mama D
JF-Expert Member
- Nov 22, 2010
- 19,760
- 35,205
Habari za asubuhi
Siku zinakwenda, mambo mengi yanabadilika, watanzania wanabadilika lakini hatari ni kwamba mifumo na miongozo ya vyama vingi vya siasa inabaki ileile ya kufanya mambo kwa mazoea.
Hivi, viongozi wa vyama vya siasa pinzani mlishawahi kujiuliza ni nini kipya mnaweza ambia wananchi au kufanya ili kuongeza thamani ya vyama vyenu huku mitaani? Mlishawahi kufanya tafiti kujua ni vitu gani wananchi wakipata watakua loyal kiasi cha kusimama kidedea na kuwalinda viongozi wao kwa hali na gharama yoyote na kuhakikisha msukumo wa kushinda uchaguzi unatoka kwao na sio kwenu?
Badala ya kutenga budget ya kwenda kutembea na kuwapa wananchi maneno matupu huko majimboni ili mjinufaishe nyie na familia zenu kwa hizo per diem, nufaikeni kidogo na wananchi mnaowatembelea wanaufaike kidogo. Mkono mtupu haulambwi. Watanzania wala hawataki mambo makuuuubwa, wnataka mambo madogomadogo yenye muendelezo
Msikurupuke makaendelea kufanya vitu vilivyokwishafanyika, sera zenu zinaweza kuwa nzuri sana ila sasa wekeni mipango itakayowapa wananchi imani kwamba sera zenu zinatekelezeka either kwa kuwashirikisha kwa vitendo au kuwapa connections muhimu au miongozo itakayogusa maisha yao.
Hakuna nchi nyepesi kuongoza na ngumu kuongoza kama Tanzania, ila kizuri na rahisi ni kwamba wepesi wa kuwaongoza watanzania unatokana na mahusiano ya kidugu mtakayokuwa mmeyajenga .
Msikurupuke mkawageza chama tawala CCM. Wenzangu hawa wana pa kusimamia tena sio padogo.... hawa wana cha kusemea sababu ndio wenye serikali na ndio watekelezaji wa mipango ya serikali.
Ingieni gharama kujenga vyama vyenu leo na baadae vyama hivi vitawajenga ninyi.
Halafu msilalamike kwamba hamna pesa ya kufanya mambo ya msingi sababu hata hayati Mwalimu Nyerere na Karume hawakuwa na pesa lakini walieweza kujenga vyama imara vilivyowaondoa wakoloni na vinavyowasumbua wapinzani hadi leo
Kama kweli mko kwaajili ya maendeleo ya taifa Amkeni ndugu zangu. Mkiendelea kufanya kilekile kinachowakoseshaga kila uchaguzi mtaendelea kukosa ushindi milele.
Rais wetu na mwenyekiti wa chama tawala ameshawaambia msisubirie msisubirie 2025 anzeni sasa. Mkumbuke pia na yeye ameshaanza kutetea kiti
Upinzani kwa afya ya taifa💥
Mungu ibariki Tanzania😍🇹🇿🤝