Nchi zilizohalalisha ushoga Afrika: Historia na takwimu za maktaba

BICHWA KOMWE -

JF-Expert Member
Jul 21, 2022
4,692
10,198
Takwimu za Human Rights Watch zinaonesha kuwa, nchi 23 katika bara la Afrika zimehalalisha ushoga. Baadhi kati ya hizo, ushoga haukuwahi kuwa kosa la jinai tokea mwanzo.

Mwaka 1998, South Africa ndiyo iliyokuwa nchi ya kwanza kuhalalisha ushoga barani Afrika kupitia Kesi ya Kikatiba Nambari 8 ya Mwaka 1998, ambapo Mahakama ilitamka wazi kwamba sheria inayozuia mapenzi ya jinsia moja ni batili na inakinzana na Katiba, na hivyo kuamuru kuifuta na kuitengua kutoka katika vitabu vya sheria.

Vivyo hivyo, mwaka 2015, Bunge la Mozambique lilifuta sheria dhidi ya ushoga ya kikoloni na kutunga sheria mpya (the 2015 Criminal Code) iliyohalalisha mapenzi ya jinsia moja. Sheria ya ushoga nchini Mozambique imekuwepo toka enzi za wakoloni na ilidumu bila mabadiliko yoyote hadi mwaka 2015 ambapo ilifutwa rasmi.

Katika mfuatano huo, mwaka 2019, Botswana ilifutilia mbali sheria dhidi ya ushoga kupitia kesi ya kikatiba baina ya Letsweletse Motshidiemang Vs State, ambapo Mahakama kuu ilitoa amri ya kufuta sheria hiyo kwa kutamka kwamba inakinzana na Katiba kwa kupoka haki ya Uhuru, Faragha na Utu. Mwaka 2021, Mahakama ya Rufaa nchini humo ilikazia na kuhalalisha hukumu ya Mahakama kuu na kufanya mapenzi ya jinsia moja kuwa halali hadi sasa.

Mwaka 2020, Angola, kupitia Bunge lake, ilifuta sheria ya kikoloni dhidi ya ushoga, na kutunga sheria mpya (the 2020 penal code) ambayo ilitoa ruhusa ya mapenzi ya jinsia moja nchini humo pamoja na kuzuia vitendo vya ubaguzi na unyanyasaji vinavyohusiana na chaguzi za kimapenzi (sexual orientation).

Vivyo hivyo, nchi zingine kama vile Syecheless, Cape verde, Namibia, Mauritius, Guinea Bissau, Lesotho, na Soa Tome and Principe nazo kwa nyakati tofauti tofauti zilifuta sheria za kikoloni za ushoga kupitia kesi mbalimbali za kikatiba zilizofunguliwa kupinga vifungu vya sheria hizo batili.

Katika takwimu hizo, inaonesha kuwa, ushoga haukuwahi kuwa kosa la jinai katika nchi kumi na mbili tangu kuanzishwa kwake. Nchi hizo ni Burkina Faso, Benin, Gabon, Ivory Coast, Djibouti Jamuhuri ya Afrika ya kati, Congo, Equatorial Guinea, Madagascar, Mali, Niger na Rwanda.

Historia inaonesha kuwa, uwepo wa sheria za jinai dhidi ya ushoga katika baadhi ya nchi za kiafrika umetokana na uvamizi wa kikoloni wa Waingereza ambao ndio waliozileta sheria hizo katika makoloni yao kuanzia karne ya 18 hadi ya 20.

Nchi ambazo hazikutawaliwa na waingereza hazikuwahi kuwa na sheria za ushoga mathalani nchi ya Rwanda.

Nchi zilizotawaliwa na Waingereza, sheria zao za ushoga zilikuwa na maneno mfanano (similar wording of the law), kitu ambacho kinathibitisha kwamba sheria hizo zilikopiwa na kupachikwa katika makoloni (copy and paste) kama jinsi zilivyo. Nchi hizo ni kama vile Uganda, Kenya, Botswana, na Tanzania.

Uhusiano wa sheria za ushoga na wakoloni wa Kingereza una chimbuko lake la kidini ambalo limeundwa katika msingi wa utawala wa kiroma uliotaka kuwalinda wakristo dhidi ya ufiraji kupitia tunu za kibiblia (biblical values).

Baada ya uhuru, nchi za Kiafrika zikaanza kubadili sheria za ushoga taratibu mpaka mwaka 1998 ambapo South Afrika ilianza kuchukua hatua za wazi kutokana na katiba yao kuwa na mawanda mapana ya haki za binadamu na utawala wa sheria.

MY TAKE: Tanzania tujifunze kutoka South Africa.
 
Bongo mashog kitambo tu wako
Wbongo kizaz cha sahv ndy kabisa
Wanafln San na kufilw
Media zenyew na sanaa wasanii kibao
Wamejaaaa wasng na wabongo wanaishi nao alafu ukiwakuta wanawaponda huku wanaishi nao

Ova
🤣🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom