Vitabu vya Willy Gamba (Elvis Musiba) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vitabu vya Willy Gamba (Elvis Musiba)

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Kaizer, Jun 20, 2009.

 1. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #1
  Jun 20, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,664
  Likes Received: 1,506
  Trophy Points: 280
  wakuu naombeni msaada wenu kama kuna anayejua ninakoweza kupata hivi vitabu ya Elvis Musiba, vikiwa na stellingi Willy Gamba.

  Vitabu hivyo ni kama vile:
  1.Kikosi cha Kisasi
  2.Kufa na Kupona
  3.Hofu.
  4.Njama
  5.Uchu

  na vinginevyo. nimevisoma baadhi zamani lakini sasa hivi sina nakala tena ningependa kujua ninakoweza kuvipata.

  shukrani!
   
 2. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #2
  Jun 20, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Mbona hivi vitabu vipo tele tu katika maduka ya kuuzia vitabu "book shops", ingekuwa upo visiwani ningekuelekeza kwa Farouk Karim, Masomo BookShop, Darajani.
  Bytheway, Huyu muandishi wa Riwaya hizi yupo wapi siku hizi, na anafanya kazi gani?
  Nilizipenda sana kazi zake kama hizo ulizozitaja, lakini iliyonisisimua zaidi ni ile ya KIKOMO.
   
 3. Superman

  Superman JF-Expert Member

  #3
  Jun 20, 2009
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 5,702
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 145
  Du! Mkuu umenikumbusha mbali saaana . . . Mwaka 1985 nadhani, mpaka maneno ya chaper ya kwanza nakumbuka kutoka Liwaya ya "Kufa na Kupona" . . . .

  "Ilivyo ni kwamba, mimi siku ya Jumapili hulala mpaka saa nne asubuhi, na kama huamini hiyo si shida yangu . . . ."

  Nadhani mkuu, ukiwaomba jamaa wanaouza vitabu mtaani kama maeneo ya Tancot House wanaweza wakakusaidia.
   
 4. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #4
  Jun 20, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,664
  Likes Received: 1,506
  Trophy Points: 280
  mkuu ikbidi nije huko visiwani nitakuja,

  ninavojua huyu Elvis Musiba sasa hivi ni mtu mzito, nadhani alikuwa mwenyekitiwa shirikisho la wenye viwanda na kilimo, sina hakika kama ni kama ana wadhifa huo hadi sasa,,
   
 5. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #5
  Jun 20, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,664
  Likes Received: 1,506
  Trophy Points: 280
  sawa sawa mkuu, mambo ya akina Lulu na Lina hayo,,, kilichapwa kwa mara ya kwana mwaka 1974!
   
 6. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #6
  Jun 20, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Sawa sawa, Mr. Aristablus Elvis Musiba alikuwa Mwenyekiti wa Tanzania Chamber of Commerce and Agriculture.Sasa hivi anafanya biashara zake.
   
 7. M

  Mbalamwezi JF-Expert Member

  #7
  Jun 20, 2009
  Joined: Sep 30, 2007
  Messages: 803
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 45
  elvis musiba. Executive chairman corporate advisory and board director of tanzania private sector foundation
   
 8. Mchizi

  Mchizi JF-Expert Member

  #8
  Jun 20, 2009
  Joined: Apr 23, 2009
  Messages: 681
  Likes Received: 854
  Trophy Points: 180
  "Si kazi yangu kujishughulisha na makosa ya jinai,nilishangaa kidogo chifu aliponiamuru kufuatilia tatizo la upungufu wa almasi kwenye mgodi wa mwadui" ah si mchezo mambo ya "kikomo",nayakumbukumba maisha yangu ya zamani enzi hizo starehe ni sinema /disco na Riwaya.... Njama,kufa na kupona,kikosi cha kisasi,kikomo,Hofu, kweli zamani tulipata starehe.
   
 9. muwaha

  muwaha JF-Expert Member

  #9
  Jun 20, 2009
  Joined: May 13, 2009
  Messages: 743
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mimi wakuu natafuta vitabu vya Juma na Roza kwa ajili ya mwanangu, nilivipenda sana enzi hizo! naweza vipata wapi?
   
 10. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #10
  Jun 21, 2009
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,499
  Likes Received: 1,080
  Trophy Points: 280
  Umekisahau Kikomo! Mle kuana Amanda Mwakasege, Ole n.k
  Ilikuwa hadithi fupi lakini ya kusisimua sana!
  Kumbuka ile barua aliyofungua Willy haikuwa na kitu chochote zaidi ya neno ELUNGATA!
  Zile hadithi mbali ya kuburudisha, zilikuwa zinatujenga kuwa tayari kuipigania nchi yetu/Africa hadi mwisho wa maisha!
  Yalikuwa makuzi mazuri sana.......
  ......siyo hizi za kina Shigongo mara ohoo kitandani na shemeji!, Kiuno cha mkwe!, Sketi ya mwanafunzi!, n.k sasa makuzi gani haya!!??
   
 11. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #11
  Jun 21, 2009
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,499
  Likes Received: 1,080
  Trophy Points: 280
  Mkuu, kama kweli unaweza kuvipata vitabu hivi please tuwasiliane, Kikosi cha Kisasi, Kikomo, Kufa na Kupona, na Njama. Au nielekeze vizuri kwa jamaa na mawasiliano yake ni mpigie nivipate hivyo vitabu kaka!
   
 12. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #12
  Jun 21, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Unfortunately sipo zanzibar muda mrefu sasa, lakini kama unavitaka kweli Masomo Bookshop, Darajani ni pahala pa uhakika zaidi, unaweza kuwasiliana na Farouk Karim mwenyewe anakuwepo dukani hapo, au unaweza kupata kontakti zake katika Ofisi yoyote ya ITV/Redio One, Dsm hapo,(yye ni mwandishi wa habari wa vituo hivyo), au mwandishi yeyote wa vituo hivyo anaweza akakupatia kontakti zake.Kama utaweza kufika zanzibar, ukifika soko kuu la Darajani, ukimuuliza mtu yeyote wapi Masomo Bookshop kwa Farouk Karim atakupeleka wala si mbali kutoka sokoni.
   
 13. Ticha

  Ticha Senior Member

  #13
  Jun 21, 2009
  Joined: Aug 26, 2007
  Messages: 136
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  umeangalia katika bookshop ukakosa?
  msaada mwingine nenda maktaba ya taifa kama uko dar
   
 14. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #14
  Jun 21, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Elvis Musiba alikuwa mwandishi mzuri wa vitabu vya riwaya...sijui kwanini ameacha hiyo kazi. Kama kuna mtu amewahi kusoma vitabu vya James Hadley Chaseatakubaliana nami uandishi wake unashabihiana sana na wa Musiba, watu wanawasi wasi huenda mzee Musiba alikuwa anafanya tafasiri ya baadhi ya kazi za Chase kwenda kiswahili na mazingira ya kitazania na kuongezea vikolombwezo vya majina ya kibantu. Nimesoma almost vitabu vyote vya Musiba na baadhi ya kazi za James Hadley Chase kama

  The Sucker Punch

  A Coffin From Hong Kong

  Tell It To The Birds

  Knock, Knock! Who's There?

  A Can Of Worms

  na You never know with women

  Nashawishika huenda bwana Musiba alikuwa anasoma novel hizi pia na kuzitafasiri......
  Pamoja na mtizamo wangu huo bado anabakia mwandishi mzuri wa riwaya aliyewahi tokea Tanzania
   
 15. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #15
  Jun 21, 2009
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,322
  Likes Received: 1,039
  Trophy Points: 280
  Yeah,jamaa alikuwa mzuri sana kwenye masuala ya Riwaya but hata mimi nashawishika kwamba alikuwa anagandamizia kwa James Hadley Chase...Za masiku kaka.....
   
 16. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #16
  Jun 21, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160

  Salama ndugu yangu, tupo na ugumu ugumu wakulalamika hapa JF!
  Nimeona watanzania kwa kugandamiza tupo makini ...inasemekana hata Marehemu Mwalimu Nyerere alikuwa anagandamiza kazi za William Shakespeare!
   
 17. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #17
  Jun 21, 2009
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,322
  Likes Received: 1,039
  Trophy Points: 280
  Habari ndo hiyo...Nashukuru nimerudi salama ndani ya jamvi Nkwingwa baada ya likizo ya muda mrefu,hao wazee wa kulialia bado tu hawajaacha!!!!!...
   
 18. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #18
  Jun 21, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Kama likizo poa, nilihisi uko na Yo Yo Jela..... nami nategemea chukua mwishoni mwa week ijayo nikatembelee makaburi ya wahenga usukumani!
   
 19. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #19
  Jun 21, 2009
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,322
  Likes Received: 1,039
  Trophy Points: 280
  YoYo sina taarifa zake...Nenda mkuu,mi mwenyewe nimetoka Usukumani karibuni tu,siku hizi kule maji bwerere
   
 20. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #20
  Jun 21, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Teh teh unamaana yale maji ya wakubwa? ama ya baraka?
   
Loading...