Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Aiseeh.. Vodacom,kwenye swala la kukomba data nimewaelewa, yaani 1GB yenu, Ni sawa na 500MB mwingine.Mabando yenu mmewekea hamira.
 
Vodacom huu utapeli mnaoufanya mie siwezi kuvumilia.. Mmeninunulisha kifurushi cha Jau mmeandika dakika 245 voda kwa voda na 240 mitandao mingine, nashangaa nimenunua nimepata dakika za voda tuu.. Ushahidi ninao, naomba kurejeshewa salio langu..
 
Habar, ninaomba kufaham namna naweza kununua hisa za vodacom au jinsi ya kupata taarifa kuhusu uuzaji na ununuzi wa hisa za vodacoma tafadhali
 
Kwa nini mtu ukiweka vocha ya kukwangua kama niya 500 inakatwa yote wakati hakuna huduma yoyote mtu alishawahi jiunga na hapo hapo akipiga ile huduma kwa wateja namba 100 mnamwekea aongee na kompyuta recoded yenu hadi anakata tamaa anashindwa kwa kusikilia masharti yenu alafu mwishoni maelezo yanakatika?huo wizi mtauacha lini?
 
Nimetuma pesa kutoka HALOPESA kwenda vodacom kimakosa,

Halotel wamesema hawana uwezo wa kuirudisha, ila tuu watanisaidia kutuma taarifa kwenu.

Mimi ninachotakiwa niongee na nyie muirudishe HALOPESA.

Sasa hakuna option ya kuongea na huduma kwa wateja kwenye namba yenu ya 100
Tuma namba hizo
 
Ndugu mteja,

Una tatizo lolote unapotumia mtandao wetu? Una ushauri wowote ili tuiboreshe huduma yetu?

Tafadhali itumie mada (thread) hii ili tukusaidie kwa urahisi.

Unapokuwa na tatizo, ili tukusaidie kirahisi zingatia haya:

- Ni tatizo gani? (M-PESA, SMS, Calls, Internet, usajili, kukatika kwa mawasiliano n.k)
- Maeneo gani? (Tukifahamu location, inakuwa rahisi kukuelekeza wapi uende ili upate physical assitance toka kwa vendor wetu aliye karibu nawe)
- Tatizo limeanza lini na limejirudia au kuendelea kuwa kero kwako kwa muda gani?
- Kama ni ushauri, zingatia ya juu lakini tutafurahi tukijua kwanini unapendekeza unachopendekeza
- Kama ni pongezi, zingatia ya juu na tungependa pia upendekeze lipi tufanye kuzidi kuiboresha huduma kwako.

Karibu

Vodacom Tanzania
bei za vifurushi vyenu si rafiki kwa ya maisha ya watanzania wa sasa ndo maan weng tumekuja na kampen ya hamia mtandao fulan🤣🤣
 
Screenshot_20200922-144352.png
vodacom hampo serious, yn mnanidai mnaniongezea deni kwa kuchelewa kulipa deni kwa wakati halafu bado mnaniambia nikope tena na mmenizidshia kiwango cha kukopa
 
Aisee kwa kama siku 3 au 4 binafsi sielewi kabisa access internet ya Vodacom imekuwa slow, unstable na inakata mara kwa mara hasa mida ya jioni. Kiulweli nina bore sana hsdi najilaumumkwa nn naendelea na huu mtandao.
Naamini hiki ni kilio cha wengi, amkeni vodacom.......
 
Habari poleni na majukumu ya kijenga Taifa nina ushauri kwa kampuni ya voda kama ifuatavyo: Kuna sehemu inaruhusu kumnunulia rafiki yako kifurushi au intetnet n.k.

Ushauri wangu ongezeni au niwe free kumtumia kifurushi chochote kile sio kama sasa ambapo ninaruhusiwa kumtumia vifurushi vichache tu kwa mfano nikitaka kumtumia kile kifurushi cha DAR UN haiwezekani.

Tafadhali jaribuni kulifanyia hili itasaidia sana kwa wateja wenu kumnunulia kifurushi au salio lolote ninalohitaji kama mimi ninavyoruhusiwa kununua chochote kile.

Hii itasaidia kwa sababu mwingine ukimtumia ajiunge mwenyewe huwa hawezi badala yake atatoa pesa na kufanyia kitu kingine wakati dhumuni langu ajiunge kifurushi.
 
Voda mi nilisha washindwa kwa kweli,hasa ukipiga simu kipokee kidada,unakielekeza hivi kinataka hivi,mwisho kwa sauti ya puani,"asante kwa kutumia Voda"na shida yako hajaimaliza
 
Back
Top Bottom