Vyama vya Upinzani Tanzania vinashindana, vikipata mshindi ndio mapambano dhidi ya CCM yataanza

busar

JF-Expert Member
Dec 22, 2011
1,068
1,061
Asalam,

Tukumbushane, 20% wanataka vyama vingi, 80% wanaitaka CCM kama Chama Pekee. Hapajakuwa tena na kura za maoni tofauti na hizo. Matokeo ya Uchaguzi Mkuu hayajawahi kushinda huu utafiti wa Je tuwe na vyama vingi au lah.

Hoja, hii 20% haina rangi kiasi kwamba unaweza kusema ni yule na yule, halkadhalika hii 80% nayo iko hivyo hivyo.

Hivi vyama vya upinzani Tanzania vina wanachama wake 20% wapinzani halisi na 80% ni wana CCM WALIOKOSA FURSA ndani ya CCM. Hadharani ni Wapinzani, lkn ndani fikra, matendo, na imani yao ni CCM. Hawa wana marafiki wengi kote kote.

Hivyo basi, 20% ya viongozi wa upinzani ni wapinzani kweli, 80% ya viongozi ndani ya vyama vya upinzani ni CCM.

Tukienda hivyo utauona ukweli. CCM inanamna ya kuwasiliana na kuwatia adabu wanachama wake walio ndani ya chama na walio nje. Walio ndani vikao vya chama vitakaa, walio nje watatupwa kidogo segerea, wakitoka wanaitwa kikaoni kuwa sasa rudi kwenye misingi. Hivyo vikao vya siri sana huwakumbusha historia zao hata ambazo watajifanya hawazijui.

Wako walioambiwa kinagaubaga juu ya koo zao halisi.

CCM ni ileile, leo, kesho na hata milele. Haibanduki.

Sasa tufanyaje?
 
Back
Top Bottom