Vitabu vya Willy Gamba (Elvis Musiba)

Vitabu vya Willy Gamba (Elvis Musiba)

Hahaaaaaa...Ngosha una mambo wewe,namaanisha maji yale ya Wachina kutoka Ziwa Victoria

Hapo nimekusoma ...maana maji ya watu wazima ni larger na maji ya uzima/baraka ni yale ya kwenye squirting! teh teh teh teh
 
Masa. Mdila bwana, ulimolah,
Mchezo wa kukojolea maua acha mzee😀Yaani pamoja na kudundwa mpira bado unaendelea tu?????? Bwahahahahahahah
 
Hahahah unajua tena sisi wengine toto tunduz! Mola sana Nkingwa
 
Elvis Musiba alikuwa mwandishi mzuri wa vitabu vya riwaya...sijui kwanini ameacha hiyo kazi. Kama kuna mtu amewahi kusoma vitabu vya James Hadley Chaseatakubaliana nami uandishi wake unashabihiana sana na wa Musiba, watu wanawasi wasi huenda mzee Musiba alikuwa anafanya tafasiri ya baadhi ya kazi za Chase kwenda kiswahili na mazingira ya kitazania na kuongezea vikolombwezo vya majina ya kibantu. Nimesoma almost vitabu vyote vya Musiba na baadhi ya kazi za James Hadley Chase kama

The Sucker Punch

A Coffin From Hong Kong

Tell It To The Birds

Knock, Knock! Who's There?

A Can Of Worms

na You never know with women

Nashawishika huenda bwana Musiba alikuwa anasoma novel hizi pia na kuzitafasiri......
Pamoja na mtizamo wangu huo bado anabakia mwandishi mzuri wa riwaya aliyewahi tokea Tanzania

Sawa kabisa mkuu..kuna hizi pia:

No business of Mine

I will get you for This

Hand me a Fig Leaf na

Have this one on Me

Umenikumbusha mbali sana muzee...
 
Sawa kabisa mkuu..kuna hizi pia:

No business of Mine

I will get you for This

Hand me a Fig Leaf na

Have this one on Me

Umenikumbusha mbali sana muzee...

Hahahah maisha bwana nakumbuka nikiwa A level unapiga kaptura yako na kitabu cha James Hadley Chase Mfuko wa nyuma, unaenda somesha demu wa Jangwani sekondari....unakariri na vimstari vichache vya kwenye novel ....mpaka somo laeleweka!
 
Yes Masa, JH Chase alikuwa ana vijimaneno flani flani vya kufurahisha sana!

My favourite novels were:

Hit and Run

An Ace up my Sleeve

Just a Matter of Time

Tiger by the Tail and

This Way for a Shroud (Vito Ferrari...)

Nilikuwa Dar last montn naona wameanza ku reprint vitabu vya huyu bwana mkubwa

Hata akama Musiba alikuwa anacopy, bado amefanya kazi kubwa!
 
Hahahaha umenikumbusha Hit and Run ile novel nilimwagiza uncle wangu alipata ka semina UK akaniuliza mpwa nikuletee nini? Nikamwambia Novel ya Hit and Run, maana siku zile hakukuwa na mobile wala walkman ambayo ningemwomba aje nayo. Aliniletea hiyo novel nilitesa nayo sana na mashori......
 
Hahahaha umenikumbusha Hit and Run ile novel nilimwagiza uncle wangu alipata ka seminar UK akaniuliza mpwa nikuletee nini? Nikamwambia Novel ya Hit and Run, maana siku zile hakukuwa na mobile wala walkman ambayo ningemwomba aje nayo. Aliniletea hiyo novel nilitesa nayo sana na mashori......
Teh teh mzee wa Walwa,Inyama na n.o
 
Alikuwa anacopy kwenye baadhi ya scene kwani kuna scene moja kwenye njama inafanana na scene ya kitabu furani cha James Hardley Chase kila kitu.
 
Baada ya kusoma Uchu ambacho amekiandika 2000 nimeondokana na dhana kuwa Musiba/Gamba alikuwa anagandamizia/desa. Kitabu hicho kimetafitiwa kwa kina maana kiko katika muktadha wa mauaji wa halaiki ya Rwanda hivyo ni rahisi kulinganisha matukio ya humo na matukio halisi ya kihistoria.

Kwa ujumla hakuna mwandishi ambaye ni 'orijino' 100%, kila mmoja anaazima kitu fulani kutoka sehemu fulani. Kilicho cha muhimu ni umahiri wa mwandishi - kwa mfano Uchu inaanza na mazungumzo kati ya Gamba na Bosi wake ambao wote wamestaafu, Bosi anamwambia inabidi urudi ulingoni kama George Foreman. Gamba anakataa. Bosi anamwambia kama ni hivyo basi inabidi yeye Bosi aingie ulingoni. Inabidi Gamba akubali kazi maana Bosi ni mzee kupita kiasi hivyo itakuwa aibu kwake kuiachia kazi hiyo ifanywe na Bosi. Sasa hapo utaona kuwa mfano wa Foreman kurudi ulingoni ambalo lilikuwa ni tukio la kweli ulivyotumika kuleta utamu kwenye riwaya hiyo ya Uchu.

Ubunifu ni uwezo wa kuboresha kilichopo.
 
Nakubaliana na wewe Mzizi wa mbuyu,ukiangalia watunzi wa riwaya za zamani kama Msiba,benny mtobwa walikuwa wamelenga kumkumbusha mtanzania wapi ametoka na wapi anakwenda na nini afanye kwa ajili ya nchi yake.Kwa sasa naona aliyebaki ni Hussein Tuwa japo vitabu vyake kuvipata ni kazi.
 
Baada ya kusoma Uchu ambacho amekiandika 2000 nimeondokana na dhana kuwa Musiba/Gamba alikuwa anagandamizia/desa. Kitabu hicho kimetafitiwa kwa kina maana kiko katika muktadha wa mauaji wa halaiki ya Rwanda hivyo ni rahisi kulinganisha matukio ya humo na matukio halisi ya kihistoria.

Kwa ujumla hakuna mwandishi ambaye ni 'orijino' 100%, kila mmoja anaazima kitu fulani kutoka sehemu fulani. Kilicho cha muhimu ni umahiri wa mwandishi - kwa mfano Uchu inaanza na mazungumzo kati ya Gamba na Bosi wake ambao wote wamestaafu, Bosi anamwambia inabidi urudi ulingoni kama George Foreman. Gamba anakataa. Bosi anamwambia kama ni hivyo basi inabidi yeye Bosi aingie ulingoni. Inabidi Gamba akubali kazi maana Bosi ni mzee kupita kiasi hivyo itakuwa aibu kwake kuiachia kazi hiyo ifanywe na Bosi. Sasa hapo utaona kuwa mfano wa Foreman kurudi ulingoni ambalo lilikuwa ni tukio la kweli ulivyotumika kuleta utamu kwenye riwaya hiyo ya Uchu.

Ubunifu ni uwezo wa kuboresha kilichopo.

Mkuu umefanya vizuri kuelezea hili maana wabongo!!
Mimi pia nimesoma kitabu cha UCHU nikiwa na umri mkubwa tofauti na vile vya zamani nilipokuwa mdogo nilikuwa nafurahia zaidi undava wa wahusika, lakini kwenye UCHU nimegundua kuwa mtunzi yule alikuwa hakurupiki kutunga, Uchu ni riwaya inayoonyesha kuwa utafiti wa kina ulifanywa kabla ya kaundika na upeo mkubwa alionao mtunzi, kama hujasoma kitabu hiki soma sasa utaniambia.
 
Unfortunately sipo zanzibar muda mrefu sasa, lakini kama unavitaka kweli Masomo Bookshop, Darajani ni pahala pa uhakika zaidi, unaweza kuwasiliana na Farouk Karim mwenyewe anakuwepo dukani hapo, au unaweza kupata kontakti zake katika Ofisi yoyote ya ITV/Redio One, Dsm hapo,(yye ni mwandishi wa habari wa vituo hivyo), au mwandishi yeyote wa vituo hivyo anaweza akakupatia kontakti zake.Kama utaweza kufika zanzibar, ukifika soko kuu la Darajani, ukimuuliza mtu yeyote wapi Masomo Bookshop kwa Farouk Karim atakupeleka wala si mbali kutoka sokoni.

Asante mkuu, ntafuatilia. Kumbe wewe ni mtu mwema hivi??!!
 
Baada ya kusoma Uchu ambacho amekiandika 2000 nimeondokana na dhana kuwa Musiba/Gamba alikuwa anagandamizia/desa. Kitabu hicho kimetafitiwa kwa kina maana kiko katika muktadha wa mauaji wa halaiki ya Rwanda hivyo ni rahisi kulinganisha matukio ya humo na matukio halisi ya kihistoria.

Kwa ujumla hakuna mwandishi ambaye ni 'orijino' 100%, kila mmoja anaazima kitu fulani kutoka sehemu fulani. Kilicho cha muhimu ni umahiri wa mwandishi - kwa mfano Uchu inaanza na mazungumzo kati ya Gamba na Bosi wake ambao wote wamestaafu, Bosi anamwambia inabidi urudi ulingoni kama George Foreman. Gamba anakataa. Bosi anamwambia kama ni hivyo basi inabidi yeye Bosi aingie ulingoni. Inabidi Gamba akubali kazi maana Bosi ni mzee kupita kiasi hivyo itakuwa aibu kwake kuiachia kazi hiyo ifanywe na Bosi. Sasa hapo utaona kuwa mfano wa Foreman kurudi ulingoni ambalo lilikuwa ni tukio la kweli ulivyotumika kuleta utamu kwenye riwaya hiyo ya Uchu.

Ubunifu ni uwezo wa kuboresha kilichopo.

Mkuu umefanya vizuri kuelezea hili maana wabongo!!
Mimi pia nimesoma kitabu cha UCHU nikiwa na umri mkubwa tofauti na vile vya zamani nilipokuwa mdogo nilikuwa nafurahia zaidi undava wa wahusika, lakini kwenye UCHU nimegundua kuwa mtunzi yule alikuwa hakurupiki kutunga, Uchu ni riwaya inayoonyesha kuwa utafiti wa kina ulifanywa kabla ya kaundika na upeo mkubwa alionao mtunzi, kama hujasoma kitabu hiki soma sasa utaniambia.

wakuu hapo juu karibia mnitoe machozi, ni kweli hata mimi nimesoma UCHU ukubwani, tukubali kuwa Musiba alikuwa na ni kichwa linapokuja suala la uandishi wa riwaya za kipelelezi! Suala la kugandamizia in the strict sense sidhani.

Na muhimu ni ile dhana ya uzalendo...yaani unakuwa inspired kweli kuwa mzalendo kwa nchi yako, ila kwa hali ilivo sasa sijui kama wapo au watazaliwa waandishi wa ki hivi. najiuliza wa sasa hivi watakuwa wanaandika nini kuinpsire kizazi cha sasa?
 
Asante mkuu, ntafuatilia. Kumbe wewe ni mtu mwema hivi??!!

hahaha, Mzizi wa Mbuyu, kwani ulikuwa na wasi wasi na wema wake?

Honestly Junius asante kwa hints, lakini inategemea sana na mtu uwe na contacts zanzibar, lakini nitafanyia kazi hii info, meanwhile kama kuna mtu ana contacts zingine hasa kwa DSM please atuambie,,,
 
Jamani vitabu hivi ndivyo vilivyonifanya mimi mwenzenu nikawa ni mpenzi wa picha, novels e.t.c. za kidetective........

enzi hizo nilikuwaga nafantasize Willy Gamba duh!! acheni tu

Hasa nlipokuwa nasoma Hofu mambo ya Nyaso mtoto wa Arusha
Na Willy alivyokuwa akijua kujifagilia ah!!
 
Mimi wakuu natafuta vitabu vya Juma na Roza kwa ajili ya mwanangu, nilivipenda sana enzi hizo! naweza vipata wapi?

huyu ni juma,
juma ni mtoto,
juma ana dada.
jina lake ni Roza.

Huyu ni Roza,
Roza ni Mtoto,
Roza ana kikombe.
Juma anasema,
Tia chai Roza,
Tia Maziwa,
Tia sukari,
Roza una kiu?
Kunywa chai Roza.

Hehe nakumbuka mistari hii kama kengele za kanisani ktk uzee huu nilionao.

willy Gamba alikuwa favorite readings zangu enzi hizooo. Ila nilisikitika sana kuzuiwa kie kitabu chake cha UHAINI.
 
Last edited:
Jamani vitabu hivi ndivyo vilivyonifanya mimi mwenzenu nikawa ni mpenzi wa picha, novels e.t.c. za kidetective........

enzi hizo nilikuwaga nafantasize Willy Gamba duh!! acheni tu

Hasa nlipokuwa nasoma Hofu mambo ya Nyaso mtoto wa Arusha
Na Willy alivyokuwa akijua kujifagilia ah!!

Eh! Umenikumbusha Nyaso! na mambo ya kininja enzi hizo! Kitabu hiki kinanitoa machozi kwa sababu nimekisoma nadhani in teh early 90s, na kilikuwa cha marehemu mama yangu mdogo (RIP) ndiye aliyekuwa anapenda sana vitabu vya hadithi! Thanks mwanajamiione
 
Back
Top Bottom