Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Imenuma Sana kukuta kifurushi cha Sms 2000 na walianzaga na shilingi 1000 mwanzon kabisa yaani ni ongezeko la asilimia 100 ndani ya kipindi ksicho zidi mwaka mmoja
 
Acha kudandia train kwa mbele. Hujaelewa unakimbilia kureply
Nmekuelewa sana hata hicho ulichosema kimenitokea kifurushi cha 2000 cha sms wiki hupati insta.

Lengo kilikuwa si kukujibu wewe nimemquote mtu sijui kwanini niposend quote haikutokea
 
Voda majizi sana,ukinunua umeme kwa luku wanasepa na Tshs 50! Ukijiunga kifurushi cha week dakika 73, kupiga mitandao yote wanaiba dakika!! Kuna kipindi nilipiga simu, kucheki salio dakika 67, nikakaa bola kupiga simu, kuja kucheki salio washasepa na dakika 10!!

Hawa niwajizi sana!!
 
Mimi nilipata tatizo upande wa MPESA na ilitakiwa hela irudushwe katika account yangu baada ya wakala kusema hakua na salio la kutosha, customer service wakadai nisubirie masaa 72(siku 3) ili pesa irudishwe kwangu ilirudishwe baada ya siku 4 tena baada ya kwenda makao makuu, kiukweli nilichukizwa sana na hili ila ilikua ni ya muhimu sana maana nilikua na mgonjwa mmeniweka siku 4 kusubiria na mambo yangu kusimama, kiukweli mbadilishe utaratibu wenu kwani mtapoteza wateja kwa jambo hili la kusubiria muda mrefu na pesa ni yangu mwenyewe ikawa kama nawaomba tena...
 
Voda mna nini?

Nimelipia king'amuzi cha DSTV toka jana sijapata sms ya muamala kukamilika wala fedha kutumwa DSTV na niliangalia salio mmenikata hela na nikiwapigia simu haipokelewi naombeni mrudishe hela yangu
 
Mimi Nikiwa kama mteja wenu wa muda mrefu naombeni msaada wenu usiku wa rarehe 19 mwenzi wa Tatu mwaka huu niliibiwa com yangu sina ya tecno j7 niliripoti polisi na rb ninayo nilikuwa naombeni msaada wenu je ili niweze kuipata com yangu nifuate taratibu zipi na gharama ni kiasi gani? Number za imei number ninazo
Com ndio nini jamani?
 
Kwa upande wangu wameniboa sehemu moja nene tu.
Nilikua na ofa inayoitwa "YA KWAKO TU" ambapo kwa takribani mwaka mzima nimekua nalipa 2000/- kupitia *149*03# napata GB 3 kwa siku tano ambazo zilikua mujarabu kabisa kwa matumizi yangu ya data. Kwa sasa wameondoa na kupandisha bei. Wameniboaje?
Tabia ya kuondoa au kubadilisha bundle hizi vodacom ndo zao.
 
vodacom vifurushi vya yakwako mmepunguza MB kutoka mb 200 hadi 25 sio sawa mnatuonea sana wateja wenu,sinunui tena vocha zenu hamnipati
 
Mimi nilishaachagaa kutumia mtandao huo toka 2011 sasa nyie sjui kwann mnakomaliaa wakt mnaibiwa
 
Voda nilinunua bunddle ya mb 500 nikatumia dakika kumi tu mtandao ukazingua mpaka ika expire kisha wakaomba radhi na kunipa mb 50 ila waksema nijiunge na kijiweni,baada ya kwenda kijiweni hapakuwa na huduma kabisa ndo nikawa nimeibiwa 0762471807
 
Vodacom kuna SMS za habari kutoka kwa MATUKIO mnanitumia kila mara..sizitaki nilishakasirika hadi nataka kutafuna line nzima nzima.

Please wambiane wasinitumie wananiboa sana midnight unasikia SMS kusoma eti eti watatu geita wazimia kwa kunywa pombe. Sasa hii Mimi inanihusu nini..arrrgh! Sitaki!
 
Kiukweli matatizo mliyonayo ninyi wenye hii kampuni ni mengi mno, mara kwa mara tunawaeleza matatizo yaliyopo lakini hamna msaada wowote ule! Napenda kuwakumbusha machache kati ya hayo mengi, neti yenu ni yenye mwendo wa kinyonga hada eneo hili nililopo mm hapa kwenye huu mnara wa Maisome island, Tafadhalini sana ongezeeni nguvu ya mtandao. (2)Kuna nyakati kadhaa tunaweka salio na kuchagua bando,cha hajabu ukitaka kuwasiliana tu, ndipo tunaelezwa ya kwamba kuna tatizo! baada ya muda tena tunaambiwa salio limeisha! (3) Endapo tunaweka muda wa maongezi bila ya kijiunga, basi hiyo pesa mnaikomba kidogo kidogo na hata kama ni zaidi ya tshs:5,000/=itaisha yote hata kama nikiwa nimezima data!

NINACHOAMINI VODA NI WEZI MLIO ALALISHWA NA SERIKALI!
 
Nimekuwa nikikatwa fedha kwa ajili ya m-paper kwa zaidi ya mwaka wakati Mimi sijajiunga na huduma hiyo.

Nimewapigia customer care mara kadhaa pasipo mafanikio naomba msaada wenu namba yangu 0754811220
 
Back
Top Bottom