Early 1990's tulipokea waalimu wawili wa kizungu katika shule yetu, kwa ule mpango wao wa kujitolea wa Peace Corps. Nikapewa jukumu la kuratibu mentorship yao. Baada ya miezi 6 akaja supervisor wao kutoka US anatembelea shule zenye Peace Corps, na kwetu akafika, akatambulishwa kwangu, tukajadili ya volunteers wake tukamaliza. Nikaona nitumie fursa kuunga urafiki huenda nami nikabahatika kwenda majuu kupitia networks hizo, kwa hiyo nikajitolea kumtoa out jioni akaone uzuri wa bongo. Tukaanzia kiwanja kilikuwa kinaitwa Bamboo kilikuwa nyuma ya KNCU hotel pale Moshi mzungu akatafuna nyama choma za kutosha na pombe. Next block baada ya hiyo Bamboo kulikuwa na restaurant wanauza vyakula asilia, akasema anataka kuonja, nikampeleka akalambalamba ng'ande akaiacha akaendelea na pombe. Alikuwa mwanaume wa mid 30's. Tukasogea naye Kilimanjaro, ilikuwa chini ya kahawa house (baadaye ilikuja kubomolewa wakajenga supermarket hata Nakumatt waliwahi kupanga pale), pale palikuwa na machangu wa kutosha na mzungu alishawaka na walikuwa wanamzengea sana lakini akawa anawapotezea. Mida ya saa 6 usiku nikachukua taxi kumrudisha hotelini kwake, amelewa chakari, mimi sikunywa pombe yoyote. Akasisitiza tukae naye siti za nyuma. Mzungu akajilaza kichwa pajani kwangu, nikajua amechoka. Punde si punde nikahisi kama anafungua zipu ya suruali yangu, na kweli akaingiza mkono akashika uume wangu. Nikamkurupua nikamtoa nikamrudisha aegemee kiti badala ya kuniegemea. Baadae akarudia kunipapasa maeneo hayo nikamtoa mkono. Akajisogeza akaninong'oneza sikioni "I'm sorry". Tumefika hotelini kwake akaonekana amelewa sana ikabidi nimsindikize hadi room, kufika ndani ananirembulia macho kama demu, lol! Nilitoka mbio!
Kesho yake alikuja ofisini yuko kawaida tu kama vile hakuna kilichotokea. Sikuelewa yale aliyotaka ni kwa sababu ya pombe tu au kuna zaidi!
Imepita miaka mingi, na enzi zile hatukuwa na email wala mobile phones kwa hiyo tulipoteana baada ya kuandikiana barua mbili tatu ile miaka ya mwanzo.