Vitabu vya Willy Gamba (Elvis Musiba)

Mzee Musiba alishafariki jamani.
Hakika vitabu vyake vilitufunza ujasiri na udadisi wa hali ya juu zaidi ya yote kujiamini.
Nakumbuka nilianza kuvisoma nikiwa darasa la 6 mwishoni mwa miaka ya 80. Ilikuwa ukipewa kazi wakati kitabu unacho mkononi ni ugomvi mkubwa sana maana hutamani ukiache. Nashukuru nilibahatika kusoma vyote.
Upatikanaji wa vitabu hivyo kwa sasa ni mgumu mno,nimejaribu kuvitafuta sana kwa location nilipo but sijafanikiwa.
Tutaendelea kujulishana namna ya kuvipata.
 
Hiki cha Hussein ni kile chenye msichana mwenye jina gumu sijui alikuwa akiitwa Tiganini sijui ? alikuwa anafanya kazi kwenye makumbusho sijui au siyo huyo? Wenzie waliuliwa walipokwenda field na yeye peke yake akabakia akiwa na mkanda unaoonyesha mauaji yalivyofanyika mle msituni? Kama ni hicho nakubaliana nanyi ni kizuri nilifanikiwa kukisoma kwa siku mbili kwani utamu wake haukuruhusu nikiweke chini kivivu!

Ndio hicho hicho mkuu,hakika ukikianza kukisoma hichi kitabu unaweza kusahau hata kula.
 
Mi mwaka 2006 niligombana na kaka yangu kisa vitabu 2 "Njama" na kingine "kufa na kupona" kisa alimhonga msichana wake!!!nililia sana mana nilikuwa navisoma mara mbili mbili nilikuwa naviita vitabu vya Willy Gamba 2liachiwa na baba ye2 dats was his legacy 2 me!!!jaman iv vitabu ni vizuri mno!!!Mtoa mada umenikumbusha mbali mno sasa iv ata cjui ntavipata wapi!!R. I.P my Dad. R. I.P Musiba!!
 
jamani kama sikosei Elvis Msiba ni marehemu. napakumbuka nyumbani kwake mtaa wa Nyamatare Musoma karibu na shule ya msingi Kamnyonge. nilisoma na Mpwa wake jina la kwanza nimelishau baba yake aliitwa Chisanyo. Kwa siku za hivi karibuni nimekuwa nikimuona pale NMB House pale Mjini. nyumbani kwake niliwahi kufika huko Msoma hata bada ya taarifa za msiba nikiwa hapa mjini nilijulishwa na ndugu yangu aliyekuwa jirani yake.
 
Mbona hivi vitabu vipo tele tu katika maduka ya kuuzia vitabu "book shops", ingekuwa upo visiwani ningekuelekeza kwa Farouk Karim, Masomo BookShop, Darajani.
Bytheway, Huyu muandishi wa Riwaya hizi yupo wapi siku hizi, na anafanya kazi gani?
Nilizipenda sana kazi zake kama hizo ulizozitaja, lakini iliyonisisimua zaidi ni ile ya KIKOMO.

Huyu bwana ni marehemu kwa sasa,tulimzika mwaka jana kwao musoma.RIP AE Musima.
 
hamna watu wenye hatimiliki ya hivyo vitabu wavyifyatue upya? au ndo kusema wamevipiga ban bandugu
 
Mmeniikumbusha mbali sana siku zile nakumbuka nilikuwa nalia kwa fulaha na uchungu.mf pale jolam anaitwa na yule mzee anamwambia jolam lazm aende afanye upelelezi anajalibu kugoma bas mzee anamua kumwambia kuwa nitaludi.mwenyewe kwenye ulingo wa mapambano ililke it jaman ule utamu tutaupata wap
 
jamani kama sikosei Elvis Msiba ni marehemu. napakumbuka nyumbani kwake mtaa wa Nyamatare Musoma karibu na shule ya msingi Kamnyonge. nilisoma na Mpwa wake jina la kwanza nimelishau baba yake aliitwa Chisanyo. Kwa siku za hivi karibuni nimekuwa nikimuona pale NMB House pale Mjini. nyumbani kwake niliwahi kufika huko Msoma hata bada ya taarifa za msiba nikiwa hapa mjini nilijulishwa na ndugu yangu aliyekuwa jirani yake.
Hapo kwenye nyekundu nadhani ulitaka kusema Nyamatare na si Kamunyonge shule ya Msingi. Unaweza pia tembelea kaburi lake hapo kwa Nyamusibha kumuenzi mzee wetu Elvis (RIP)
 
Back
Top Bottom