Vitabu vya Willy Gamba (Elvis Musiba)

wakuu naombeni msaada wenu kama kuna anayejua ninakoweza kupata hivi vitabu ya Elvis Musiba, vikiwa na stellingi Willy Gamba.

Vitabu hivyo ni kama vile:
1.Kikosi cha Kisasi
2.Kufa na Kupona
3.Hofu.
4.Njama
5.Uchu

na vinginevyo. nimevisoma baadhi zamani lakini sasa hivi sina nakala tena ningependa kujua ninakoweza kuvipata.

shukrani!
Jamani si nasikia vilipigwa marufuku hivi vitabu? eti vinafundisha ujambazi?sasa Kaizer unavitakia vya nini?
 
...nakumbuka kipande hiki kama sikosei kwenye kufa na kupona 'nenda rudi salama umefanikiwa, kwenda na mwoneshaji wa mavazi, leo usiku toka uaduini tunamofikiri' acha kabisa novo zile.

vipi kuhusu lile kipande kwenye njama wakati yupo pale bintuman hotel jijini freetown sierra leone akiwa na mrembo veronica na kijana sharrif kisha maselina akamtumia ujumbe uliosema mama mgonjwa sana unatakiwa urudi haraka kisha willy akajua kwa ujumbe huo basi tena likizo ishaharibika bila kujua kuwa veronica na sharrif nao walikuwa ndani ya kamati ya ukombozi

acha kabisaaaaaaaa
 
hapo nakuunga mguuu mkuuu Hussein Chuwa anafata nyayo za akina Musiba na Kiango nimekisoma hicho kitabu kizuri sana , jamaniiiii shigongo anabore na hadithi zake zinazofanana na picha za kinigeria na kisha kujirudiarudia nilikuwa mpenzi wa hadithi zake lakini baada ya kusoma nne tu nikajua jamaaa amefulia huyuuuuu mpaka leo sijagusa hata moja maana naona uzushi tu bora niangalie 24hrs kuliko kuangalia tafsiri za movie za kinigeria

Anaitwa Hussein TUWA,jamaa ni mzuri sana,nami nimesoma Riwaya zake za MDUNGUAJI(The Sniper) na ile ya MKIMBIZI...Ni nzuri sana
 
Hiki cha Hussein ni kile chenye msichana mwenye jina gumu sijui alikuwa akiitwa Tiganini sijui ? alikuwa anafanya kazi kwenye makumbusho sijui au siyo huyo? Wenzie waliuliwa walipokwenda field na yeye peke yake akabakia akiwa na mkanda unaoonyesha mauaji yalivyofanyika mle msituni? Kama ni hicho nakubaliana nanyi ni kizuri nilifanikiwa kukisoma kwa siku mbili kwani utamu wake haukuruhusu nikiweke chini kivivu!

Yule dada anaitwa TIGA MUMBA...Riwaya ya MKIMBIZI ni nzuri sana,ipo nyingine ya MDUNGUAJI(ya huyuhuyu TUWA) nayo ni nzuri sana aisee
 
Duh Hakika mmenikumbusha mbali mno! Je, na kile kitabu cha Allan Quarteman..."Umslopogas na Inkosikazi"
kama ntakuwa nimekosea mtanisahihisha.
 
Miye nkivipata nitavi-design upya, ili vitoke kwa muonekano wa kisasa zaidi. Enzi zile Macintosh hazikuwapo, hivyo PrintPak pekee ndio waliokuwa na tenda za typesetting! Ilikuwa kasheshe!
 
Hivi wasanii weyu kwa nini wasiigize movies za stories kutoka kwenye hivi vitabu!
Maana story wanazo ekti ni mapenzi tuu hazina vichwa wala miguu.
 
Hivi wasanii weyu kwa nini wasiigize movies za stories kutoka kwenye hivi vitabu!
Maana story wanazo ekti ni mapenzi tuu hazina vichwa wala miguu.

Script ya kugeuza kitabu kuwa filamu ataandika nani? Film industry yetu ni ya kuunga unga tu kuanzia kwenye waigizaji, watayarishaji mpaka sisi watazamaji. Hakuna viwango vya kudiriki hata kushindanisha filamu zetu na za nje ya nchi. Kitabu kama kile cha Njama kiliandikwa kwa ufundi mkubwa kiasi ya kwamba kinahitaji uwezo mkubwa sana wa kiutendaji, fedha na teknolojia wa kukifanya filamu la sivyo hatutokuwa tumekitendea kitabu haki
 
Mi nimesoma vitabu vyote vya James Hadley Chase na Erle stanley Gardner. Nimesoma pia vitabu vya Musiba. Kwa kifupi sidhani kam vitabu vya Chase vinafanana hata kidogo na vya Musiba. Chase ni 3W- women, wealth and wine. vitabu vyote vya Chase vinafanana. Mwanamke mzuri anasababisha mtu afanye mambo ya kipuuzi ikiwepo kuiba pesa na mwisho anakamatwa. Willy Gamba ni tofauti vitabu vyote ni kuhusus hujuma ya mabeberu wa kimagharibi.Sidhani kama anaiga hata kidogo, ila kuna jambo muhimu moja. Ukiwa unasoma vitabu vingi unajikuta unakuwa mkosoaji sana wa vitabu na iyo ndo njia inaweza kukufanya kuandika vizuri au kuwa na mawazo mapana. Kwa mfano Tanzania nani mtunzi mzuri kati ya Musiba, Mtobwa au shingongo? ntampa asilimia kubwa Musiba kwa kuwa anjua namna ya kuvutia msomaji kila mara awe anajikuta ameingia kimawazo, Mtobwa na Joram kiango wake kwa kiasi anajitahidi ila ana tatizo moja la kuchanganya mambo mengi. Kuhusus Shingongo, kwanza hana kipaji cha kuandika, analazimisha uku akisaidiwa na majarida yake, ila upeo wake ni mdogo wa ubunifu, na watu wataofurahia uandishi wake hawajasoma vitabu vya waandishi wazuri kama Grisham. Shingongo ana tabia ya uandishi wa kuandika maneno mengi akifikiri kuandika sana ndo uzuri ila hawezi kuunganisha matukio kwa njia itakayo vutia msomaji
 
Msisahau vitabu vya marehemu Eddie Gazel, alikuwa na vitabu kama: File maalum, Jogoo la shamba na vingine vingi
 
Kuna waandishi wengine mahiri sana ambao watu wengi hawawafahamu, mfano mmoja wapo ni Mwandishi ajulikanae kwa jina la Muhamed Said Abdulla a.k.a bwana Msa (Marehemu), ana vitabu kama vile Kosa la Bwana MSA, Siri ya Sifuri, Mzimu wa Watu wa Kale, Kisiwa cha Giningi, Duniani Kuna Watu, Mke Mmoja Waume Watatu na Mwana wa Yungi Hulewa. Vile vile kuna huyu ajuliukanae kwa jina la Said Ahmed Mohamed na vitabu vyake ni Kiza katika Nuru, Utengano, Asali Chungu... Bila kumsahau Mzee Shafi Adam Shafi. Na Vitabu vyake vijulikanavyo kwa majina haya: Kasri Ya Mwinyi Fuad, Kuli, Haini na Vuta N' Kuvute.
 
Mkuu X-P,
Umenikumbusha watu wanaojuwa kutunga hasa, huyu bw. Msa alikuwa kikaa Kikwajuni kule Zanzibar, nimesoma vitabu vyake vina hadithi tamu za upelelezi na ujasusi, kilichonivutia zaidi "mashetani" na "Kisima cha Giningi".

Ama Shafi Adam Shaffi, huyu mkongwe ni gwiji hasa la utunzi...hadithi ya "Kuli" ndiyo iliyonifundisha riwaya ni nini, niliposoma "Kasri ya Mwinyi Fuadi" na " vuta n'kuvute" nikajuwa hasa huyu mzee kiboko sana...hadithi kali sana..."Haini" sijakisoma bado nafikiri alikuwa akitaswirisha na mkasa wa kweli uliomtokezea wa kutiwa ndani baada ya mauwaji ya Mzee Karume mwaka 1972.

Said Ahmed, nilisoma "Asali chungu", hadithi nzuri sana sijapata kuona, sijuwi ni huyu huyu aliyetunga "Nyota ya Rehema" au na ile tamthiliya ya "Kivuli kinaishi" au ni mwengine ila jina ni kama hilo.

Mkuu umemsahau mama mmoja mkali sana kwa riwaya akiitwa Zainabu M. Mwanga, huyu alikuja na riwaya kali sana kama "Hiba ya Wivu" na " Kiu ya Haki", huwezi kuviweka chini vitabu hivyo ukivisoma.
 
Mi nimesoma vitabu vyote vya James Hadley Chase na Erle stanley Gardner. Nimesoma pia vitabu vya Musiba. Kwa kifupi sidhani kam vitabu vya Chase vinafanana hata kidogo na vya Musiba..Sidhani kama anaiga hata kidogo, ila kuna jambo muhimu moja. Ukiwa unasoma vitabu vingi unajikuta unakuwa mkosoaji sana wa vitabu na iyo ndo njia inaweza kukufanya k......vutia msomaji

Mkuu nakubaliana na wewe kwamba vitabu vya Chase hafifanani na vya Musiba.
Lakini je uliwahi kusoma vitabu vya Nick carter? Vitabu vya Musiba havina tofauti na vitabu vingi vya Carter ..... hapo alikuwa anabadilisha majina ya kizungu anaweka ya kibantu ..... !! Scene zote .. kila kitu. katika kitabu labda alikuwa anabadilisha na kuongeza vijisehemu vidogo mno ambavyo kwa uliyesoma hizo Carters unaweza ukajua kabisa ni kitu gani kitatokea kwenye chapter inayofuata.
Kwa hiyo statement yako hapo juu Mkuu sio sahihi..
 
Nadhani Nick Carter alikuwa anawalenga Teenagers kwenye riwaya zake, sawa na mtunzi huyu wa Kimarekani Stephenie Meyer na vitabu vyake vya ki-vampire. Musiba ukimfananisha na watunzi aina ya kina Nick Carter utakuwa umemshushia sana hadhi yake.... Musiba yupo juu zaidi ya Nick Carter... Tatizo yupo Tanzania tu basi.
 
Mkuu nakubaliana na wewe kwamba vitabu vya Chase hafifanani na vya Musiba.
Lakini je uliwahi kusoma vitabu vya Nick carter? Vitabu vya Musiba havina tofauti na vitabu vingi vya Carter ..... hapo alikuwa anabadilisha majina ya kizungu anaweka ya kibantu ..... !! Scene zote .. kila kitu. katika kitabu labda alikuwa anabadilisha na kuongeza vijisehemu vidogo mno ambavyo kwa uliyesoma hizo Carters unaweza ukajua kabisa ni kitu gani kitatokea kwenye chapter inayofuata.
Kwa hiyo statement yako hapo juu Mkuu sio sahihi..
Hapo nakubaliana nawe asilimia 100, ni kweli Musiba alikua aniga kutoka kwa carter. Ila unapokua unasoma vitabu vingi ni rahisi kuwa na mawazo yako na kuunganisha na hadithi ulizowai soma, kumbuka hakuna jambo lipya duniani.
 
Mkuu unaweza kutoa mfano wa riwaya mojawapo inayo fafana na ya Nick Carter!?
 
Nimepokea taarifa zinazosema kuwa,

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa "Tanzania Chamber of Commerce, Industry & Agriculture" (TCCIA) Bwana ELVIS A. MUSIBA amefariki dunia alfajiri ya leo.

Habari za mipango ya mazishi zitafuata mara tu baada ya kupatikana.

Kwa watu walioko London, mnakaribishwa kwa binti yake, Lisa Musiba, anwani ni:

6 MANTON Rd
ENFIELD
MIDDLESEX
LONDON,
EN3 6XZ

Mobile: 07949737185

Pole kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki na wale wote mliofikwa na msiba huu.

Roho ya Marehemu Elvis A. Musiba ipumzike pema.

AMIN.

source: http://www.wavuti.com/
 
hebu nisaidie kujua duka pale bongo ambalo naweza pata hata baadhi ya maandiko haya
 
wakuu naombeni msaada wenu kama kuna anayejua ninakoweza kupata hivi vitabu ya Elvis Musiba, vikiwa na stellingi Willy Gamba.

Vitabu hivyo ni kama vile:
1.Kikosi cha Kisasi
2.Kufa na Kupona
3.Hofu.
4.Njama
5.Uchu

na vinginevyo. nimevisoma baadhi zamani lakini sasa hivi sina nakala tena ningependa kujua ninakoweza kuvipata.

shukrani!
hivi vitabu vinauzwa na wamachinga wewe ukiwaona kule mabarabarani waulize utabahatika. mi lishakutana na mmjo sinza nikammuliza akaniambia vipo na alikuwa ananipigia simu alipovipata.
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom