Vurugu mitaani Mwanza kati ya wamachinga na polisi

Vurugu mitaani Mwanza kati ya wamachinga na polisi

Mu-Israeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 21, 2012
Posts
2,454
Reaction score
975
Mwanza kuna vurugu kati ya wamachinga wa soko la Makoroboi na polisi.
Mabomu ya machozi yanapigwa sasa.

======Updates======

Mh. Wenje akiwa bungeni ameuliza swali la dharura na amesema kuwa sasa hivi Mwanza hali sio shwari tena maana mabomu nayapigwa kila sehemu.Maduka jijini Mwanza yamefungwa kwa siku ya leo katika operesheni ya kuondoa machinga mtaa wa Makoroboi.

Ameomba pia serikali kuweka mipango madhubuti kwa wafanyabishara ndogo ndogo (Machinga) ili wapate sehemu ya kufanyia biashara.

Ameomba serikali kusitisha hiyo operesheni mara moja na muafaka wa swala hilo upatiwe ufumbuzi na wizara husika ya viwanda na biashara.

Mh. Lukuvi amejibu swali la dharura kwa kusema, Amesema ni kweli jambo hili limetolewa humu ndani na bado serikali inakusudia kutoa taarifa, anasema mh waziri mkuu alitoka bungeni na kwenda kuongea na wahusika na watachukua hatua kwa ishu ya Mwanza kutafta ukweli wa hali halisi na pia hawawezi kusimamisha operesheni hiyo kwa kauli wakiwa bungeni.Mhe Amekuja bungeni kupiga kura na anaendelea kushughulikia hili jambo.

attachment.php


attachment.php


attachment.php
 

Attachments

  • mza4.JPG
    mza4.JPG
    31.3 KB · Views: 5,737
  • mza6.JPG
    mza6.JPG
    25.1 KB · Views: 5,668
  • mza 1.JPG
    mza 1.JPG
    26.9 KB · Views: 5,938
Duh.... Ni balaa nusura ya mkosi....

Inasemekana kuna jengo limechomwa moto, ngoja tufatilie!!
 
Kwa mujibu wa Mbunge Wenje akiomba mwongozo bungeni, amesema kuna fujo kubwa kati ya Polisi na wamachinga eneo la Makoroboi na kwamba mabomu na risasi vinarindima.
Please aliyepo eneo la tukio atupashe nini kinaendelea hapo?


Sent from my iPad using JamiiForums
 
Nimemwona mh.Wenje akiomba mwongozo kwa spika kuhusu vurugu hizo.majibu ya spika:mh,Wenje huwezi kuniongoza mimi kuhusu serikali...katibu endelea...
 
Mabomu ya machozi yanapigwa kila kona ya mji kufuatia bomoa boma ya vibanda vya machinga eneo la makoroboi. Ilikuwa nifanye shooping hapa kabla ya kuendelea na safari yangu lakini naona haiwezekani. Huu utawala wa kibabe siku moja utatufikisha kusikostahili.
 
hivi hiyo makoroboi inashida gani!kila kukiwa na fujo mwanza zinaanzia hapo!!!kwa nn wasiwaache vijana wachape kazi bila bugudha!!
 
Kwa mujibu wa Mbunge Wenje akiomba mwongozo bungeni, amesema kuna fujo kubwa kati ya Polisi na wamachinga eneo la Makoroboi na kwamba mabomu na risasi vinarindima.
Please aliyepo eneo la tukio atupashe nini kinaendelea hapo?


Sent from my iPad using JamiiForums

nipo mwanza mjini vizano hotel na nilikuwa nasafari yakwenda NBC nimeshindwa kutoka hotelin kwasababu ya mabom

yanayo endelea kat ya machingana polisi
 
Vurugu siyo kubwa kiasi hicho, ninachokioa ni polisi wakitumia vibaya kodi zetu kwa kupiga mabomu hovyo hovyo. Mimi nilikuwa safarini nikaamua kufanya hovyohovyo. Haya nimatumizi mabaya ya kodi zetu.
 
Vibanda vya machinga makoroboi?sio kwamba wanatandaza bidhaa chini?
 
Majibu kama haya ya spika ndiyo serikali inapata nguvu ya kufanya wafanyavyo
 
Bajeti yetu ya wizara ya mambo ya ndani imetengwa prss nyingi kununulia mabomu na si kuboresha maslahi ya hao wapiga mabomu.Tutashuhudia sana upigwaji wa mabomu pasipo hitajika hayo mabomu kupigwa.
 
haii ndo tz bana..kila ukijaribu kujikwamua kiuchumi unavutwa shati..cjui wanataka vijana tuende wap..
 
Vurugu zinaelekea kutulia sasa.
Sababu ya vurugu hizo ni kuvunjwa kwa vibanda vya wamachinga usiku wa kuamkia leo.
 
Nimejaribu kutafuta hasa chanzo cha hayo kwa kuongea na wenye mduka hapa mjini. Inasemekana waliwahi kondolewa kipindi cha nyuma. Tatizo ni kuwa baada ya kuondolewa baadae kuna walopewa vibali kinyemela ktk eneo hilo hilo walilo fukuzwa wengine. Hali hii ilipelekea wwle wqliofukuzwa kurejea. Haya kwangu mimi ni matumizi mabaya yq madaraka, kama tumeamua kuzuia machinga kufanya biashara flani then tumaanishe tunachokifanya, siyo leo unamzuia huyu, halafu kesho unampatia huyu eneo lile lile.
 
Nilikuwa hapo barclays yaani ni hekaheka, kwa mara ya pili leo na nawa uso sababu ya mambomu ya machozi, yaani ni balaa. Mji mweupe hakuna kinzhoendelea zaidi ya polisi kupiga mabomu ya machozi

Mwanza kuna vurugu kati ya wamachinga wa soko la Makoroboi na polisi.
Mabomu ya machozi yanapigwa sasa.
 
Ningejua upo hapo, ningekuja kukupa hi, nimeshatoka town CHAMIlady kamsalimie Mashimba1 hapo miti mirefu ila sijui utapita wapi manake kila kona ni difenda za polisi tu na mabomu yao

Charming lady, uko wapi nikusalimie. Mimi nipo hapa karibu ni stabd ya mohamed trans. Ila nipo safarini, baada ya muda naendelea na safari yangu.
 
Last edited by a moderator:
Katikati ya mji sasa kimya kabisa, maduka na shughuli nyingine nyingi zimesimama kabisa.
Wamachinga wamefunga barabara.
 
Back
Top Bottom