Tetesi: Vyuo vikuu vya Umma Tanzania viko hoi kifedha, skuli, ndaki, Idara hata Karatasi shida

Wadiz

JF-Expert Member
Nov 10, 2022
5,411
11,061
Habari!

Niende moja Kwa moja maada, habari kutoka kwa wahusika, hali ya kifedha vyuo vikuu Tanzania so njema, inasemekana, ndaki, skuli, idara toka mwaka jana mwezi Juni hawapati pesa za uwendeshaji, mathalani hata karatasi tu za kuchapishia mitihani ya mazoezi ni shida tu, je hazina na Waziri wa elimu na wakurugenzi wanafahamu hilo, Rais wa nchi anajua hilo, waziri mkuu anajua hilo?

Mamlaka husika amkeni hali ya kifedha vyuo vikuu vya Umma si shwari, vyuo vingi hicho mnachoita OC/ sijui mapato ya ndani hawana kuhimili mzigo wa uendeshaji.

Sisi tuliopo Dodoma tuna fursa ya kufahamu mengi kazi kwenu wahusika vyuo vikuu viko katika hali ya aibu. Madokezo mbalimbali tunayaona timizeni wajibu.

Ikiwezana waambieni waitishe minada ya kuuza baadhi ya magari ili wajikimu kibajeti.

Sio ajabu wakuu wa vyuo pesa za vikao, safari, na extra duty allowances, na overtime wanazo, huku skuli, ndaki, idara, directorates zikiwa hoi

Kazi kwenu

Wabillahi
 
Acha uongo jamaa narudia acha uongo jamaa narudia tena na tena na tena achaaaaa uongoooo jamaaaa
Tetesi unajua maana yake? Hali jumuishi imetumika kuondoa hali ya kutaja mifano, ukitaka niweke bayana wakuu wa baadhi ya hivyo vyuo watapoteza kazi, anaebisha, serikali isambaze makachero wapite vyuoni waongee wa wafanyakazi kwa kificho ama kwa siri, vyuo vikifuria hakunaga Siri.
Kabla hawajafika dodoma waanze na vyuo vya DSM na Morogoro kwa kwanzia
 
Tatizo linaanzia wapi mpaka wanafikia kwenye hali hii
Mapato ya Ada yanaenda hazina na hazina hawajali vyuo, they don't dish out money on time ni kama hawajali na waendeshaji ni waoga, centralized system.
 
Vyuo vikuu viruhusiwe kukopa hadi asilimia 25 ya bajeti yao kutoka kwenye taasisi za fedha ili kuweza kukidhi majukumu ya kifedha hasa pale wanapochelewa kupata pesa kutoka vyanzo husika.
Hii itasaidia kupunguza kukwamisha shughuli za vyuo hasa pale fedha zinapochelewa kuletwa.
 
Vyuo vikuu viruhusiwe kukopa hadi asilimia 25 ya bajeti yao kutoka kwenye taasisi za fedha ili kuweza kukidhi majukumu ya kifedha hasa pale wanapochelewa kupata fedha kutoka vyanzo husika.
Hii itasaidia kupunguza kukwamisha shughuli za vyuo hasa pale fedha zinapochelewa kuletwa.
Maji,umeme na makaratasi!!
 
Mapato ya Ada yanaenda hazina na hazina hawajali vyuo, they don't dish out money on time ni kama hawajali na waendeshaji ni waoga, centralized system.
Wanaosimamia hazina si zao la vyuo hivi hivi?
Kama mliwafunfusha hivyo kwa nini mnalalamika?
Wao ndio walipendekeza utaratibu uwe hivyo sasa inabidi msilalamike.
Nchi hii imekuwa na ukiritimba mwingi hasa kutokana na aina ya wasomi tulio nao.Na kwa kiasi kikubwa wanaiga tabia za walimu wao vyuoni.
Elimu zinawapa kiburi ila nashangaa kuwa kwenye kiburi leo mnakuja kulalamika hapa?

Sent from my Infinix X626 using JamiiForums mobile app
 
Mimi sihusiki na hio kazi ya misukule tafadhari ualimu ni ungedere tu kwangu, hapa dodoma mimi nawafadhili bata na mikopo ya hapa na pale mimi nafaidi mbususu tu, tafadhari sana.
 
Mimi sihusiki na hio kazi ya misukule tafadhari ualimu ni ungedere tu kwangu, hapa dodoma mimi nawafadhili bata na mikopo ya hapa na pale mimi nafaidi mbususu tu, tafadhari sana.

Punguza dhara kwa kazi za watu. Unaita ualimu wa chuo kikuu ni sawa na msukule?. Please.
 
Back
Top Bottom