Adharusi
JF-Expert Member
- Jan 22, 2012
- 14,402
- 7,310
Msingi wa vyama vyote siasa Duniani umezaliwa ubavuni mwa vyama vya wafanyakazi. Kwa sababu kundi la vyama vya wafanyakazi wote wanakua wamesoma na werevu, ndio kundi la kwanza kuona ukandamizaji katika jamii, na kuanza kutoa elimu kwa jamii.
Vyama vya wafanyakazi mara nyingi kazi ngumu ya kupambana na muajiri, wakiwa wameweka rehani ajira yao. Ndio maana viongozi wengi wa vyama vya wafanyakazi wanapoteza ajira zao kwa sababu ya kupigania ustawi wa wanaowapigania, wanapoteza mahusiano na muajiri katika mazingira ya kazi.
Kuna tofauti kubwa kati ya vyama vya wafanyakazi na vyama vya siasa. Viongozi wa vyama vya siasa wapo huru kupambana na dola kwasababu hawako ndani ya ajira ,na hawana cha kupoteza.
Viongozi wa vyama vya wafanyakazi ni waajiriwa yaani wanapambana muajiri ambae anaweza kuwa serikali au sekta binafsi lakini ni muajiriwa tofauti kubwa sana.
Kuna tofauti kubwa sana ufanyaji wa kazi vyama vya siasa na vyama vya wafanyakazi, ukiona mtu kiongozi wa chama cha wafanyakazi hata kama ni ngazi ya Tawi mpe heshima yake, maana amejitoa muhanga kwa ajili ya wenzake.
Kwahiyo Abdul Nondo na Heche labda hawajui historia ya vyama vya wafanyakazi, wakae na waombe hitoria sio kudharau na kushambulia vyama vya wafanyakazi sitaki kuamini kuwa wamekodiwa kwa mradi maalumu kushambulia vyama vya wafanyakazi.
Vyama vya wafanyakazi vipo kwa mujibu wa sheria ya ajira na mahusiano kazini,sheria ya majadiliano. Kwahiyo wananjia za kupita katika majadiliano kabla ya kupiga kelele.
Nimeona Heche akishambulia vyama vya wafanyakazi Mara ya kwanza nilidhani bahati mbaya, juzi nimemuona ameshambulia chama walimu Tanzania, na kudharau kabisa CWT kwangu inaniambia hana taarifa za kutosha namna vyama vinavyofanya kazi, akae atafute watu wamuelimishe na asome sheria ya ajira na mahusiano kazini sasa huyu ni kijana kutoka chadema alikua kiongozi wa vijana chadema
Nimemuona tena kijana wa ACT Wazalendo Abdul Nondo, huyu ameandika hadithi nyingi akishambulia viongozi wa CWT, na kumpigania aliekua katibu mkuu 2020 mpaka June 28 ,2022.
Nondo anaonekana kabisa kanunuliwa kumpigia chapuo Aliekua Katibu mkuu Thefu, ambae alifungwa miezi sita kwa uchepushaji wa fedha ,ni kweli amekata rufaa ni haki yake lakini kimaadili tu peke yake hastahili hata kusogelea CWT.
Kipindi cha Thefu na mtandao wake CWT ilijaa udikteta, waliondoa viongozi wote waliokua na mawazo ya kuwajali walimu, walifuta mkono wa kwaheri, walifuta Tshirt kwa walimu ,walinyima uhuru wa wanachama kutoa maoni yao.
Sasa baada ya kuingia Katibu mkuu mpya ,anarudisha fedha wilayani, Thefu alikataa kupeleka fedha wilayani, sasa hivi chama kimeandaa mikutano mikuu bila kukopa fedha ,wananunuaa Tshirt za walimu wote ,ambayo Thefu alishafuta na genge lake, Thefu alinunua media zote na watu maarufu wakiwepo Thadeo Mushi kumpamba kwenye mitandao ya kijamii.
Niwaambie Heche na Nondo kama wametumwa kushambulia vyama vya wafanyakazi, wajiandae kundi wanalolishambulia ndio kubwa na werevu kuanzia katika vijiji.
Pia wanatakiwa kujua bila vyama vya wafanyakazi, wafanyakazi wnagekua wanyonge sana kwa muajiri
Jukumu la vyama vya siasa ni kutetea makundi yote kwenye jamii na kuungana makundi yote yanayopigania haki ya jamii ikiwepo kundi la vyama vya wafanyakazi sio kuwabeza.