Vita Kali ndani ya CHADEMA

Mtoto wa Mkulima

JF-Expert Member
Apr 12, 2007
681
126
Jamani hii nimeipata kwenye e mail na naona inazunguka hapa sija-add chochote.

Nawasilisha hoja


Tarehe 11/10/2007 katika kituo kimoja maarufu cha runinga kulionyeshwa kipindi kimoja cha vichekesho ambacho sasa kimezua jambo ndani ya chama maarufu cha CHADEMA.

Katika kipindi hicho, baadhi ya vitendo vichafu vya Dr. WILBROD SLAA vilianikwa hadharani. Awali watazamaji wengi hawakutilia maanani yaliyosemwa kwenye kipindi hicho kwani walidhani ni vichekesho vya kawaida. Lakini sio hivyo tena baada ya hali ya kisiasa isiyotarajiwa kufahamika ndani ya chama cha CHADEMA.

Katika siku za karibuni Dr. SLAA amejichotea sifa nyingi baada ya kutoa hadharani tuhuma alizoziita za kifisadi na kutaja majina ya watu aliowaita mafisadi. Ingawaje Dr. SLAA mwenyewe amekiri miongoni mwa marafiki zake kwamba tuhuma zake hazina hata chembe ya uthibitisho lakini amepata furaha ya mshangao kuona jinsi ambavyo tuhuma zake zimempa sifa lukuki ndani na nje ya nchi.

Habari toka ndani ya chama cha CHADEMA zinasema kuwa ingawaje kwa juu juu MBOWE na ZITTO KABWE wanaonekana kufurahia umaarufu wa Dr. SLAA lakini wote hao wawili kwa sababu zao tofauti wameelezwa kuumia sana kwani wanaona Dr. SLAA anawapiku umaarufu wa kisiasa na kwamba huenda akaamua kugombea urais mwaka 2010 kwa tiketi ya CHADEMA.

Mhe. MBOWE na ZITTO KABWE wameapa kummaliza kabla hajafika mbali. Ati MBOWE anaona Ikulu inamwita na njia ni nyeupe lakini sasa anaibuka mtu anaitwa SLAA anataka kumnyang'nya kilicho chake!

Ni kwa msingi huo, sasa MBOWE na ZITTO wameamua kuanika madhambi ya Dr. SLAA ili wananchi wajionee kwani wanaamini madhambi yao wao hayajulikani maana wameshatumia mamilioni ya pesa kuyazika madhambi hayo. Ili kutimiza lengo lao wameamua kusambaza baadhi ya vioja vya Dr. SLAA. Hivi wanadai ni baadhi tu kwa vile orodha ni ndefu na wataitoa kwa awamu. Wameanza na nyepesinyepesi. Haya ndiyo wameyaanika kwa sasa:

MJUE DR SLAA

Mpaka sasa SLAA hana nyumba huko Karatu, badala yake hulala kwa rafiki yake ambaye inadaiwa ni shoga.

Tangu mwaka 1977 hadi 1991, SLAA alikuwa Padre wa Kanisa Katoliki Jimbo la Mbulu. Aliachishwa Upadre baada ya kukosa uaminifu na kuendekeza tabia ya ufuska na wake za waumini. Hali hiyo ilimpelekea kupata watoto wawili wakati akiendelea kutoa huduma za kiroho. Watoto hao ni EMILIANA aliyezaliwa 18/06/1987 na LINUS aliyezaliwa 23/09/1988. Dr. SLAA alimuoa ROSE, mmoja wa waumini wake mwaka 1991 ndipo kanisa likamfukuza Upadri. Wakati huo ROSE alikuwa mchumba wa mweka hazina wa Kanisa ambaye miaka michache baadaye alikufa kutokana na mfadhaiko.

Uchunguzi umeonesha kwamba, Dr. SLAA ni fuska aliyebobea, na anayo tabia ya kufanya mapenzi na wake wa marafiki zake hata baada ya kuoa. Kwa mfano Diwani wa Kata ya Baray wilayani Karatu LAZARO TITUS MASSAY (CHADEMA) aliwahi kupeleka malalamiko katika uongozi wa juu wa CHADEMA kuhusu tabia ya SLAA ya kufanya mapenzi na wake za watu wakiwemo hata wake za Madiwani Jimboni Karatu. Aidha, tarehe 01/11/2004, SLAA alifumaniwa na mkewe katika chumba kimojawapo cha Hotel 56 mjini Dodoma akiwa anafanya mapenzi na msichana aitwaye NJARI. SLAA aliruka dirishani bila nguo na wahudumu wa hoteli wakamsetiri kwa shuka na kumficha hadi mke wake alipoondoka kwa hasira kali baada ya kupambana na wizi・wake sawasawa - tukio hilo lilinaswa kwenye mkanda wa simu ya mkononi ya mhudumu na umehifadhiwa kwa matumizi katika wakati muafaka.

Dr. SLAA anasumbuliwa na ugonjwa mkubwa・ Amekuwa akienda kutibiwa mara kwa mara nchini Afrika Kusini. Mwezi Oktoba hadi Desemba, 2006, SLAA alilazwa katika Hospitali ya Aga Khan jijini Dar es Salaam akitibwa gonjwa moja hatari sana.

Dr. SLAA amewahi kula mamilioni ya fedha za vilema ambazo zililetwa na wafadhili toka Ujerumani. Ushahidi upo kama atafanya ubishi.

Alihongwa nyumba Ujerumani na hawara yake wa Kijerumani ambaye sasa ni marehemu na Dr. SLAA anategemea kuhamia huko. Inasemekana Dr. SLAA na hawara yake ambaye ni marehemu walishirikiana kumuua mume halali wa mama huyo aliyejulikana kwa jina la 全imbosh・

Dr. SLAA alikuwa kachero wa Idara ya Usalama wa Taifa kama alivyo LYATONGA MREMA na alikuwa anaendelea kulipwa kiasi kikubwa cha fedha. Baadaye Idara hiyo nyeti iligundua fedha hizo anapeleka kwa hawara zake hivyo ikasitisha malipo hayo hali ambayo imemuudhi na akaanza kuipaka matope kwa kuituhumu na taarifa za kughushi anazodai amezipata. Vyanzo vya kuaminika vimebaini SLAA alipewa taarifa ya kughushi na akainunua kwa bei mbaya. Baada ya kubaini hivyo sasa anamsaka mbaya wake aliyemwingiza mjini.

Ujumbe huu ambao inaaminika MBOWE na ZITTO KABWE wanausambaza kwa kasi umemtia hofu Dr. SLAA kwani anajua yapo mengi yanayomhusu ambayo asingependa yajulikane. MBOWE na ZITTO wanaungwa mkono na chama cha CUF ambacho nacho kinadhani CHADEMA imekipiku katika umaarufu wa upinzani. Sera ni jino kwa jino.

JAMANI ATI HAWA NDIO WANATAKA KUCHUKUA
NCHI ・WATANZANIA TUTAFAKARI KWA MAKINI

=========
Ufafanuzi toka CHADEMA - Oktoba 16, 2007

Wana JF,

Nimesoma majibu ya wanajambo kwa hoja iliyotolewa kuhusiana na uzushi wa maisha ya Dkt. Slaa. Mimi binafsi nilijua haya masuala ya uzushi yatatokea kwani ndio umekua utamaduni wetu kisiasa hapa tanzania. Yalitokea kwa Kambona, Bibi Titi na baade akina Mrema. Slaa, Zitto, Mbowe, Mnyika etc hawatapona katika siasa hizi za kipuuzi kabisa.

Mambo haya yaliyoandikwa juu ya Dr. Slaa ni uzushi ambao hata haiingilii akilini kwa mtu mwenye akili kuanza kujibu. Unajibu nini jamani?

Sisi CHADEMA tunaongoza kama timu. Hatuna la kuoneana kijicho kuhusiana na umaarufu wa yeyote. Kazi ambazo viongozi wetu wanafanya ni kwa niaba ya nchi na ili kuiweka nchi yetu pazuri tunaimarisha chama chetu.

Dkt. Slaa aliacha Upadre kwa taratibu zote za kanisa katoliki na kupewa kibali kutoka Vatican. Wanaosema kafukuzwa, kirahisi tu hawajui wasemacho.

Dkt. Slaa mpaka hapa tunapozungumza ni mjumbe wa bodi ya Tanzania League of the Blind. Pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya CCBRT. Kama aliiba huko angekuwa amefukuzwa!

Mimi ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, mahusiano ya Dkt. Slaa na Lazaro Masay ni mzuri mno na hakuna dalili zozote ati kuwa Dkt. Slaa kachukua mkewe nk.

Ninavyojua mimi Dkt. Slaa hana ambition za Urais. Honest person doing his work. Mbona watu wanaweweseka sana na Urais ujao? Maana kitu hii inazuka sana, mtu akifanya kazi yake, anataka Urais........ mchecheto huu ni wa nini?

Mimi nadhani tuangalie masuala ya msingi zaidi yanayohusu nchi yetu..... Ufisadi unamong'onyoa taifa letu. Juhudi za kuchafua viongozi wa upinzani haziaidii kuliendeleza taifa letu
 
Kuna kila dalili hizi ni njama za CCM kumchafua Slaa na kuanzisha kasheshe ndani ya CHADEMA, na siyo Zitto au Mbowe kama unavyotaka tufikirie.. Hebu tupe source ya habari hii. Zitto kama upo maeneo ya usawa wa JF hebu tupe habari zaidi kuhusu shutuma hizi.
 
Kuna kila dalili hizi ni njama za CCM kumchafua Slaa na kuanzisha kasheshe ndani ya CHADEMA, na siyo Zitto au Mbowe kama unavyotaka tufikirie.. Hebu tupe source ya habari hii. Zitto kama upo maeneo ya usawa wa JF hebu tupe habari zaidi kuhusu shutuma hizi.

Mkuu Bubu hii habari sijaandika mimi kama nilivyoeleza hapo juu nimekuta kwa email yangu ni kama kampeni ya kuisambaza nikakopy na kupest hapa ili ijadiliwe. Mimi binafsi naona hizi ni njama sa kuchafua silaa. Kama aliwahi kuuwa kwanini hao wajerumani wa mwache aendelee kutanua mtaani na si gerezani? Hapo kuna kauli nyingi sana ukisoma unajua kabisa haziwezi kutoka kwa Zitto wala Mbowe. Hii ni kampeni tuu ya kuchafua na nimejaribu kutrace hii e mail nimeona ilikotokea ila sijui kama ndio mwanzo wa hizo forward au ni zaidi ya hapo.
 
UPUPU mtupu kwenye huu ujumbe. Hauhitaji kuwa na madegree kibao kugundua ni CCM wanataka kumchafua Dr. Slaa kwasababu anaonekana yeye ndiye mwenye nguvu zaidi.

Mwandishi si ataje jina lake?
 
Bubu Ataka Kusema, unamuuliza Mtoto wa Mkulima akupe source wakati yeye ndiye source yenyewe si atajiuma ulimi?

Kaanza kwa kusema kuwa yeye kaileta jinsi alivyoipata bila ku-add cho chote lakini kichwa cha mada yake ni "Vita kali Ndani Ya Chadema" . Na hicho kichwa cha mada hakuweka kama swali au kuuliza kama yasemwayo ni kweli, bali kaweka kwa njia ya kuvutia au kuamsha hisia za wasomaji.

Mjumbe hauwawi, ila mjumbe akiupamba ujumbe na kubadili maana ya ujumbe anaweza akasababisha mtu akauwawa (na huyo mtu anaweza akawa yeye mjumbe)!
 
watu watasema ni njama za ccm !

just wait and watch ! watu watakavyoanza kujaza nafasi !
 
Bubu Ataka Kusema, unamuuliza Mtoto wa Mkulima akupe source wakati yeye ndiye source yenyewe si atajiuma ulimi?

Kaanza kwa kusema kuwa yeye kaileta jinsi alivyoipata bila ku-add cho chote lakini kichwa cha mada yake ni "Vita kali Ndani Ya Chadema" . Na hicho kichwa cha mada hakuweka kama swali au kuuliza kama yasemwayo ni kweli, bali kaweka kwa njia ya kuvutia au kuamsha hisia za wasomaji.

Mjumbe hauwawi, ila mjumbe akiupamba ujumbe na kubadili maana ya ujumbe anaweza akasababisha mtu akauwawa (na huyo mtu anaweza akawa yeye mjumbe)!

Nonono Kiungani. Kwani e mail haina subject? Hiyo title ni subject kwenye e mail hiyo. labda mnataka niiweka kama nukuu? Unauhakika gani kuwa mimi ni source ya hiyo e mail? kwani ningekuwa source ngekuwa na haja gani ya kusema kuwa nimeipata kwa e mail, kwa sababu siogopi mtu eti nifiche kuwa source ni email. Mimi mkuu wala sijapamba chochote hapo kwani wewe unaona huo ujumbe umepambwa? Unanifanya nicheke sana. Nahakika hii imeshafikia baadhi ya wana JF maana ni list ndefu ya walio forwadiwa hadi kufika kwangu.
 
Mwl Nyerere aliwahi kusema hivi"mtu mwenye akili akikupa ushauri wa kijinga,na huku akijua wewe una akili na unajua ushauri huo ni wa kijinga halafu ukaukubali,ATAKUDHARAU".

Wote mliopata hiyo mail anayodai jamaa hapo juu,nadhani mna akili mkikubaliana na huo utumbo ulioandikwa hapo basi mwandishi wa hiyo mail atawadharau.Wana JF,hivi kuna logic gani kwenye hiyo message hapo juu,huyo mwandishi alichofanya ni kutuambia private issues za Dr. Slaa ambazo hatujui ukweli wake,kuhusu ufuska,hiyo haituhusu,kuwa na hawara ujerumani aliyemwachia nyumba,hilo ni jambo la kheri kuliko yeye kuhonga nyumba kama wengi wafanyavyo hapo nyumbani.Dr.Slaa kutokua na nyumba kwao,na hayo hayatuhusu,ni uamuzi wake,muda ukifika atajenga tu,au atahamia hiyo nyumba yake ya ujerumani amabyo mwandishi anadai,kwani kuna mwiko gani akienda kuishi ujerumani?Dr.Slaa kuwa na ugonjwa wa ajabu,hiyo ni mipango ya Mungu,hata wewe uliyeandika hiyo mail naona ndio una ugonjwa mkubwa wa akili ambao hutaweza kuutibu.

Hii hapa nitaifanananisha na michezo ya kuigiza,tunarudi kwenye mada yetu ya MAFISADI,hayo tumeyasikia yameshapita,lakini mada ya UFISADI kipindi hiki haipiti,tupo nanyi hadi kieleweke.
 
...upupu mtupu,hivi mnafikiri watanzania ni wajinga kiasi gani kuamini huu utumbo wenu? mmeishiwa kweli kweli kilichobaki ni kuwapiga chini tuu
 
Wewe BUBU ATAKA KUSEMA. Nenda Karatu na Hanang kaulize hizi habari ndipo utajua hakuna njama yoyote ya CCM. Ni uchafu wake Slaa. Vipi mbona imekuuma?
 
Kama hana nyumba huko na Dar hana nyumba ? Kwani Slaa kutokuwa na nyumba , maisha yake binafsi yana muumiza nani kama anaitendea Taifa hili mema ?Hii si mail ya mzunguko ila imejengwa na mleta hoja hii . Niko Karatu as we speak .Nimeonyeshwa nyumbani kwa Dr.Slaa na mambo mengine .Kusema rafiki yake shoga this is extreme lakini kwa kuwa CCM ni wajuzi wa kupika majungu maana hata Salim aliambiwa ni Hizbu leo sitashangaa Slaa kuitwa majina yeyote .
 
Wewe BUBU ATAKA KUSEMA. Nenda Karatu na Hanang kaulize hizi habari ndipo utajua hakuna njama yoyote ya CCM. Ni uchafu wake Slaa. Vipi mbona imekuuma?

....habari gani wewe za kuuliza huko karatu? na kama hamna cha kuandika bora mkae kimya maana mnajiaibisha tuu.
 
Wewe BUBU ATAKA KUSEMA. Nenda Karatu na Hanang kaulize hizi habari ndipo utajua hakuna njama yoyote ya CCM. Ni uchafu wake Slaa. Vipi mbona imekuuma?

Naweza kusema kuwa hizo tuhuma zina ukweli ndani yake. Lakini kwanini zitolewe sasa na sio huko nyuma? Na kwani hakuna CCM anayefanya mambo kama hayo? Kwanini yeye asiandikwe hivyo? Mimi naona ndio siasa za Salva za kupambana na watu kwa kuspread fitna, no more no less, it is all pack of crap. La muhimu tunaloangalia zaidi ni yale yenye manufaa kwa taifa letu, mambo binafsi hatuna haja nayo. Kuna watu wengine mawaziri walikuwa wanatembea na wafanyakazi wenzao maofisini, lakini hakuna anayejali, kwanini Slaa iwe issue? ni njama tu ya CCM.
 
nasema hivi :

subirini tu hapa muone nafasi zitakavyojazwa watu kusema kwamba hii ni kampeni chafu dhidi ya chadema, cha kushangaza basi utadhani hawajui mbowe, zitto, slaa walipo ili wawaulize ! kizuri zaidi kama mnataka habari hii ikemewe zittoni mwanachama wa JF hivyo itakuwa vizuri aje akanushe haya ( definitely i expect him kukanusha vilivyo ili kuokoa maslahi ya chama so i wont be suprised ) kama alivyokanusha habari ya mbowe kula mabilioni ya kampeni !

Mh. Zitto eeeh nakuomba utokee hapa ukanushe haya madai, na simaanishi washika dau wa chadema i.e akina .................. na ................. na.......................... na..................... na...........................na......................and the list goes on, bali nakuhitaji wewe au mbowe mkanushe !
 
Upumbavu mtupu huu. Anayefanya hizi kampeni kama ni mwanasiasa afadhali atafute career nyingine kwani amefilisika ki siasa.

Upumbavu zaidi umejionyesha pale kila mtu ambaye anaweza kuwa shahidi wa kuthibitisha tuhuma hizi ni marehemu. Muweka hazina ameisha fariki, anayedaiwa kuwa ni hawara wa kijerumani ameisha fariki. Sintoshangaa hata kusikia aliyetunga huu upumbavu ameisha fariki.

Kama mtu huna jipya si afadhali ukae kimya kuliko kuuonyesha upumbavu wako mbele ya kadamnasi. Ninadhani aliyetunga hizi habari ndiye shoga na nitaendelea kuamini kuwa muandishi wa hizi habari ni shoga mpaka athibitishe tofauti.

Ndiyo maana bado tunaendelea kuomba miaka 46 baada ya uhuru na mali asili tunayo...
 
I ONLY HAVE ONE THING TO SAY TO THE WORLD ( INLCUDING TANZANIA AND ITS LEADERS ) !!

YOU CAN PLAN IT, ACT IT, CALCULATE IT, MANIPULATE IT, CONTROL IT, HIDE IT, BUT THERE IS ALWAYS A TRACE OF EVIDENCE YOU ARE GOING TO LEAVE BEHIND.... sasa chadema jianikeni uwanjani !
nasema hivi, mliona mkuki mtamu kwa nguruwe sasa mnajichoma wenyewe mnasema sumu !

there's more to come ! lets party !
 
Upumbavu mtupu huu. Anayefanya hizi kampeni kama ni mwanasiasa afadhali atafute career nyingine kwani amefilisika ki siasa.

Upumbavu zaidi umejionyesha pale kila mtu ambaye anaweza kuwa shahidi wa kuthibitisha tuhuma hizi ni marehemu. Muweka hazina ameisha fariki, anayedaiwa kuwa ni hawara wa kijerumani ameisha fariki. Sintoshangaa hata kusikia aliyetunga huu upumbavu ameisha fariki.

Kama mtu huna jipya si afadhali ukae kimya kuliko kuuonyesha upumbavu wako mbele ya kadamnasi. Ninadhani aliyetunga hizi habari ndiye shoga na nitaendelea kuamini kuwa muandishi wa hizi habari ni shoga mpaka athibitishe tofauti.

Ndiyo maana bado tunaendelea kuomba miaka 46 baada ya uhuru na mali asili tunayo...

sasa mnaona slaa ni msafi hivyo au ? acheni kuabudu watu hasa pale maovu yao yanapoanikwa !

leo hii mnaambiwa haya na mnakanusha, akiingia madarakani ndiomtaanza kusema kuna machizi fulani walisema slaa mchafu hatukumsikiliza ! binadamu always tunajirudisha steps behind, jambo likitokea tunaanza kulia !
 
.... Katika kipindi hicho, ....Dr. WILBROD SLAA ..... Dr. SLAA amejichotea sifa nyingi .... Ingawaje Dr. SLAA .....juu MBOWE na ZITTO KABWE wanaonekana kufurahia umaarufu wa Dr. SLAA ....Dr. SLAA ... anaitwa SLAA .... sasa MBOWE na ZITTO wameamua .....ya Dr. SLAA ili wananchi ...... Dr. SLAA.


MJUE DR SLAA

Mpaka sasa SLAA hana nyumba huko Karatu, ...SLAA .... Dr. SLAA ..., Dr. SLAA ni fuska aliyebobea, SLAA ...SLAA ... SLAA ....Dr. SLAA anasumbuliwa na 爽gonjwa mkubwa.. SLAA alilazwa katika Hospitali ya Aga Khan jijini Dar es Salaam .... Dr. SLAA ..... Ushahidi upo kama atafanya ubishi.
Dr. SLAA na hawara yake ambaye ni marehemu walishirikiana kumuua mume halali


Dr. SLAA .... SLAA ...

....

Next time watasema Slaa alikuwa kwenye coup attempt ya miaka ya 60, amesababisha jeti ya rais iliyonunuliwa kwa mabilioni kukwama, and on and on....

Tanzania yetu.......
 
sasa mnaona slaa ni msafi hivyo au ? acheni kuabudu watu hasa pale maovu yao yanapoanikwa !

leo hii mnaambiwa haya na mnakanusha, akiingia madarakani ndiomtaanza kusema kuna machizi fulani walisema slaa mchafu hatukumsikiliza ! binadamu always tunajirudisha steps behind, jambo likitokea tunaanza kulia !

Kada,

You know that God is omniscient. That is the only person I believe in. No more, no less.
 
sasa mnaona slaa ni msafi hivyo au ? acheni kuabudu watu hasa pale maovu yao yanapoanikwa !

leo hii mnaambiwa haya na mnakanusha, akiingia madarakani ndiomtaanza kusema kuna machizi fulani walisema slaa mchafu hatukumsikiliza ! binadamu always tunajirudisha steps behind, jambo likitokea tunaanza kulia !

mbona unaanza kulia..... toa point yako na uisimamie sio kulazimisha watu kukubaliana nawe!

BTW.... unamjua vipi huyo shoga wa stori?
 
Back
Top Bottom