Zitto
Former MP Kigoma Urban
- Mar 2, 2007
- 1,562
- 10,891
Wana JF,
Nimesoma majibu ya wanajambo kwa hoja iliyotolewa kuhusiana na uzushi wa maisha ya Dkt. Slaa. Mimi binafsi nilijua haya masuala ya uzushi yatatokea kwani ndio umekua utamaduni wetu kisiasa hapa tanzania. Yalitokea kwa Kambona, Bibi Titi na baade akina Mrema. Slaa, Zitto, Mbowe, Mnyika etc hawatapona katika siasa hizi za kipuuzi kabisa.
Mambo haya yaliyoandikwa juu ya Dr. Slaa ni uzushi ambao hata haiingilii akilini kwa mtu mwenye akili kuanza kujibu. Unajibu nini jamani?
Sisi CHADEMA tunaongoza kama timu. Hatuna la kuoneana kijicho kuhusiana na umaarufu wa yeyote. Kazi ambazo viongozi wetu wanafanya ni kwa niaba ya nchi na ili kuiweka nchi yetu pazuri tunaimarisha chama chetu.
Dkt. Slaa aliacha Upadre kwa taratibu zote za kanisa katoliki na kupewa kibali kutoka Vatican. Wanaosema kafukuzwa, kirahisi tu hawajui wasemacho.
Dkt. Slaa mpaka hapa tunapozungumza ni mjumbe wa bodi ya Tanzania League of the Blind. Pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya CCBRT. Kama aliiba huko angekuwa amefukuzwa!
Mimi ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, mahusiano ya Dkt. Slaa na Lazaro Masay ni mzuri mno na hakuna dalili zozote ati kuwa Dkt. Slaa kachukua mkewe nk.
Ninavyojua mimi Dkt. Slaa hana ambition za Urais. Honest person doing his work. Mbona watu wanaweweseka sana na Urais ujao? Maana kitu hii inazuka sana, mtu akifanya kazi yake, anataka Urais........ mchecheto huu ni wa nini?
Mimi nadhani tuangalie masuala ya msingi zaidi yanayohusu nchi yetu..... Ufisadi unamong'onyoa taifa letu. Juhudi za kuchafua viongozi wa upinzani haziaidii kuliendeleza taifa letu