Vyama vya Siasa, Vijana waaswa kwenda kujifunza Maadili na Uzalendo katika Chuo cha Uongozi cha Mwl. Nyerere

MIMI BABA YENU

JF-Expert Member
Mar 1, 2019
208
500
1613377597236.png

Wajumbe wa Baraza la wadhamini la Chama Cha Mapinduzi ,(CCM) limewataka viongozi wa vyama vya upinzani nchini kujiunga na Chuo cha uongozi na Itikadi cha Mwalimu Nyerere ,kilichopo Kwamfipa,Kibaha,mkoani Pwani, ili kujiongezea uwezo na kujifunza maadili na uzalendo wa nchi yao.

Walizungumza hayo mara baada ya kukagua majengo ya chuo hicho,wakati walipofanya ziara ya kutembelea chuo hicho ,kujionea maendeleo ya mradi wa ujenzi wa chuo hicho.

Mwenyekiti wa baraza hilo ,ANNA ABDALLAH na makamu wake PANDU OMARY KIFICHO walisema, vyama imara kama CCM viongozi wake huandaliwa kuwa na maadili na uzalendo hivyo hivyo chama chochote kinachotaka kujiimarisha basi kipeleke viongozi na vijana wao kupikwa katika chuo hicho .

Hata hivyo ,walielezea, baraza limeridhishwa na kukamilika kwa ujenzi huo ambapo hatua iliyoko sasa ni kukamilisha kupitisha rasimu ya mitaala.

Anna alishauri kuingiza somo uzalendo na maadili kwa wanafunzi watakaopikwa katika chuo hicho hususani vijana waweze kujua historia ya nchi yao.

PANDU OMARY KIFICHO ambae ni Makamu mwenyekiti wa baraza hilo ,aliwataka vijana kujiunga na Chuo hicho ili kupata mafunzo yatakayowapa maarifa watakapofanikiwa kuwa viongozi kwenye ngazi mbalimbali.

Kwa upande wake,Naibu Katibu Mkuu, Rodrick Mpogoro alisema kuwa wataendeleza fikra za hayati Mwalimu Julius Nyerere.

"" Ambapo na ujenzi wa Chuo hiki unatekeleza kwa vitendo fikra hizo na wanavyowaona viongozi waliotangulia wanapata faraja"aliongeza Mpogolo.

Msimamizi wa mradi huo, EMANUELA KAGANDA ,alifafanua, mradi huo umekamilika kwa upande wa Ujenzi wa majengo ,umegharimu kiasi cha sh.bilioni 90, na kitakuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 200.

Alisema kuwa, ujenzi huo ulianza mwaka 2018, ambapo amedai umechelewa kutokana na hali ya mvua pamoja na kuibuka kwa ugonjwa wa Covid-19 Corona.

Kaganda aliweka bayana , hatua iliyoko sasa ni kupitisha rasimu ya mitaala.
 

tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
40,706
2,000
Hakuna uzalendo utafundishwa kwenye hicho chuo zaidi ya siasa outdated zenye mitazamo ya kijamaa. Huko watu watafundishwa siasa za kinafiki, wizi wa kura na kung'ang'ania madaraka. Wapinzani watakaopeleka wanafunzi hapo kuwa brainwashed ni yale matawi ya ccm.

Huu ujinga wa watu kujifanya wazalendo niliuona enzi za kina Mwigulu walipoenda JKT, walipotoka tu bomu lililipuka kwenye mkutano wa cdm huko Arusha. Mpaka leo jambo lile serikali halijatoa majibu ya mauaji yale ya kinyama. Huo ndio uzalendo utakaofundishwa kwenye hicho chuo.
 

Bila bila

JF-Expert Member
Dec 20, 2016
13,496
2,000
Ujinga mtupu!Kwani zamani enzi za mwalimu ambapo karibia kila mtu alikuwa mzalendo hadi watoto wadogo walikuwa wazalendo,je wao walifundishwa kuwa wazalendo katika chuo kipi?
Nasikia somo la Historia ya Tanzania zamani lllikuwa linafundishwa wakati wa Nyerere ila Mwinyi akalifuta, tukaishiwa uzalendo.
 

Scoundrel

JF-Expert Member
Jan 14, 2019
534
500
Tumepitia wengi sana JKT lakini si suluhisho la uzalendo wapo wezi wengi na wabadhilifu wakiwamo hao hao mnaosema wana uzalendo
 

FUSO

JF-Expert Member
Nov 19, 2010
23,252
2,000
kujifunza nini? siasa za fitna, siasa za vita, siasa za majungu !! Yaani hawa hawa wateka watu watufundishie vijana uzalendo?
 

Masanja

JF-Expert Member
Aug 1, 2007
4,350
2,000
Shida ni kwamba hata viongozi wetu wa sasa waliopita kwenye 'hivyo vyuo' vya Nyerere...mpaka wengine kufanya kazi na huyo Nyerere.... hawana maadili wala uzalendo. Sasa sijui unawaambiaje wengine kwamba kusoma chuo chenye jina la Nyerere ndo kuwa na maadili ya Mwalimu. Kuna sehemu iko shida na watawala wetu. Wakishiba kodi za wananchi wanaongea lolote tuu ilmradi…..
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom