folks had a chance and they blew it, the question is why? why did they find comfort to vote back Mtu wa CCM? Even if huyo Mbunge could have been a Saint, but he belongs to a party of Thieves, why in the heck did they give him a mandate and increase the dominance of Chama cha Mafisadi? Isn't it "ndivyo walivyo" wameridhika na Zimwi liwajualo?
Naomba tusilete usanii ambao tunaoutumia katika suala la uzawa. Nyani Nguba aliposema hivi hakumaanisha wahindi waishio Afrika au makaburu pengine hata wale waarabu wa kaskazini kwetu hawakuwemo kwenye ramani yake. Kinachozungumziwa hapa ni Mwafrika Mmatumbi. Ndio maana wale wengine walio wazi katika kutetea hoja hii waliingiza neno Nyani!
Statistics zinaonyesha kuwa mtu mweusi anayetoka Afrika anafanya vizuri kuliko wamarekani weusi marekani na wale wanaotoka katika visiwa vya karibian huko uingereza. Hawa waafrika wanajitahidi mashuleni na kwenye maisha ni wahangaikaji kuliko wenyeji wao. Kwa bahati mbaya hii imewafanya waafrika kuwa na tabia ya kuwadharau weusi wenyeji. Si mara moja nimemsikia mswahili akiwazungumzia 'niggas' kwa dharau. tunasahau mzigo wa historia. Ingawa sisi nasi tulitawaliwa lakini hatukuwa dehumanised kama walivyo fanywa hao ndugu zetu. Afrika ya kusini tunaona wanavyohangaika na hali hii. Sisi tulikuwa kwetu, tukapata uhuru kwetu na katika sehemu nyingi, pamoja na juhudi za wageni, asili yetu ilibaki pale pale na ndiyo iliyoweza kutupa confidence.
Nadhani hapa tatizo ni kuwa hatujaweza hasa ku'define' utanzania wetu. Sidhani kama mtu unaweza kusema kweli kuna tamaduni ya kitanzania bali ni tamaduni mchanganyiko wa makabila na watu wote wanaoishi Tanzania. Kujenga identity sio kitu kidogo. Hao wazungu mpaka leo wanahangaika katika kujaribu kuji'define'. Hii kazi wasingeweza kuifanya hao unaowataja peke yao. Mchango wa watu kama Shaaban Robert, Mwinyimila, Salum Abdallah, Mathias Tinga Tinga na wengine wengi wote wamechangia. Kazi ni yetu wote kuwaenzi katika huu mradi wa kujenga utaifa wetu.
Mkuu, kumbuka kuwa kuanzisha ni rahisi kuliko kuendeleza.
Mimi ninachopinga kwenye dhana hii ni matumizi yake katika kuwakebehi waafrika na kuwakatisha tamaa. Hayo yote yanayotolewa mifano ni tabia, tamaduni ambazo zinaweza kubalika. Ulaya kulikuwa hakuishi na magonjwa yanayotokana na uchafu hadi hivi karibuni tu. Nchi/Mji wa Singapore ulipopata uhuru ulikuwa mchafu kupindukia wenye vibiashara vya ajabu na hivi sasa ni moja ya miji safi duniani! Tunawalaumu watanzania kwa kuendelea kuikumbatia CCM, mbona wamarekani wamemchagua George W mara mbili?
Tusikate tamaa, na tusikubali kukatishwa tamaa.
Amandla!!!
Bagosha ne Basungu Kinehe, Ulimhola wa mamishago!
Baada ya kusikiliza pande zote mbili za waliomo na wasiomo, naomba wote mrudie bandiko la kwanza nililolitoa liwe mwongozo wa kujua mwelekeo huu ni wapi!
Nilifanya kwa makusudi kabisa kwa kuanzia Waafrika nikaongeza kwa kubadilisha na kusema I mean Watanzania ndivyo tulivyo!
Lengo langu ni kujichangua sisi Watanzania kama Taifa na kama Wananchi. Naomba tusianze kukimbilia kujifananisha na Wamarekani Weusi au Watogo maana hata kama wao wanamitabia inayofanana fanana, suluhisho la kusahihisha dhana ya "hivi ndivyo tulivyo" kwa Tanzania ni jukumu letu na tujipime ni vipi tutajisahihisha kama tutasema ni dhana potofu. Tukisema ni dhana jenzi na marudufu, ni vipi tutaifanya iwe yetu wote?
Mimi nitaendela kuhoji kama nilivyohoji awali, ni kwa nini tunaendelea kulea na kuishi katika tabia ambazo si endelevu? Zaidi ni ule uvivu wa kujituma, kuchacharika na kufikiri! Mbaya zaidi ni ule utashi wa urahisi kujifanyia mambo tunavyotaka kwa kukiuka sheria au kuzipuuzia, Angamizi zaidi ni kule kutaka kupata mapato na manono bila kutoka jasho au kutumika!
Ndio maana nikauliza, je ndivyo tulivyo? je ndio tabia zetu hizo na tumeridhika nazo? je kelele zetu hapa ni mazoea na kawaida kulalamika tuu bila kuchukua hatua ya kupanga mawazo yetu, kutafakari ni nini tunakipigia kelele na kufanya utafiti wa kupatia ufumbuzi au ni kawaida kupiga domo kulalama na kuendelea kulalama kwa kila jipya?
Suala la nani ni sawa ni subjective, kutokana na utashi wako. Nyani kahoji tabia za watu kula pale Kipawa mbele ya uchafu, je "hivyo ndivyo walivyo"?
Mwanakijiji ananena, wale waliopiga kura dhidi ya CCM "sivyo walivyo" lakini machoni pa CCM, "ndivyo walivyo", je lini Mtanzania atapiga kura yake kwa kutafuta mtu wa kumpa haki na tumaini na si mazoea? Je Wapiga kura wetu wengi "ndivyo walivyo" na wameridhika "jinsi walivyo"?
Je kupiga kwetu kelele kudai haki, heshima, uwajibikaji, kupiga vita ufisadi na uhujumu kunapokelewa na Watanzania kama "JF ndivyo walivyo" na kupuuzwa?
Bubu,
Kiteto folks had a chance and they blew it, the question is why? why did they find comfort to vote back Mtu wa CCM? Even if huyo Mbunge could have been a Saint, but he belongs to a party of Thieves, why in the heck did they give him a mandate and increase the dominance of Chama cha Mafisadi? Isn't it "ndivyo walivyo" wameridhika na Zimwi liwajualo?
Unasema kitu kibaya wazungu walichotutenda zaidi ya kutubeba utumwani, ni kutukandamiza fikra. Sasa kwa nini walitukandamiza na sisi tukakubali tu huku tukijua kwa hivyo wanavyofanya si sahihi? Kama tulikuwa tunatambua kosa hilo kwa nini hatukulikataa au kwa vile Ndivyo Tulivyo tulishindwa hata kukataa?
Na kwa nini hatukuwabeba wao utumwani au kwenda kuwatawala kwao kama walivyotutawala sisi wakati wa ukoloni?
Kwa nini nchi kama Zimbabwe iliyokuwa nuru ya matumaini barani Afrika wakati inapata uhuru sasa hivi imekuwa kichekesho na kutia huruma? Wananchi wake wanakula panya...wengine wengi tu wanakimbilia hadi Msumbiji....mfumuko wa bei umefikia asilimia 66,000...kwa nini?
soma kitabu cha Walter Rodney, How Europe Underdeveloped Africa...