Profesa Mkumbo: Msiweke wagombea wasiokubalika na wananchi uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
5,897
10,358
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji na Mbunge wa Jimbo la Ubungo Kitila Mkumbo amewataka mabalozi wa mashina kujiandaa na uchaguzi wa Serikali za mitaa utakaofanyika mwaka 2024.

Akizungumza na mabalozi wa mashina katika kata ya Manzese baada ya kufanya ziara ya kuwatembelea wananchi Prof. Kitila amesema kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa wananchi na viongozi wanapaswa kujiandaa na kuzungumza mambo yanayofanywa na Serikali.

Prof. Kitila amesema uchaguzi wa awamu hii utakuwa na ushindani mkubwa baina ya vyama vya siasa hivyo ipo haja ya kuweka wagombea wanaokubalika na Wananchi na siyo wanaopendwa na viongozi.

Amesema sheria ya uchaguzi imebadilishwa na hairuhusu mgombea kupita bila kupingwa, hivyo hata kama yupo mgombea mmoja zitapigwa kura za ndiyo au hapana hivyo ipo haja ya kujipanga kwaajili ya uchaguzi.

"Muwachuje wagombea vizuri ili mnaowapeleka kwa Wananchi wawe ni watu wanaokubalika na kuuzika, tusipeane wakati mgumu katika kutafuta kura kwa wananchi" amesema Prof. Kitila Mkumbo

Pia amesema hata ikitokea chama hakimpendi mtu lakini wananchi wanampenda apelekwe ili wananchi wawe na uhuru wa kuchagua, mambo mengine yatarekebishwa mbele na akitokea mgombea viongozi wa chama wanamtaka lakini wananchi hawamtaki huyo naye aachwe

Amewataka wajumbe wa mashina kuwa huru kumuita muda wowote wanaomuhitaji katika maeneo yao ili aweze kushirikiana na wananchi ili kusikiliza changamoto na maoni yao.
 
Kuna haja katika kuchagua wale watakaogombea kwenye serikali za mitaa wawe wale wenye nyumba kwenye sehemu wanazotaka kugombea! Matatizo yanatokea pale walinzi wa viwanja na sio wenye nyumba wanapojitokeza na kugombea Uongozi ili hali hawana mali sehemu hizo; hivyo kutojali maendeleo ya sehemu hizo hasa Kuhusu kuruhusu ujenzi holela kwenye sehemu zisizotakiwa kujengwa kama vile barabarani na upenuni mwa nyumba za watu hivyo kusababisha uchafu na kuenea kwa magonjwa kwani hawa Watu huwa hawana vyoo hivyo kujisaidia hovyo na kueneza magonjwa!!!

Waziri Mchengerwa hana buda kuhakikisha kuwa wale wanaoteuliwa kugombea kwenye mashina sio walinzi wa viwanja/nyumba bali wenye mali ili wawe na uchungu wa Maendeleo ya sehemu zao! Walinzi wa site wakiwa wajumbe ,wanawaruhusu Watu kujenga mabanda ya kuishi kwenye viwanja wanavyolinda ambako watu wanakuwa wengi lakini hawana vyoo vya kujisaidia hivyo kutupa vinyesi barabarani na kuwa hatari kwa kueneza magonjwa.
 
Huyo Kitila aache utapeli wa kijinga, ccm haitegemei kura za wananchi kukaa madarakani. Wanalazimisha kukaa madarakani kwa shuruti Hadi wamefanya box la kura lidharaulike, matokeo yake watu hawana muda tena wa kupoteza kwenye mstari wa kura. Sasa huo ugumu anaoongelea ni upi?
 
Vipi?
Mtashiriki uchaguzi?
 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji na Mbunge wa Jimbo la Ubungo Kitila Mkumbo amewataka mabalozi wa mashina kujiandaa na uchaguzi wa Serikali za mitaa utakaofanyika mwaka 2024...
Yeye mwenyewe hakubaliki kwenye ubunge alipita kwa nguvu na ushawishi wa jiwe aangalie moto wake uchaguzi ujao, mmoja atakaeangushwa saa nne asubuhi ni Kitula makumbo
 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji na Mbunge wa Jimbo la Ubungo Kitila Mkumbo amewataka mabalozi wa mashina kujiandaa na uchaguzi wa Serikali za mitaa utakaofanyika mwaka 2024...
Vyama vingine vitaweka waogombea ambao ni hodari na jasiri wa kuporomosha mitusi, matokeo yake anaambulia kura yake moja na yake pekeyake
 
Maneno mengi ila uchaguzi ukifika wanazima internet na kuingiza maboksi ya kura. Stupid
 
Prof Mkumbo anatuchekesha tu.
Yy hawezi mshinda DED Mwantumu 2025 kura za maoni CCM.Alimuibia kura 2020 atamuibia tena kura 2025.Prof hakubaliki kabisa Ubungo.

2025 hawezi mshinda Meya Bonifas lkn DED anaye tangaza matokeo ni ‘ndugu yake’
 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji na Mbunge wa Jimbo la Ubungo Kitila Mkumbo amewataka mabalozi wa mashina kujiandaa na uchaguzi wa Serikali za mitaa utakaofanyika mwaka 2024.

Akizungumza na mabalozi wa mashina katika kata ya Manzese baada ya kufanya ziara ya kuwatembelea wananchi Prof. Kitila amesema kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa wananchi na viongozi wanapaswa kujiandaa na kuzungumza mambo yanayofanywa na Serikali.

Prof. Kitila amesema uchaguzi wa awamu hii utakuwa na ushindani mkubwa baina ya vyama vya siasa hivyo ipo haja ya kuweka wagombea wanaokubalika na Wananchi na siyo wanaopendwa na viongozi.

Amesema sheria ya uchaguzi imebadilishwa na hairuhusu mgombea kupita bila kupingwa, hivyo hata kama yupo mgombea mmoja zitapigwa kura za ndiyo au hapana hivyo ipo haja ya kujipanga kwaajili ya uchaguzi.

"Muwachuje wagombea vizuri ili mnaowapeleka kwa Wananchi wawe ni watu wanaokubalika na kuuzika, tusipeane wakati mgumu katika kutafuta kura kwa wananchi" amesema Prof. Kitila Mkumbo

Pia amesema hata ikitokea chama hakimpendi mtu lakini wananchi wanampenda apelekwe ili wananchi wawe na uhuru wa kuchagua, mambo mengine yatarekebishwa mbele na akitokea mgombea viongozi wa chama wanamtaka lakini wananchi hawamtaki huyo naye aachwe

Amewataka wajumbe wa mashina kuwa huru kumuita muda wowote wanaomuhitaji katika maeneo yao ili aweze kushirikiana na wananchi ili kusikiliza changamoto na maoni yao.
Stupid, yeye alikubalika na nani? Magufuli? Stupid of him!
 
Back
Top Bottom