Kibaha: Wanaodaiwa kuwa ni Polisi wavamia usiku wa manane na kuwakamata wananchi, watatu hawajulikani walipo

Kibaha: Wanaodaiwa kuwa ni Polisi wavamia usiku wa manane na kuwakamata wananchi, watatu hawajulikani walipo

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,035
Reaction score
3,206
Wakazi wa eneo la Lupaso, Vikawe wilayani Kibaha mkoani Pwani wameingiwa na hofu baada ya watu wanaodaiwa kujitambulisha kuwa polisi kufanya operesheni ya usiku na kuwakamata baadhi ya wananchi, siku nane tangu kutokee vurugu zilizohusishwa na mgogoro wa ardhi katika eneo hilo.

Tukio hilo limetokea majira ya saa 8 usiku kuamkia leo Mei 14, 2026 ambapo watu kadhaa walichukuliwa bila maelezo ya wazi kuhusu wanakopelekwa.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Vikawe, Shaban Ally Shaban, amesema jumla ya watu 13 walikamatwa katika operesheni hiyo, lakini baadaye watu 10 waliachiwa huku watatu wakichukuliwa na watu hao bila taarifa rasmi.

Amesema hadi sasa uongozi wa mtaa haujui sababu za kukamatwa kwao wala walikopelekwa, jambo lililoibua taharuki kwa wananchi wa eneo hilo.

Akizungumzia hali ya usalama baada ya vurugu za Mei 6, 2026, mwenyekiti huyo amesema wananchi walikuwa wamejipanga kuimarisha ulinzi wa maeneo yao kufuatia mgogoro wa muda mrefu wa ardhi kati ya wakazi wa Vikawe na familia ya Juma Ngololo inayodaiwa kumiliki eneo hilo kihalali.

Uongozi wa mtaa sasa unapanga kwenda Makao Makuu ya Polisi Mkoa wa Pwani ili kupata taarifa rasmi kuhusu watu hao watatu walioondolewa wakati wa operesheni hiyo.

Juhudi za kulitafuta Jeshi la polisi zinaendelea, kupata undani wa taarifa hii

Chanzo: EATV
 
Inavyoelekea huyo aliye organize ule uvamizi na kuvunja nyumba za watu akiwa na watu waliojaa coaster 4 ana nguvu sana
 
Nafikiri RPC/OCD atakuwa na majibu

Utaratibu upo wazi kabisa, pale mtaani kuna mwenyekiti wa mtaa/mjumbe wa shina, wangepewa taarifa kuhusu hiyo operesheni ili kuondoa taharuki kwa wananchi
 
Nafikiri RPC/OCD atakuwa na majibu

Utaratibu upo wazi kabisa, pale mtaani kuna mwenyekiti wa mtaa/mjumbe wa shina, wangepewa taarifa kuhusu hiyo operesheni ili kuondoa taharuki kwa wananchi
Haya mambo (MB) Simbachewane ndio alikuwa hataki na alikuwa anataka yafanyia kazi. Ila bahati nzuri nchi yetu haitaki watu smart
 
Haya mambo (MB) Simbachewane ndio alikuwa hataki na alikuwa anataka yafanyia kazi. Ila bahati nzuri nchi yetu haitaki watu smart
Watawala wa nchi hii ndo hawataki watu smart. Yaan nchi inaendeshwa kibabiloni
 
Haya mambo (MB) Simbachewane ndio alikuwa hataki na alikuwa anataka yafanyia kazi. Ila bahati nzuri nchi yetu haitaki watu smart
Utaratibu upo wazi kabisa lakini hakuna taarifa inatolewa ili kuondoa sintofahamu kwa wananchi

Kuna kamati ya usalama ya Kata, lakini hata hao pia huoni wakipewa taarifa

Ni kuzua mkanganyiko kwa Wananchi tu
 
Protocal za kiutendaji zimeisha vunjwa zamani sanaa, sasa hivi kila mtu anajiendea tu
 
Haya mambo (MB) Simbachewane ndio alikuwa hataki na alikuwa anataka yafanyia kazi. Ila bahati nzuri nchi yetu haitaki watu smart
Nadhani tunakosea sana tunapoweka matumaini yetu kwa viongozi wale tunaodhani ni wazuri. Bila sisi hawawezi kufanya lolote. Samia anadharau wananchi kweli kweli na anaamini kuwa hawawezi kumfanya chochote kwa sababu ya vyombo vya dola alivyonavyo. Kwa kilichotokea 29/10, Samia kama angekuwa anaogopa wananchi, ujinga kama huu usingefanyika sasa hivi ambapo nchi iko kwenye sintofahamu kwa sababu wangeogopa riot kulipuka. Lakini kinyume chake ndiyo kwanza wanafanya nyodo kali na kuzidisha ujinga wa kila namna. Bila wananchi kuungana, hakuna namna tutatoka hapa.
 
Unachosema ni kweli, kwasababu viongozi wenyewe pia wapo limited kufanya mambo hata kama wana dhamira nzuri ( wanafunikwa na maovu na uovu ). Nachofahamu kila jambo huwa lina kikomao, hakuna alietegemea kama ingetokea siku watanzania wakaamu kujitoa kama 29 October, ni hivyo pia wanaweza kushangaza pia katika mda ambao hawatozania
 
Hakuna protocol ya uongozi nchi inaongozwa kwa utashi wa mtu MOJA.USALAMA WA TAIFA NAO WAMEKUWA WATUHUMIWA NAMBA MOJA
 
Huko mambo yanaendeshwa kihuni sana

Ova
 
Pole yao, ndio utawala tulio nao kwa sasa...MABAVU.

Ila hao wananchi nao wamepoa sana, wangeendeleza pale walipoachia, hao wanajiita polisi wa saa nane za usiku ambao hawafuati taratibu, walitakiwa waokotwe makorongoni.

Huu ujinga ni nadra sana kuusikia kwa watu wa huko Chugga.
 
Back
Top Bottom