Visa gani pombe ilikufanyia hutasahau?

Visa gani pombe ilikufanyia hutasahau?

Visa tutakua kesho vingine maana leo, hata Mimi nimependeza japo niliapa sinywi Tena

Nataka nikazie maji mengi kabla sijalala kesho angalau nikipigiwa simu niweze kupokea🤣
 
Oya mlioahidi kuacha mmesha acha tungi au ndo zilikua porojo tu
 
Yaani mi binafsi sina wazo kabisa la kuiacha pamoja na yote inayonifanyiaga lakini haijanikomoa.
Ninakumbuka kiroba cha boss tangawizi hangover yake balaa,inafunga hamu ya kula,kunya mpaka kuoga na ukijilazimisha kunywa supu basi mchuzi mnaugawana na meza kwa jinsi mikono inavyotetemeka.
Mpaka kunya mkuu 😂😂😂
 
Pombe imeniletea visa vingi sana hapa duniani, nilikwenda Mbeya kikazi miaka tisa au kumi iliyopita. Kukawa kuna baa mpya inazunduliwa pale Uyole njia panda inaitwa Queen bar, nilikunywa pombe nakuja kuzinduka alfajiri nimelala kwenye mashamba ya mahindi ya chuo cha kilimo. Yaani badala ya kwenda guest niliyofikia nikaenda upande mwingine kabisa.
Unaweza jikataa chief [emoji3]
 
Ngoja niweke mkasa wangu mwingine ulitokea 2004, Jamaa zangu walitoka mgodini wana hela ya maana wamekuja na mshikaji wao watupambanishe kunywa pombe wanajua mimi kichwa ngumu kwenye bia. Nikawapa masharti kuwa nakunywa bia na si pombe kali. Wakaleta kreti moja ya Tusker na jamaa akapewa yakwake hiyo ni saa mbili asubuhi tumeshakula ugali kwa supu ya samaki. Kufika saa saba nimemaliza kreti jamaa kachemsha. Nikaaga nikaenda kulala, nakuja kushtuka kesho yake mchana majirani wanabomoa mlango wakijua nimekufa. Walichungulia dirishani wanaona mtu kalala chini wakajua nishaenda kwa Sir God. Niliugua siku 3 sijiwezi kabisa.
Ulikua unakata moto kisembe kabisa [emoji3]
 
Kipindi Niko chuo kikuu Cha Dar es Salaam miaka Ile. Tulikua tunakwenda kunywa wanzuki au mbege maeneo ya Riverside. Siku hiyo tulipata boom vzr Basi tukaona tukapate mbili tatu. Tukafika pale zilipo hostel za mabibo enzi hizo hazijajengwa kulikua na vibanda vya pombe za ovyo. Tukaanza kugida wanzuki. Wenzangu wakachoka wakaniacha na li barmeid Fulani umri umesogea. Kufika saa nne hivi nikaanza kuliona Ni beautiful Fulani. Basi nikalikokota Hadi hall one tower block kwa wale mliopitia shule za ukweli. Tukapanda mpaka kwa room na kufanya majambooz. Asubuhi naamka kwenda kukojoa nikaona ndala za yule mmama zilikua zimetoboka pale anapokanyagia na zimekarabatiwa na waya. Kumcheki kichwani ametia Ile kalkit ya muonekano Kama nywele zimetiwa maji au mafuta mengi. Kumbuka wanafunzi wameshaanza kukaa pale chini karibu na ofisi ya hall manager, wengine wanapiga stori wakitokea kafeteria kupata chai. Mimi Niko juu gorofani na msukule wangu unao dai lazima nimpeleke kituo Cha Basi. Madem wa chuo nao wapo pale stendi wanasubiri daladala. Mimi bado Nina msukule wangu anadai anataka kuwahi kutengeneza pombe mabibo. Aloo.
Nilimlaumu shetani na kazi zake zote. Nitampitishaje yule msukule mbele ya ma brazamen?
Dah nimecheka aisee [emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Enzi za lango la jiji Magomeni nilikutana na mama mmoja. Nikamtania kwamba huo mwendo Ni barabarani tu au hata chumbani? Akajibu hata chumbani. Maza alikua na kalio balaa. Nikamwambia wapi akasema Buguruni. Tukapanda kipanya Hadi Buguruni tukaenda kwake. Nikakuta ana mabinti ambao ndio saizi yangu wako barazani. Tukaingia chumbani kwake direct. Akawaambia binti zake watoke hapo barazani kwani hakutaka wasikie nikipakua mzigo maana mimama ya enzi zile ukichomeka tu anaanza kulia utadhani umetonesha kidonda. Asubuhi ndio pombe zimetoka nakutana na binti zake. Hiyo aibu siwezi kuisahau.
 
Wakati niko kijana mdogo ndio naanza kazi, kulikua na party ya kiofisi pale Agip Motel Dar. Sasa na Mimi wakati huo najifunza pombe nikanywa beer mbili, zilipopanda kichwani nikaanza kumtongoza mama MTU mzima aliyekua amekaa pembeni yangu. Mama akawa anacheka tu na wenzake. Mimi ndio nazidi kumtongoza na mkono uko kwenye Goti lake. Mwisho wa party kila MTU alirudi kwao. Jumatatu asubuhi mama aliniita ofisini kwake halafu akaniambia, nimuambie Yale maneno nikiyosema juzi kwenye party. Aisee hiyo aibu ilikua sio ya dunia hii.
 
Back
Top Bottom