Kuna jamaa yangu best sana. Alinitangulia kuoa kidogo Ila kazini tulikua pamoja na tulinunua viwanja sehemu moja Tabata na kuanza kujenga polis post wote. Kwa wale dotcom polis post Ni nyumba ya chumba sebule chumba choo na bafu nnje.
Ok. Tuendelee na Hadith. Christmas moja tulienda mkesha Kama kawaida, kutoka kanisani tukahamia bar enzi zile hakuna Makonda Wala Nini, kwenye grosare za mtaani bia mnapiga mpaka majogoo. Basi tukazianza Ile saa tano usiku, hapo ujue wanywaji wote Ni majirani na tunajuana, sasa unakuta mtu una beer tatu hazijafunguliwa, Ni mwendo wa kata mti panda miwili. Baas bwana, ilipofika majogoo mie na jamaa yangu na jirani yangu toka mkoani Geita tukaanza kurudi nyumbani. Kufika jamaa kaingia kwake kwa mkewe na watoto wawili na mahaus geli wawili. Unajua siku ya Xmas kina mama hasa wanaokaa Tabata hupenda kupikia nje madishi kibao. Pale pilau, huku kitimoto, pale kuku, huku hausgel huyu anakata kachumbari, yule anawasha mkaa mama anasupavais na vijana wake wanacheza na baiskeli. Kufika muda wa saa tatu watu wote wako nje. Jamaa yangu huyu ambae hajaenda jando mkojo ukambana. Pombe zikamtuma kwamba bado Ni Kuna giza hivyo anaweza kwenda kukojoa chap akiwa uchi na kurudi kuendelea na usingizi. Jamaa yangu akatoka nje Kama alivyozaliwa na kukojolea ukuta karibu na dirisha lake. Mke na mahausgel na watoto wameshikwa butwaa maana kidogo akojolee ungo uliokua na viungo. Jamaa akaitingisha Kama kawaida ya wanaume na kuingia ndani kuendelea na usingizi. Jamaa kauchapa Ila kunako saa Saba harufu ya pilau ikamuamsha. Mke akamiwahi na kumwambia kabla hakatoka nje Tena na kumpasha. ULICHOTENDA LEO HAKINA MFANO. UMERUDI ALFAJIRI UMEONA BADO HAITOSHI, UNAKUJA KUNIDHALILISHA MBELE YA HAUSEGELI NA MAJIRANI KWA KUTOKA NJE UCHI. jamaa yangu kawa mkali na kusema hajatoka nje uchi. Bi mkubwa kaenda kumuonyesha ukutani jamaa yangu huyu mbabe alipokojolea maana japo mkojo ulishakauka lkn ramani ilikuwapo. Basi jamaa ilibidi awe mpole na kuapa pia alihamia makanisa ya walokole ambayo hayaruhusu pombe.