Vyoo vya kukaa vimenishinda

Vyoo vya kukaa vimenishinda

Habari wakuu,natumai mko vyedi kabisaa katika harakati za kusaka noti.Niende kwenye point,hivi karibuni nilikuja hapa jf nikaandika uzi wa kutafuta chumba so baada ya muda nikapata,sasa kimbembe hii room ina choo cha kukaa (KINU).

kiukweli toka nizaliwe sijawahi kuishi nyumba yenye choo cha aina hii,hivyo matumizi yake ni mtihani kwangu.

Kukaa napata shida mara ndonga iingie kwenye maji,mara mzigo ukishuka kwa uzito wa hali ya juu unasababisha mlipuko wa maji yananirukia makalioni dah,yani napata tabu sana kifupi mpaka nimekua nikienda kutumia choo cha kuchutama kwa rafiki yangu wa karibu.

Kazi njema wote.
Wanaoleta vyoo vya kukaa wanafanya makusudi au hawajui specifications za vyoo aina ya 'non splash symphonic' hasa vile toka Uingereza, TYFORD UK (sio tyford vya China) havina hilo tatizo.
Ila kuvijua inahitaji uelewa.
 
Vyoo vya kukaa hasa vikiwa public mi huwa hata mzingo wenyewe unapotea kabisa yaani mtu anatoka hapo amekaa hujui anamagonjwa gani ya ngozi huwa vinakera kwakweli sivipendi labda mtu atumie kwake yy na mke wake tu
 
😀😀😀😀😀 NDONGA,umenikumbusha kitambo sana mkuu.Big Up
 
Nani asiyependa kustarehe wakati wa kujisaidia?? Sio siri choo cha kukaa kina raha yake!!yaani unaweza shusha mzigo huku unasoma gazeti.....ninachokiona humu ni wachangiaji wengi hawa afford choo cha kukaa ndyo maana wanapeana moyo kuwa choo cha kuchuchumaaa ndyo kizuri!!
No! Choo cha kukaa kwa public hapana!
 
Hicho choo kilinisababisha sikukata gogo wiki, kila nikienda nakaa tigiti haitoki navaa ile natoka chooni tu najisikia kuharibu kiasi kwamba nikishtuliwa tigiti inatoka yenyewe, nikirudi chooni nikikaa vilevile
 
Kama wasiwasi wako ni kuguswa na yale maji weka tissue kabla ya kukata gogo.

Chumbani kwangu natumia choo cha kukaa lkn hakifai kama matumizi ni ya watu wengi
 
Mwenzangu nilikaa kama lisaa hivi natafuta maji si unajua uswahilini kwetu shimo huna haja ya maji

Katika kufikiriaaa aaa nikaona wasinitanie ikabidi nichote maji na jagi nililikuta toi mwagia wapi!! Daah

Nikitoka na choo ni cha ndani lazima watajua ni mm,ikabidi niweke mkono juu nifikilie kwa makini nifanyaje

Lahaula kumbe nilipoweka mkono paka bonyea sehemu nikaona maji hayo aaaa wacha ninogewe nikaendelea na zoezi la kubonyeza hahaha.
Hahahhahha mkuu siku hyo sijui ungetokaje bila kubahatika na mkono kugusa kidude
 
Nani asiyependa kustarehe wakati wa kujisaidia?? Sio siri choo cha kukaa kina raha yake!!yaani unaweza shusha mzigo huku unasoma gazeti.....ninachokiona humu ni wachangiaji wengi hawa afford choo cha kukaa ndyo maana wanapeana moyo kuwa choo cha kuchuchumaaa ndyo kizuri!!
Vipi kuhusu maswala ya kujisafisha mkuu tupe darasa hapo
 
Back
Top Bottom