Vitu vya kuzingatia unapopewa Lifti

Vitu vya kuzingatia unapopewa Lifti

Hahahaha namjengea picha mpewa lift naona katulia zaid ya mnyolewa..!
 
Wengine wakipewa lift wanataka kupiga hadi honi, usumbufu tu.😀
 
Hiyo namba12 duuuh!! Kwani mimi nimechangia kwenye makosa yake?
Ulikuepo ndani ya gari lake.....Changia chochote kuonesha unajali na sio shuruti...Ukimsaidia atakukumbuka daima
 
tehe tehe tehe hajui kula na kipofu huyo, sasa hivi ataweka budget ya usafiri

Alishanunua gari tayari, nakumbuka kuna siku nimemwomba nitoke na gari lake make nilikuwa sina gari siku hiyo, basi nikapiga route mafuta yakashuka sana, nilivyomrudishia akaanza kumind nimpe hela ya mafuta nikamchomolea.

Akawa kila tukionana ananikumbusha, ikabidi nimwambie dogo acha ufala, umewahi kutoa hela yoyote ya mafuta nilipokuwa nakupa lift? Ikabidi awe mdogo tu.
 
Ulikuepo ndani ya gari lake.....Changia chochote kuonesha unajali na sio shuruti...Ukimsaidia atakukumbuka daima
Waiiii!! Kwahiyo nisingekuwepo asinefanya hayo makosa? Kama ambavyo vingine vimekatazwa na hilo likatazwe pia.
 
Unapokuwa umepewa lift katika gari zingatia mambo yafuatayo:-

1. Usiwe busy sana na simu, tablet au kifaa kingine chochote cha ki electronic ulicho nacho kwa wakati huo. Watoa lift huwa hawapendi.

2. Usipende kukimbilia seat ya mbele, vinginevyo uwe umeelekezwa kufanya hivyo.

3. Usilisifie gari lililo mbele au nyuma au gari lingine tofauti na ulilopewa lift.

4. Usimuulize aliyekupa lift habari ya eti safari yake inaishia wapi. Si swali zuri kwa muomba lift.

5. Usimpe maelekezo yeyote mtoa lift. Kwa mfano, kumwambia aongeze kasi. Au awashe ama kuzima AC.

6. Usimpe dharura yako binafsi, mfano, samahani kaka simama kidogo pale ninunue mboga.

7. Usimwombee lift mtu mwingine mbele ya safari.

8. Usipende kulakula vitu kama karanga, korosho au pipi, baadhi ya watoa lift huwa hawapendi.

9. Usifanye maongezi yanayo ashiria kuwa wewe ni much know.

10. Kama unapendelea sana singeli au bongo fleva na muda wote mwenzio ana piga gospel, just keep cool and think clear, if possible make the most of it.

11. Ikitokea gari limepata matatizo ya kiufundi(technical difficulties) usimwache aliyekupa lift mpaka gari liwe sawa mwendelee na safari.

12. Aliyekupa lift akipigwa faini na traffic changia japo nusu ya faini.

13. Usiongee lugha ambayo mwenzio haijui hasa pale unapowasiliana ukiwa ndani ya gari ulilopewa lift.
14. Usimwelezee shida zako. Msaada wa lift unakutosha.

15. Control jicho lako uangaliapo vitu vya nje na comment zako kwa ulivyoviona.

C&P
 
Sio kwamba unazuiwa ila ni kwamba unapoona vitu vya ajabu au vya kushangaza..kushtusha...usihamaki au kuogofya kias kwamba ukamchanganya na dereva aliyekupa lift...Kuangaliwa nje haikatazwi Honey Faith
Hapana bwana.Halafu eti kuchangia pesa akipigwa faini mie hata gari sijui kiendesha wala sheria zake naanzaje kuchangia pesa na mbaya zaidi eti usiongee lugha nyingine mie imetokea nimepigiwa na bibi tunaongea zetu kikurya nitaikata simu kisa lifti?
 
Hapana bwana.Halafu eti kuchangia pesa akipigwa faini mie hata gari sijui kiendesha wala sheria zake naanzaje kuchangia pesa na mbaya zaidi eti usiongee lugha nyingine mie imetokea nimepigiwa na bibi tunaongea zetu kikurya nitaikata simu kisa lifti?
Khaaah!! Nitaongea kimasai changu vizuri, nikikukera nishushe.
 
Waiiii!! Kwahiyo nisingekuwepo asinefanya hayo makosa? Kama ambavyo vingine vimekatazwa na hilo likatazwe pia.
Sio sheria kwamba ni lazima ulipie ndugu...kiroho safi na kistaarabu unaweza ukamwambia tu ningekuwa na uwezo ningekusaidia ila tu sina hela..Atakuelewa na haiwagombanishi mbona
 
Mie huwa napata tabu sana pale ninapopewa lift na mdada alafu kavaa kimini. Macho hameumbwa kutazama jamani.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom