Lyceum
JF-Expert Member
- Oct 1, 2009
- 1,046
- 568
Japo umeweka na mzaha kwenye huu uzi ukweli ni kuwa vyuo vina hali mbaya. Na wakulaumiwa ni wamiliki wa vyuo. Pale Tumaini Iringa wamefanya ufisadi usio na mfano na sasa nadhani ni mwaka wafanyakazi hawajalipwa salary. Waliofisadi hawajashitakiwa hata kwa balozi. Ovyo sana na misalaba yao vifuani
Vyuo tajwa vipo hoi kifedha mathalani SAUT Tawi la Arusha hatujalipwa mwezi wa tatu sasa. St. John's centre ya Kigoma imefungwa kwa kukosa wanafunzi. Hakika twafwa na elimu yetu ya kuunga-unga.
**Twende wapi na tumesoma vyuo vya kanisa tukiomba kazi pale UDSM sijui SUA hawatupi hata kazi ya ulinzi. Wanatudharau sana asee. Wanadai sisi eti KIWANGO DUNI (KIWADU).
