Visa gani pombe ilikufanyia hutasahau?

Visa gani pombe ilikufanyia hutasahau?

Kama unainywa kwa kiasi chako nadhani si mbaya kabisa. Sisi wengine ilikuwa ni majanga kila siku.
Mkuu nakunywa kwa kiasi changamoto moja nakunywa na kampani kubwa nafilisika nakosa mpaka hela ya kula
 
Mkuu nakunywa kwa kiasi changamoto moja nakunywa na kampani kubwa nafilisika nakosa mpaka hela ya kula
Hiyo ni changamoto kubwa sana, huwa inatufanya kukosa akiba kabisa, yaani ikitokea dharula inakuwa ni majanga. Ni kujaribu kubalance na kupanga kiasi cha kutumia kulingana na kipato chako mkuu
 
Amen Amen nategemea updates zaidi

Hata kama hutaacha kabisa lakini ukipiga mara moja ukazima ukatulia miezi au mwezi si mbaya

Sio sawa na kuzima daily unapoteza vingi, Afya, Heshima na pesa

Unazungumzia kutetema mikono naelewa unachozungumza niliwahi kufikia stage hiyo, bahati mbaya kazi yangu ni ya kuandika sana, ikija kazi nakosa amani, nazunguka zunguka tu huku na huko mradi hiyo kazi afanye mwingine mimi siwezi kabisa

Kuna dada nilimuonyesha huu uzi akaanza kunishuhudia jinsi mwanaume wake anateswa na uraibu wa pombe kwa kweli mpaka nilidhani ni wewe ila kuna vitu ni tofauti kidogo

Huyo mwenzio(mwanaume wa huyo dada) nafikiri anakuzidi parefu sana ikiwa umeshaandika yote hapa

Yeye alipelekwa mpaka sober alipotoka tu akarudishwa nyumbani na mkokoteni ameokotwa siku hiyo hiyo

Bidada amekata tamaa ameachana nae na anadhani kwa jamaa alipofikia hana muda anafariki


Mungu atakusaidia mkuu uraibu wa aina yoyote ni mbaya sana unatesa mhusika mpaka watu wa karibu
Alcoholic Syndrome inatibika jamani
 
Amen Amen nategemea updates zaidi

Hata kama hutaacha kabisa lakini ukipiga mara moja ukazima ukatulia miezi au mwezi si mbaya

Sio sawa na kuzima daily unapoteza vingi, Afya, Heshima na pesa

Unazungumzia kutetema mikono naelewa unachozungumza niliwahi kufikia stage hiyo, bahati mbaya kazi yangu ni ya kuandika sana, ikija kazi nakosa amani, nazunguka zunguka tu huku na huko mradi hiyo kazi afanye mwingine mimi siwezi kabisa

Kuna dada nilimuonyesha huu uzi akaanza kunishuhudia jinsi mwanaume wake anateswa na uraibu wa pombe kwa kweli mpaka nilidhani ni wewe ila kuna vitu ni tofauti kidogo

Huyo mwenzio(mwanaume wa huyo dada) nafikiri anakuzidi parefu sana ikiwa umeshaandika yote hapa

Yeye alipelekwa mpaka sober alipotoka tu akarudishwa nyumbani na mkokoteni ameokotwa siku hiyo hiyo

Bidada amekata tamaa ameachana nae na anadhani kwa jamaa alipofikia hana muda anafariki


Mungu atakusaidia mkuu uraibu wa aina yoyote ni mbaya sana unatesa mhusika mpaka watu wa karibu
Mkuu bado naendelea poa, hadi sasa nimeanza kusahau kinywaji kabisa. Huu uzi huwa naamua kuupitiamara kwa mara na kupata nguvu zaidi
 
  • Thanks
Reactions: T11
Nikiwa Mtwara kikazi miaka michache iliyopita.
Siku hiyo nimelewa chakali nikachukua wale watu wetu waleeee wa 20K mnamalizana.
Aisee kutokana na ule ulevi nilivaa condom lakini mbeleni nikashindwa kukojoa, upumbavu wa ulevi ukanishawishi nikavua condom yaan nikapiga game pekupeku tena kwa ma.la.ya wa kujiuza.
Pombe zimeisha naziona condom zangu hazijatumika ziko pembeni ya kitanda.

Nilikosa raha kwa miezi mitatu mfululizo, niliapa sitarudia kuchukua demu ugenini tena nikiwa nimelewa. Siku naenda kupima nakuta niko mzima nilipiga magoti kumshukuru Mungu, Dr. alicheka sana
Mkuu ulipiga magoti hapo hapo chumba cha dokta?
 
Jamani pombe we acha tu.
Kule kijijini Kuna pombe inaitwa dengerua au boha. Hii pombe Ni very potent. Wengi wanainywea bar/vilabuni lakini wale watu matawi wa kijijini Kama walimu, daktari, nesi na mchungaji huwa Wana agiza na kuzama ndani ya nyumba ya mwalimu mmoja na kuanza kukata kiu.
Kuna siku moja shetani alitembelea kile Kijiji na kwa bahati mbaya team matawi walikua wanakata kiu Kama kawaida. Walikuweko walimu watatu, nesi wa Kijiji na mchungaji nae alikwenda kugida akiamini Hawa watamtunzia Siri.
Wakati wanaendelea kukata kiu shetani akamnongoneza mchungaji kwamba aondoke na yule nesi wakapumzike kwenye migomba kwa dharula. Nesi nae hakupenda kumpunja mchungaji starehe aliyoipenda pamoja na utu uzima wake.
Walivyokua wanatumia sign language na kukonyezana walidhani wale wengine hawaoni. Giza lilipoingia wakaona umefika muda muafaka.
Mara nesi akaaga anatoka, dakika mbili nyingi mchungaji nae akajifanya ametosheka. Nesi kwake Kuna watoto mchungaji nae kwake Kuna mke , watoto na kijukuu kimoja hivo wakaamua waende green lodge a.k.a kwenye migomba kupeana uroda.
Mchungaji alivua nguo zote ili zisichafuke kwenye zoezi Hilo ovu otherwise wife atastuka. Nesi nae kaamua kuvua zote ili zisiingie udongo. Wakaanza kupeana mahaba, kumbe mwalimu mmoja alikua anamuwania yule nesi sasa kitendo Cha nesi kuchukuliwa kirahisi rahisi na mchungaji kilimuudhi sana hivyo akaona awakomeshe once and for all. Yeye aliwafuatia nyuma tartiib na walipokua kwenye mchakato wa starehe yule mwalimu mkware akachukua nguo zao zote Hadi boxer ya mchungaji na kufuli na sidiria za nesi na pombe ikamtuma kuzipeleka LIVE kwa mke wa mchungaji. Alipofika alimwambia mama mchungaji mumeo Ni mzinzi Kama huamini nguo zake hizi hapa na za huyo kimada wake.
Kile kitendo Cha nguo zao kuchukuliwa mchungaji hakukiona maana alikua anakaribia kufika Mawenzi lakini nesi aliona. Kabla hata mchungaji hajafika Mawenzi vizuri nesi alimwambia mwalimu Fulani amechukua nguo zao na kuondoka zazo. Ile habari ulikifanya kitendea uroda Cha mchungaji kusinyaa chap Kama Kobe anavyoingiza kichwa kwenye kasa lake.
Kwanza kabisa waliondoka pale vile vile wakiwa uchi lakini hakuna aliyemtamani mwenzake Tena. Mchungaji pombe zilinitoka na alikua anamuona nesi Kama Dada yake mkubwa.
Mchungaji hakurudi nyumbani siku Ile ilhali akiwa uchi, nesi alizubaa na usiku wa manane akarudi kwake na kuapa hatarudia pombe Tena akirudia afe.
Mchungaji haikueleweka Ila saa mbili asubuhi kesho yake akiwa na nguo zisizokua zake na zilizombana sana alionekana kwa mkuu wa Jimbo na barua ya kujiuzulu uchungaji bila sababu za msingi.
Huku nyumbani nesi nae Hana raha maana nguo zake pamoja na chupi na sidiria viko kwa mbaya wake.
Ukitaka kumuumiza mwanamke wa kipare kisaikolojia chukua chupi yake ambayo haijafuliwa halafu tokomea nayo. Sasa huyu chupi iko kwa mbaya wake ataanzaje? Sio chupi tu na khanga na gauni na sidiria.
Ina maana mke wa mchungaji alikua amemuweka nesi anapomtaka.
Itaendelea...........
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]

Duh hii ilikuwa babkubwa.
 
Hahahaa nikiwa Chuo mwaka wa pili nililala kwenye Mtaro wa maji machafu halafu fresh tu, sasa Imagine Dom usiku kunavyokuwa na baridi hilo wala halikufua dafu. Nakuja kushtuka asubuhi kelele za watu wakielekea pindi! Aisee nilisimama pombe kama miezi sita hivi
[emoji3][emoji3][emoji3]
 
Nilipiga magoti room kwa Dr. alikuwa kijana mwenzangu tu ni private hospital ndio alikuwa kaajiriwa, so kwa umri wake ni rika langu stori nyingi sana.
Hongera sana aisee, Vipi ulirudia kubeba beba milupo tena hovyo?
 
Mkuu kwanza nashukuru kwa kunipa pole, pili tangu tarehe 18/10/2020 sijagusa kabisa hiyo kitu. Hilo la mdunguaji huko Tarime pengine sitokuwa kwenye nafasi nzuri sana ya kulisemea. Kwani mtuhumiwa alikamatwa akiwa kafika huko Tanga na sijajua kesi yake iliishia wapi. Ila aliyekuwa amekamatwa kimakosa mwanzoni na akapata makashikashi kibao kazini hadi kupelekea sherehe za kufunga ndoa yake zikaarishwa najua alishaachiwa na anaendelea na shughuli zake. Habari zisitothibitika ni kuwa wengi waliouwawa waliwahi kufanya kazi na huyo muuaji katika mgodi wa North Mara na pengine (hisia tu) walitokea kudhulumiana kwenye deals zao.
Kuhusu kufanya kazi mgodini sina uhakika. Ila waliouawa wengi ni wananchi wa kawaida kabisa kwakuwa yeye alikuwa havamii nyumba. Mlikuwa mnakutana usiku na maisha ya akheraa yanakuhusu. Ameua sana wanafunzi waliokuwa wakienda kujisomea usiku. Ameua kina mama wanaofanya biashara ndogondogo. Kifupi aliua watu wengi wasio na hatia kabisa.
 
Kuhusu kufanya kazi mgodini sina uhakika. Ila waliouawa wengi ni wananchi wa kawaida kabisa kwakuwa yeye alikuwa havamii nyumba. Mlikuwa mnakutana usiku na maisha ya akheraa yanakuhusu. Ameua sana wanafunzi waliokuwa wakienda kujisomea usiku. Ameua kina mama wanaofanya biashara ndogondogo. Kifupi aliua watu wengi wasio na hatia kabisa.
Hao wawili waliouawa siku moja wote walifanya kazi mgodini, il mmoja aliacha akaanza biashara zake. Hayo ndiyo yalikuwa yanasemwa na watu wao wa karibu (kama ni kweli)
 
Yupo jamaa yangu Mnyiramba mtu na kazi yake na heshma tele. Hivi majuzi tu alikwenda pale Loliondo Kibaha kula nyama choma peke yake asubuhi ya saa tatu. Basi alikua amekaa meza moja na mdada lakini hawajuani nadhani mdada ni danga. Pale nyama tunakula kwa round. Yaani round one labda utumbo wa kuchoma au supu ya utumbo fresh then beer, round two hii ndio Ile yenyewe zinakuja nyama nyingi, kachumbari, pilipili, sauce nk. Then beer halafu jioni Kuna kajiround kakupunguza pombe mwekichwa. Sasa kwasababu huyu mnyiramba alikua amekaa na mdada kama ilivyo kwa watanzania ilibidi jamaa amkaribishe binti nyama na beer. Binti nae mchango wake ulikua story za umbea na kuchekacheka.

Basi wamekaa mpaka moja usiku, kumbe kuna kipindi jamaa alimuambia mdada kwamba hana mke. Wakati wa kutoka jamaa alimpa binti lifti lakini kajisahau kapitiliza nae mpaka maeneo ya Pangani Kibaha. Kumbe jamaa kichwani hana coordination. Akatoka kwenye gari huku amemshika yule mdada wa watu mkono huku anamuongoza moja kwa moja kwenda chumbani au master bedroom. Mke wa jamaa alikua kwenye jikoni hivyo alivyowaona alistuka Ila wale walevi hawakumuona waif. Kufumba na kufungua jamaa anaingia na mdada chumbani wako bwii.

Waif alienda kumshika mdada na kuanza kumshushia kipigo Cha mbwa Koko wa Dodoma. Kipindi hicho mdada anaadhibiwa jamaa yangu alikua kitandani na usingizi wa pono. Kilichomuokoa mdada kutoka kwenye kipigo ni makelele ya waif na majirani kuja fasta kuokoa. Maana alikua anapiga huku analia baba watoto kaonyesha dharau ya kiwango Cha SGR.
 
Yupo jamaa yangu mnyiramba mtu na kazi yake na heshma tele.
Hivi majuzi tu alikwenda pale Loliondo Kibaha kula nyama choma peke yake asubuhi ya saa tatu. Basi alikua amekaa meza moja na mdada lkn hawajuani nadhani mdada Ni danga. Pale nyama tunakula kwa round. Yaani round one labda utumbo wa kuchoma au supu ya utumbo fresh then beer, round two hii ndio Ile yenyewe zinakuja nyama nyingi, kachumbari, pilipili, sauce nk. Then beer halafu jioni Kuna kajiround kakupunguza pombe mwekichwa. Sasa kwasababu huyu mnyiramba alikua amekaa na mdada Kama ilivyo kwa watanzania ilibidi jamaa amkaribishe binti nyama na beer. Binti nae mchango wake ulikua story za umbea na kuchekacheka.
Basi wamekaa mpaka moja usiku, kumbe Kuna kipindi jamaa alimuambia mdada kwamba Hana mke.
Wakati wa kutoka jamaa alimpa binti lifti lakini kajisahau kapitiliza nae mpaka maeneo ya Pangani Kibaha. Kumbe jamaa kichwani Hana coordination. Akatoka kwenye gari huku amemshika yule mdada wa watu mkono huku anamuongoza moja kwa moja kwenda chumbani au master bedroom. Mke wa jamaa alikua kwenye jikoni hivyo alivyowaona alistuka Ila wale walevi hawakumuona waif. Kufumba na kufungua jamaa anaingia na mdada chumbani wako bwii.
Waif alienda kumshika mdada na kuanza kumshushia kipigo Cha mbwa Koko wa Dodoma.
Kipindi hicho mdada anaadhibiwa jamaa yangu alikua kitandani na usingizi wa pono. Kilichomuokoa mdada kutoka kwenye kipigo Ni makelele ya waif na majirani kuja fasta kuokoa. Maana alikua anapiga huku analia baba watoto kaonyesha dharau ya kiwango Cha SGR.
Kama inakuja hiviiii afu inakataaa
 
Hongera sana aisee, Vipi ulirudia kubeba beba milupo tena hovyo?
Niliapa sirudii na mpaka leo nasema sitarudia huo upuuzi. Unajua maisha ni kitu delicate sana, unaweza kuua ndoto zako zote kwa starehe ya sekunde kadhaa.
 
Back
Top Bottom