Vyoo vya kuchuchumaa ni bora kuliko vyoo vya kukalia

NetMaster

JF-Expert Member
Sep 12, 2022
1,454
4,853
NB: Haihusishi walemavu ambao inabidi wavitumie vyoo vya kukalia.

Kiukweli linapokuja suala la kwenda haja, choo cha kuchuchumaa ni kizuri zadi kuliko cha kukaa..

1. mkao wa Mchuchuma ndio pozi la asili kwajili ya kutoa haja kwa ufanisi wa hali ya juu, njia ya haja linafunguka zaidi pale tunapochuchumaa, na hii ndio sababu kuu ya kwenda haja kwa kuchuchumaa.

2. kuchuchumaa ni zoezi ambalo ni zuri kiafya kulifanya mara moja moja si mbaya kwajili ya nguvu za magoti, kunyoosha mgongo, n.k.

3. Choo cha kukaa, kinyesi huwa kinatua moja kwa moja kwenye tundu lenye maji, kero hapa ni pale kinyesi kikiwa kizito au kikubwa kikitua yale maji huwa yanaruka na kumfikia mtumiaji kwenye sehemu za kutoa haja, hii ni hatari kiafya.

4 choo cha kukalia ni vema ukitumie mwenyewe ama wawili mke na mme kwa kuzingatia usafi na afya, si vizuri kitumike na wengi kwasababu zifuatazo:
  • mtu akikaa kuna ule mgusano wa mapaja na choo unaweza kupelekea magonjwa ya ngozi,
  • mtu anapokaa anaweza kuliacha jasho lake sehemu ya kukaa,
  • mtumiaji akikojoa huwa kuna matone ya mikojo yanaweza kudondokea sehemu ya kukaa,

5. Choo cha kuchuchumaa unaweza kujisafisha kirahisi kuliko choo cha kukaa.
 
Huwa nawazaga, hivi Mtu mwenye mtambi mkubwaaa huwa anachuchumaeje? Au mdada mwenye kilo nyingi, au nyamanyama nyingiiiiiii huwa anachuchumaeje?
 
NB: Haihusishi walemavu ambao inabidi wavitumie vyoo vya kukalia.

Kiukweli linapokuja suala la kwenda haja, choo cha kuchuchumaa ni kizuri zadi kuliko cha kukaa..

mkao wa Mchuchuma ndio pozi la asili kwajili ya kutoa haja kwa ufanisi wa hali ya juu, Tundu la haja linafunguka zaidi pale tunapochuchumaa, na hii ndio sababu kuu ya kwenda haja kwa kuchuchumaa.

Pia kuchuchumaa ni zoezi ambalo ni zuri kiafya kulifanya mara moja moja kwa muda mfupi.

Kwa ajili ya usafi na afya, choo cha kukalia ni vema ukitumie mwenyewe ama wawili mke na mme wake huku usafi ukizingatiwa sana
Yani umesema kweli kabisa.
Majuzi hapa nyumba nloenda Kuna choo cha kukaa. Nlipata shida sana maan nlikua nakojoa matako juu miguu hadi imetokea vinumbu.
 
Mi huniambii kitu choo cha kukaa ,toka nitumie choo cha kukaa hata UTI sipati tena au kuwashwa na nakisafisha vizuri na sabuni na dawa kila siku,choo cha public ni cha kuchuchumaa wanatumia watoto,ila chumbani choo cha kukaa safii ukisafisha ukakausha maji panakuwa pakavu halaf na kale kabomba pressure water huku unachart
 
Usafi ni muhimu sana Chooni ili kudhibiti UTI, haijalishi ni choo cha kukaa ama kuchuchumaa.

Ila choo cha kukalia ni hatari zaidi kwenye uti kwa sababu urinary tract ni rahisi kugusana na bacteria unapokaa kwenye choo, hivyo inabidi kiwe kinafanyiwa usafi wa hali ya juu sana.
 
Nasindikiza na kapicha
IMG_20221213_155947_882.jpg
 
Huwa nawazaga, hivi Mtu mwenye mtambi mkubwaaa huwa anachuchumaeje? Au mdada mwenye kilo nyingi, au nyamanyama nyingiiiiiii huwa anachuchumaeje?
Nilipokuwa dogo tulikuwa tunakaa nyumba moja hivi ya kupanga, choo ni cha nje tunatumia watu wengi. Siku moja nilienda chooni sikujua kama kuna na sikubisha hodi kumbe kuna bimkubwa mmoja bonge alikuwa anakata gogo. Nilishuhudia ameyashikilia makalio yake ameyatawanya huku na huku ili aweze kupuu. Tangu siku ile ile picha ilibaki kichwani mwangu so nahisi watu wanene ndo wanavyokata gogo!
 
Vyoo vyote ni bora tofauti ni kipi umekizoea ukizoea cha kukaa(European type) basi cha kuchuchumaa( Asian type)kitakupa shida kukizoea cha muhimu nikuzingatia usafi sana cha mwisho kwa mazingira yetu cha kukaa kina itaji watu wawili au mmoja kwa matumizi sio vyema kuwekwa public
 
Back
Top Bottom