Vitu vya kuzingatia unapopewa Lifti

Vitu vya kuzingatia unapopewa Lifti

Mfano wa kauli hizo;

"Dah aisee humu gari lako kuna joto sana huku unajipepea,hivi ac haifanyi kazi eeh au wewe joto hulioni"

"Jamaa gari lake kali halafu new model kabisa pia anatembea sana si unakumbuka tulimpa ananunua mkaa njiani,sasa ametupita"

"ivi unaishia wapi ikiwezekana unisogeze sogeze mbele kidogo maana naposhukia ni mbali sana na ninapoishi"

"hapa barabara imenyooka sasa unaweza ongeza speed,haha"

"Dah..aisee ndugu yangu huyo naomba umchukue tunaishi nyumba moja"

"hiyo nyimbo siipendi kweli yani huyo jamaa hajui kabisa kuimba,weka zile za akina.....(hapo umetaja jina la msanii)"

Mwisho "loh hili gari lako limepata pancha litanichelewesha kaka nashukuru kwa msaada ulionipa mpaka kufikia hapa wacha mimi niwahi,nikutakie matengenezo mema"
Mkuu unatoaga lift nini
Hahahaaaaaaaa
 
Unapokuwa umepewa lift katika gari zingatia mambo yafuatayo:-

1. Usiwe busy sana na simu, tablet au kifaa kingine chochote cha ki electronic ulicho nacho kwa wakati huo. Watoa lift huwa hawapendi.

2. Usipende kukimbilia seat ya mbele, vinginevyo uwe umeelekezwa kufanya hivyo.

3. Usilisifie gari lililo mbele au nyuma au gari lingine tofauti na ulilopewa lift.

4. Usimuulize aliyekupa lift habari ya eti safari yake inaishia wapi. Si swali zuri kwa muomba lift.

5. Usimpe maelekezo yeyote mtoa lift. Kwa mfano, kumwambia aongeze kasi. Au awashe ama kuzima AC.

6. Usimpe dharura yako binafsi, mfano, samahani kaka simama kidogo pale ninunue mboga.

7. Usimwombee lift mtu mwingine mbele ya safari.

8. Usipende kulakula vitu kama karanga, korosho au pipi, baadhi ya watoa lift huwa hawapendi.

9. Usifanye maongezi yanayo ashiria kuwa wewe ni much know.

10. Kama unapendelea sana singeli au bongo fleva na muda wote mwenzio ana piga gospel, just keep cool and think clear, if possible make the most of it.

11. Ikitokea gari limepata matatizo ya kiufundi(technical difficulties) usimwache aliyekupa lift mpaka gari liwe sawa mwendelee na safari.

12. Aliyekupa lift akipigwa faini na traffic changia japo nusu ya faini.

13. Usiongee lugha ambayo mwenzio haijui hasa pale unapowasiliana ukiwa ndani ya gari ulilopewa lift.
14. Usimwelezee shida zako. Msaada wa lift unakutosha.

15. Control jicho lako uangaliapo vitu vya nje na comment zako kwa ulivyoviona.

C&P
Hiyo No. 12 inahusika pia kama mwenye gari atapitia "sheli"
 
Ya ziada.
Mwenye gari akipigwa pasi na daladala akaanza mtukana dereva wa daladala unatakiwa utukane kwa nguvu na matusi ya uchungu zaidi ya anavyotukana yeye

akiweka mziki kwenye gari ukaona anatikisa kichwa kuonesha anaupenda mziki unatakiwa utikise kichwa ikiwezekana kuomba asimamishe kidogo gari ili ucheze mziki
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom