Neno makoroboi linatokana kweli na mafundi koroboi waliokuwa hapo miaka mingi nyuma, baadaye walianza kuingia wafanyabiasahara wa nguo za mitumba ambao walihamishiwa eneo la Mlango mmoja (Langolango) miaka ya 90 (1990s). Eneo linalozunguka maeneo hayo kumekuwa na maduka miaka yote hiyo. Kwa sababu ambazo mimi naziita ni za kisiasa Wenje alianza kuwatetea wafanyabiashara wamachinga wauze bidhaa zao bila kubughudhiwa ndipo kidogo-kidogo wakaongezeka na sasa wamefurika wakiuza bidhaa mbalimbali zikiwemo zile zinazouzwa na wenye maduka kuzungukia eneo hilo. Kama miezi mitatu au miwili hivi kulitangazwa kuwa wafanyabiashara wenye vibanda kandokando ya barabara na wale wa makoroboi waondoe biashara zao kwa vile sio biashara rasmi yaani hazijasajiriwa. Wenje amekuwa akisisitiza kuwatetea kupitia chama chake na ubunge wake. Lakini kinachoonekana ni unafiki ni kujifanya hajui kinachoendelea ilhali yeye ni mbunge na maamuzi ya jiji anayafahamu, lkn anajiinua mbele ya hadhara na kusema anawatetea n kuwa wanaonewa. Wenje anafahamu jinsi Eneo la makoroboi lilivyokuwa halina msongamano wa ajabu kabla hajawa mbunge na kutoa kauli zake. Wenje anapaswa kujua lile sio eneo la soko kama anavyotaka kuwaaminisha watu. Wamachinga wamepewa maeneo ambayo Wenje anajua wamekataa kuhamia ikiwemo eneo la Kiloleli, Sabasaba, nk. Watanzania tuwe wakweli tusiangalie upande wa kujidai kutetea Wamachinga wakati ukweli ni kuwa tunawadanganya na hatuwapi mbinu sahihi za kufanya.Kama waliokuwepo Makoroboi walihamishiwa Langolango, na wamejaa wengine wanataka watengewe eneo, hatuoni sasa utakuwa ni mchezo wa kujikusanya hapo na kudai watengewe eneo?