G.MWAKASEGE
Senior Member
- Jun 29, 2007
- 153
- 21
Wana JF,
Nimesoma majibu ya wanajambo kwa hoja iliyotolewa kuhusiana na uzushi wa maisha ya Dkt. Slaa. Mimi binafsi nilijua haya masuala ya uzushi yatatokea kwani ndio umekua utamaduni wetu kisiasa hapa tanzania. Yalitokea kwa Kambona, Bibi Titi na baade akina Mrema. Slaa, Zitto, Mbowe, Mnyika etc hawatapona katika siasa hizi za kipuuzi kabisa.
Mambo haya yaliyoandikwa juu ya Dr. Slaa ni uzushi ambao hata haiingilii akilini kwa mtu mwenye akili kuanza kujibu. Unajibu nini jamani?
Sisi CHADEMA tunaongoza kama timu. Hatuna la kuoneana kijicho kuhusiana na umaarufu wa yeyote. Kazi ambazo viongozi wetu wanafanya ni kwa niaba ya nchi na ili kuiweka nchi yetu pazuri tunaimarisha chama chetu.
Dkt. Slaa aliacha Upadre kwa taratibu zote za kanisa katoliki na kupewa kibali kutoka Vatican. Wanaosema kafukuzwa, kirahisi tu hawajui wasemacho.
Dkt. Slaa mpaka hapa tunapozungumza ni mjumbe wa bodi ya Tanzania League of the Blind. Pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya CCBRT. Kama aliiba huko angekuwa amefukuzwa!
Mimi ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, mahusiano ya Dkt. Slaa na Lazaro Masay ni mzuri mno na hakuna dalili zozote ati kuwa Dkt. Slaa kachukua mkewe nk.
Ninavyojua mimi Dkt. Slaa hana ambition za Urais. Honest person doing his work. Mbona watu wanaweweseka sana na Urais ujao? Maana kitu hii inazuka sana, mtu akifanya kazi yake, anataka Urais........ mchecheto huu ni wa nini?
Mimi nadhani tuangalie masuala ya msingi zaidi yanayohusu nchi yetu..... Ufisadi unamong'onyoa taifa letu. Juhudi za kuchafua viongozi wa upinzani haziaidii kuliendeleza taifa letu
Kilitime,
Naona unaanza kuishiwa ndugu yangu..
Nduguyo
Tehe tehe tehe,,, FD, Mimi siwezi ishiwa nguvu labda siku uzalendo wako utapokuwa umeondoka ambao sio leo au kesho!!!
Kwa bahati mbaya mimi siye yule ninaye amini kuwa kila mtoa mabomu ni kiongozi mzuri, au kila mkosoaji ni kiongozi mzuri, wakati mwingine kuna mtu ni mzuri kwenye kukosoa tu! mimi nampima kiongozi kwa mambo mengine zaidi, na kwa mwana siasa ambaye pia siasa ni ajira yake kwangu ni sawa sawa na fisadi tu!
Thus why mimi ni mpenzi wa siasa za Kenya sana.
Tunaangalia mambo kwa mapana yake, na tunapenda haki itendeke na ionekane kama inatendeka!!!
Kiltime said:Thus why mimi ni mpenzi wa siasa za Kenya sana.
Yoooh,
Soma tena ulicho andika hapo juu, unaongea nini wewe? mbona unajichanganya sana......?lazima utakuwa umedata flani hivi!!. Yaani ktk siasa zote za dunia hii wewe umeziona za kenya!!!??? ama kweli kazi ipo.
watu wanataka kupaka viongozi wa taifa/ccm mavi kama akina jk, el, n.k tunafahamu wana mabaya yao lakini wapi watu wanapata idea ya kusema hii kitu inafanywa na hao viongozi ?
this is a shame, na udaku wa hali ya juu !
Rafiki yangu moja wa Kenya alinitonya kwamba rais aliyestaafu Mzee Moi ana ardhi kama hekari 500,000. Sasa kwa kiongozi wa nchi kuwa na ardhi kubwa namna hiyo iliniogopesha sana ukitilia maanani Kenya tunaambiwa kuna uhaba wa ardhi. Mkiwa na 100 Moi's hizo ni ekari 50,000,0000 (50 million) na nchi yenyewe ina watu wangapi sijui?
Mimi nafikiri wanaoshambuliwa watakuja kujibu mapigo wenyewe kwa sababu ni members hapa.
Tujadili hoja, lakini mengine, utaelewa ukivua hilo pazia machoni/mbeleni mwako!!!
Kwa taarifa yako, they are matured in politics than we do!!! kama huamini sio tatizo langu kaka yangu lakini mwenye macho haambiwi ona,,, suala la katiba walivyofanya, issue ya economy kwenda mbele 7%
Mambo ya mawasiliano,,, unajua wanafanya connection na Uarabuni kwa kutumia fibre,,, baada ya nchi kama Tanzania, SA etc... kuwa na mwendo wa kinyonga...
Wenzetu wamekomaa,,, wanauwezo wa kukataa wanasiasa wa chama tawala na wa upinzani kwa hoja pia,,, mapungufu yapo ya ukabila lakini sio makubwa sana.