Je, unataka kila siku upewe lift? Yafuatayo ni mambo 10 yakuzingatia unapopewa lift sehemu yeyote ile

hannibali

JF-Expert Member
Jul 7, 2020
468
427
Habari za muda huu wanaJamiiForums, natumai na leo muwazima wa afya na mnaendelea vyema kulisongesha life.

Haya kijana wenu kwa mara nyingine tena leo tunakutana hapa tuweze kuongea na jamii kwa pamoja, sasa kuna kitu cha lift hapa tukijadili nadhani ushawahi ata siku moja kupewa lift au kumpatia lift mtu, Basi yafuatayo ni mambo 10 ambayo unatakiwa uzingatie unapopewa lift sehemu yeyote ile.

NB: Vise versa ya mambo yafuatayo yatakufanya usipewe lift tena:

(1) usipende kukimbilia seat ya mbele mara nyingi watoa lift hawapendagi labda kwa ruhusa maalum kutoka kwake. Ukishaingia kwenye gari usibamize mlango kwa nguvu mtoa lift hapendi kwani anaona kama umembamiza yeye.

(2) Ukiingia utulie usishike shike vitu hovyo kama vile kushusha kioo na wala usiwe mtu wa kuongea ongea ovyo, kwa mfano usipende kumpa maelekezo mwenye gari kama vile sijui awashe AC au aongeze speed ya gari" "kauli kama Dah aisee humu gari lako kuna joto sana huku unajipepea,hivi ac haifanyi kazi eeh au wewe joto hulioni"

(3) Usijifanye eti uko busy sana na simu, tablet au kifaa kingine chochote cha kielectronic ulicho nacho kwa wakati huo utulivu wa hali ya juu unahitajika na atakama mwenye gari atakuwa kabeba mtoto wake halafu anakulalia, kuchezeazea sharubu sharubu zako wewe kuwa mtulivu vumilia tu wala usikasirike akiwa anazidisha muulize tu akuhesabie moja mpaka kumi kwa Kiingereza, hapo utakuwa umempa kazi kidogo.

(4) Ukipewa vitu vya kutafuna kama bites wala usipokee wewe sema tu ahsante ubarikiwe sana mkuu na hatakama umeingia na vitu vyako kwenye gari usipende kutafunatafuna ikiwezekana subiria mpaka ushuke ndo ule.

(5) Jiupushe na maswali kama eti umejifunzia chuo gani udereva watoa lift hawapendagi maswali hayo vilevile Usimuulize aliyekupa lift eti safari yake inaishia wapi wewe kaa kimya yeye ndo atakuuliza kwamba unaishia wapi.

(6) Mwenye gari akipigwa pasi na daladala au akimkosakosa bodaboda akaanza mtukana dereva wa iyo daladala au bodaboda unatakiwa utukane kwa nguvu na matusi ya nguoni zaidi ya anavyotukana yeye.

(7) Usipende kusifia gari lililo mbele au nyuma au gari lingine tofauti na ulilopewa lift. Watoa lift sikuzote wanapenda kusifiwa wao, hapa epuka kauli kama "Jamaa gari lake kali halafu new model kabisa afu inatembea kinoma nikipata hela nitanunua kama ile"

(8) Usimuombee lift mtu mwingine katikati ya safari hata kama ndugu yako unakaa nae nyumba moja we kausha tu fanya kama humjui..hapa epuka kauli kama""aisee kaka yangu huyo nakaa nae nyumba moja naomba umchukue aise watoa lift hawapendi dharura zako barabarani."" samahani wewe kaka naomba tusimame kidogo ninunue mboga mara moja""

(9) Usipende kuongea kilugha ukiwa ndani ya lift ikitokea umepigiwa simu ya kilugha mwambie tu nitakupigia baadae. Vilevile, watoa lift hawapendi watu wanaojifanya much know sana vile vidada vinavyochanganya Kiswahili na kiingereza.

(10) Mwisho kabisa chunga sana jicho lako ikiwa mtoa lift ni mdada kwani sometimes wanavaaga vipedo hawapendi kupigwa pigwa jicho utakuwa unamkosesha focus na hatokupa tena lift.

Haya, kazi kwenu tena hapo wanazengo!
 
Kwa yote uliyoandika si bora nitembee tu kwa miguu, I honestly hate lift aisee hata Kama tunaenda njia moja, gari naona huwa ni personal sana, sasa wengi huwa hawapendi watu wapande, Mimi nikiona mtu ana gari najifanya busy mpaka aondoke. Better nichukue Uber.
 
11. Ukiwa Unaomba lift jitenge pembeni na Kama Ni mwanamke hakikisha uwe mrembo
12. Usiwe na haraka kuliko; kwani umemkodi?
13. Saidia kupakia na kushusha mizigo siyo mpaka uombwe hata Kama Ni mkaa!
Namba 13 nakubaliana nalo
 
Back
Top Bottom