Vurugu mitaani Mwanza kati ya wamachinga na polisi

Vurugu mitaani Mwanza kati ya wamachinga na polisi

Vibanda vya machinga makoroboi?sio kwamba wanatandaza bidhaa chini?

Pamoja na kutandaza chini lakini pia huwa wana vibanda vya muda pembeni kwenye kuta za yale majengo ya Wahindu! Waondoke bwana waache vile vibanda vya kudumu vifanye kazi! Wewe unakabwa mpaka mlangoni utafanyaje biashara?
 
hawa POLISI mbona siwaelewi hapa MWANZA wanaleta vugurugu watu tuna shindwa kufanya shughuli zetu, wamebomoa vibaNDA VYA MACHINGA WAMETULIA SASA nashangaa polisi wamekazana kufukuza watu mjini
 
yaan hii serikali taabu tupu, watu wakijiajiri napo shida.............pale wala hapana tatizo kwsbb watu wanafanya biashara zao kwa utulivu sasa sijui serikali inakereka nn, na sijui waende wapi sasa hawa watu.

Mkuu issue kubwa ni kwamba Wenye maduka wanalalamikia Serikali kwanini wao wanalipa kodi kisha anakuja mtu (mmachinga) anapanga bidhaa nje ya duka lake wakati halipi pango wala kodi, unategemea huyu mwenye duka atauza??

Makoroboi kuna eneo ambalo ni kwa ajili ya wamachinga na wanaruhusiwa kupanga bidhaa zao. Sasa basi wamachinga wengine wamevamia hata eneo ambalo sio la kwao na hata mbele ya maduka.

Hapo ndipo mgogoro unapoanzia!
 
Umeona eeh, yanakimbia hovyo tu, kinachoniudhi hayo mabomu mengine wanayapiga hata sehemu ambayo hakuna kikundi cha watu wala nini, nadhani wanayo mengi inabidi wayatumie hadi yaishe leo

Nilichogundua hawa askari wetu ni waoga ile mbaya, japo wamesheheni silaha kibao lakini ukiona speed wanayopita nayo wakati wakirusha mabomu, utashangaa mwenyewe. Sasa najiuliza, wewe ni mjeshi na una siraha, mbio zote za nini wakati unaepambana nae ni raia tu na hana hata rungu!?
 
yaan hii serikali taabu tupu, watu wakijiajiri napo shida.............pale wala hapana tatizo kwsbb watu wanafanya biashara zao kwa utulivu sasa sijui serikali inakereka nn, na sijui waende wapi sasa hawa watu.

Kuwaacha pale Mkuu maanake Wenje anafunga 3-0! ndo maana magamba hayataki kusikia habari ya machinga kubaki mjini! Ila kwa makoroboi mji unachafuka sana! Wacha wahamie mlango mmoja bwana, mbona kuna eneo kubwa tu la biashara?
 
hizi habari kuwa JWTZ wapo mtaani ni za kweli?
na wametangaza raia wote watoke mjini?
 
Duh.... Ni balaa nusura ya mkosi....

Inasemekana kuna jengo limechomwa moto, ngoja tufatilie!!

Umesalimika lakini huko?

Sisi tuko nje ya mji,nyie mlioko huko sijui kama ni salama!
 
Hawa askari wetu wapewe mafunzo sio kila mahali nikupiga mabomu. Niko hapa ppf ofcn kwangu lakn chakushangaza nashuka hapa chin nakuta kamata kamata na mabomu yasiyokua na msingi . Askari wetu mnakera sana tena sana.
 
Wapigwe tu, hao ni wakwepa kodi. Kwanini mimi nilipe kodi wengine wasilipe kupitia umachinga? Hao ni wahujumu uchumi. Mnataka uchumi wa nchi uteketezwe na machinga badala ya kuwa na investments kubwa mijini? Hivi kila kijana akiwaza umachinga, tutakuwa na taifa la aina gani?
ni kweli mkuu wanakera sana,utaratibu sharti ufuatwe!
 
Hawa askari wetu wapewe mafunzo sio kila mahali nikupiga mabomu. Niko hapa ppf ofcn kwangu lakn chakushangaza nashuka hapa chin nakuta kamata kamata na mabomu yasiyokua na msingi . Askari wetu mnakera sana tena sana.

Hhaaaaa... Usinambie tuko Jengo moja? Afu kama nakustukiaga nikuja hapo ofcn kwako!
 
Back
Top Bottom