kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 12,319
- 12,622
Wazungu wanao msemo wao maarufu usemao "nionyeshe rafiki zako ili nikwambie tabia yako", wakimaanisha kuwa kama ukiwa na marafiki shoga na wewe upo uwezekano mkubwa ni shoga vilevile au huuchukii ushoga hata kama wewe sio shoga.
Baba yangu alikuwa sheikh mkubwa lakini alikuwa na marafiki zake wengi ambao ni wachungaji, mapadre na wakristo ambao walikuwa wanamtembelea hadi nyumbani na wakati mwingine alikuwa anawaomba fedha za kujengea au kumalizia kujenga misikiti mbalimbali.
Tabia hii ya baba ilisababisha baadhi ya watoto wake kuolewa na kuoa wakristo bila kipingamizi kutoka kwa baba, yaani hakuona kama haiwezekani kabisakabisa mtoto wake kubadili dini na kuwa mkristo.
Tanzania tunapokea misaada na mikopo mingi kutoka "nchi rafiki" zetu ambazo wanaamini ushoga ni haki ya msingi ya mtu, na tunajisikia vizuri sana kuwa na marafiki kama hao wanaotusaidia fedha za kukwamua maendeleo yetu.
Binafsi sioni kama tunao uwezo wa kuwaambia kwa dhati na kwa moyo wetu wote marafiki zetu hawa kuwa ushoga kwetu hapana kwa sauti kubwa na ya mamlaka kwa kumaanisha.
Kama una rafiki shoga lazima na wewe nyuma ya pazia na off-camera unakubaliana na tabia hiyo. Kama hutaki tabia ya mtu furani lazina ukae nae mbali yeye na hata vitu vyake, vinginevyo utakumbana na msemo ule wa baniani mbaya kiatu chake dawa.
Kama tumedhamiria kupambana na ushoga kwa dhati na kwavitendo LAZIMA tukatae marafiki mashoga au wanaoamini kwenye ushoga. Kwenye hili nchi zote zinazoona ushoga sio sawa hazina budi kuzigeuzia mgongo nchi za magharibi hata kama kwa kufanya hivyo tutakosa mengi sana, yaani ni ile wachumi wanayoiita "opportunity cost".
Yaani tuchague kati hasara na faida za ushoga vs hasara na faida za kukosa misaada kutoka nchi za mashoga. vinginevyo tusidanganyane kuwa kuna kiongozi wa siasa mwenye mahusiano na nchi za magharibi anaepinga ushoga.