Ndugu zangu, kwanza nawapongeza kwa dhati wale wote waliojitokeza kupinga uchafu huu wa kutojibu hoja kwa kujibu kwa vioja. Ni lazima tuweke kanuni ambayo si rahisi kuivunja katika kujenga hoja amasivyo itakuwa ni yale kwa kiswahili tunayaita "kuzunguka mbuyu"!
Katika mapambano haya ya kifikra silaha zote zinaruhusiwa na zinakaribishwa, ni mapambano ambayo hatima yake ni ushindi wa utawala wa sheria, demokrasia, usawa, na nafasi sawa kwa watu wote katika Taifa letu. Kuna watu ambao hawako tayari kuona hilo linatokea ingawa mbele ya hadhara wanaimba pambio za sifa zake.
Na hii ni mojawapo ya sababu zinazotufanya wengine tuweke mbali kwa muda majina yetu ili tuweze kujenga hoja pasipo kuleta maisha yetu binafsi hadharani kwani tunafahamu kuwa watawala wakishindwa hoja wao huleta kejeli na tuhuma zisizo na msingi. Askofu Ncube wa Zimbabwe alipokuwa anapiga kelele sana dhidi ya utawala wa Zimbabwe, mashushushu wakamseti up na mke wa kiongozi mmoja wa kanisa na kumkuta katika "compromising position" (KLH Exclusive pictures ziko kule
HAPA.
Na huko tunakokwenda tuhuma za nani alivaa nguo gani alipoenda kulala na nani alikula na nani na watoto wao walilala wapi zitaendelea kutolewa katika kuzima uzito wa hoja.
Jambo nashukuru ni kuwa wengi tumegundua kuwa yeyote aliyeleta hoja hizi ana kusudio la kuchafua mjadala. Kwa vile wao watawala wamekuja na huu mtindo kuwa wao wanaheshimu utawala wa sheria sana na ya kuwa mwenye kutoa tuhuma basi aende mahakamani, wakati umefika kama wanatuhuma za ubadhirifu au uvunjaji wa sheria uliofanywa na Dr. Slaa au kiongozi yoyote yule basi waende mahakamani! Si wao wanasema Mahakamani ndiko haki inawezekana kupatikana?
Vinginevyo, tutaendelea bila kutishwa, kubabaishwa, au kwa namna yoyote ile kufanywa duni katika kuzungumza mustakabali wa Taifa letu. Binafsi sina muda wa mambo binafsi ambayo hayahusiani na kazi na utumishi wa mtu na hayavunji sheria. Dito alipofumaniwa na mke wa mtu mbona alizawadiwa Ukuu wa Mkoa na hawakusema kuwa inamfanya mtu mbaya? Kwani Karamagi mke wake kamtoa wapi? .. mkijua hili wenzenu wanajua lile.. huo ni mfano tu..!!!
Siasa ni fani yangu na wakitaka kuleta mchezo mchafu, wajue kwamba binafsi sina mpinzani!!! Ukianza kuchezea matope kuwarushia wengine, na wewe yanakuchafua!