Vitu vya kuzingatia unapopewa Lifti

Vitu vya kuzingatia unapopewa Lifti

Unalikuta limtu umelipa lifti halafu lisimu lake linaita mlio mkali, anachelewa kupokea na akipokea anaaza kuzungumza kwa sauti muda mrefu na mazungumzo yake ambayo kwako ni kichefuchefu hayaishi. Nashauri ukiwa mstaarabu hata ukiwa kwenye maonezi na watu simu yako ikiita nenda pembeni kabisa kamalize dharura yako ya mazungumzu kwa privace na utulivu mkuu baadaye rudi ungana na wenzako. Usiwakatishe wenzio wasikilize siri au maujinga yako inaboa
 
Unapokuwa umepewa lift katika gari zingatia mambo yafuatayo:-

1. Usiwe busy sana na simu, tablet au kifaa kingine chochote cha ki electronic ulicho nacho kwa wakati huo. Watoa lift huwa hawapendi.

2. Usipende kukimbilia seat ya mbele, vinginevyo uwe umeelekezwa kufanya hivyo.

3. Usilisifie gari lililo mbele au nyuma au gari lingine tofauti na ulilopewa lift.

4. Usimuulize aliyekupa lift habari ya eti safari yake inaishia wapi. Si swali zuri kwa muomba lift.

5. Usimpe maelekezo yeyote mtoa lift. Kwa mfano, kumwambia aongeze kasi. Au awashe ama kuzima AC.

6. Usimpe dharura yako binafsi, mfano, samahani kaka simama kidogo pale ninunue mboga.

7. Usimwombee lift mtu mwingine mbele ya safari.

8. Usipende kulakula vitu kama karanga, korosho au pipi, baadhi ya watoa lift huwa hawapendi.

9. Usifanye maongezi yanayo ashiria kuwa wewe ni much know.

10. Kama unapendelea sana singeli au bongo fleva na muda wote mwenzio ana piga gospel, just keep cool and think clear, if possible make the most of it.

11. Ikitokea gari limepata matatizo ya kiufundi(technical difficulties) usimwache aliyekupa lift mpaka gari liwe sawa mwendelee na safari.

12. Aliyekupa lift akipigwa faini na traffic changia japo nusu ya faini.

13. Usiongee lugha ambayo mwenzio haijui hasa pale unapowasiliana ukiwa ndani ya gari ulilopewa lift.
14. Usimwelezee shida zako. Msaada wa lift unakutosha.

15. Control jicho lako uangaliapo vitu vya nje na comment zako kwa ulivyoviona.

C&P
THANKS MKUU
 
Ya ziada.
Mwenye gari akipigwa pasi na daladala akaanza mtukana dereva wa daladala unatakiwa utukane kwa nguvu na matusi ya uchungu zaidi ya anavyotukana yeye

akiweka mziki kwenye gari ukaona anatikisa kichwa kuonesha anaupenda mziki unatakiwa utikise kichwa ikiwezekana kuomba asimamishe kidogo gari ili ucheze mziki
ha ahahha
 
Kuna wale wanaozoea lifti mpaka wanalifanya gari la kukodi. Yaani usipowapitia mtaa mzima utajua!!! Yaani mapaka mwenye gari anatamani ahame njia
tehe tehe tehe we acha tu, unaitwa ushoga pilipili, unamsubiria nusu saa, na ole wako umuache, unaringa na gari lake
 
lift ilishawahi kunicost ndugu yangu sina hamu,nilipewa lift ndani ya gari walikuwa mke na mume tena wao walinikuta njiani wakasimama sasa nikawa na mvutano wa nafsi mbili moja inasema watose tu waende zao nyingine inasema jumuika nao tu kuonyesha ujamaa..!1ebwanaee kumbe ile nafsi yenye chembechembe za uungwana ikaniponza kumbe wenzangu kuna mahali wanapita kufika wakaniomba niwasubiri au nijoin nao sasa sikuona kujoin nao kama inamantiki mimi nikawaambia ntabaki kwenye gari,wakani promise hatuchelewi...!!mayowanee nilikaa kwenye gari saa zima yaani mpaka nikajiona kituko nikajuta kwanini nisngeendelea nasafari zangu ningekuwa nishafika home,walivyorudi wakani please ila nikatathimini tu kuwa hiyo pleasing ilikuwa yakunambia ukome kudandiadandia vya watu...!!😕😕😕😕😳😳
ha hahahahaha
 
Asante aliyeanzisha huduma ya daladala huko hakuna mashariti na konda akizingua unamjibu upendavyo kwendraa na vigari vyenu daladala raha sana.

Kuna misemo kibao mara utasikia

abilia: wewe konda ingiza yote
konda: nini hiyo?
Abilia: si mizigo yangu

ahaaaa daladala oyeee
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom