Unfortunately sipo zanzibar muda mrefu sasa, lakini kama unavitaka kweli Masomo Bookshop, Darajani ni pahala pa uhakika zaidi, unaweza kuwasiliana na Farouk Karim mwenyewe anakuwepo dukani hapo, au unaweza kupata kontakti zake katika Ofisi yoyote ya ITV/Redio One, Dsm hapo,(yye ni mwandishi wa habari wa vituo hivyo), au mwandishi yeyote wa vituo hivyo anaweza akakupatia kontakti zake.Kama utaweza kufika zanzibar, ukifika soko kuu la Darajani, ukimuuliza mtu yeyote wapi Masomo Bookshop kwa Farouk Karim atakupeleka wala si mbali kutoka sokoni.