Visa gani pombe ilikufanyia hutasahau?

Visa gani pombe ilikufanyia hutasahau?

Mwaka 2008, Nilikuwa Mbeya Tukuyu Kikazi, Nilikuwa nimetokea Mbeya Mjini ambapo Kuna baridi, Dose yangu ilikuwa Tusker Kumi,

Kwenda Tukuyu Nikaendelea na dose ileile bila kugundua kuwa Hali ya hewa ya Tukuyu Ni Tofauti na Mbeya Mjini. Na Pombe. Hukolea kwenye Joto, Tukuyu Kuna Joto.

Mzee Mzima Nikavesha Kama kawaida, mpaka saa tano FULANI hivi, Sasa kimbembe Nikasahau Guest, Nikaenda kugonga Nyumba ambayo Inaangaliana na Guest Huku Povu likinitoka kwanini wafunge na Mimi bado sijarudi.

Ebwana mlango ulifunguliwa na Mbaba mmoja akiwa na njemba tatu (Watoto wake) Nilichezea vitasa vyakutosha kila nikiweka Gurd wapi.

Niliokolewa na Staff wenzangu Baada ya kuhisi kuwa sijarudi na wanasikia kelele za sauti yangu.

Asee hiyo ilikuwa moja Ila Pombe kuacha bado nafikiria.
rest in peace mkuu...anh kumbe ulipona
 
Jamaa umenikumbusha mbali matukio ni mengi ila moja ni hili:
Wakati nikiwa chuo mwaka wa mwisho tulikuwa tunafanya vikao vya tungi ,kama kawaida faru john mtu nne ila nilikua nachelewa kulewa tofauti na wenzangu kwa bahati mbaya Siku iyo nlikula slace mbili za mkate ,nikakaza kibingwa Hamna kutegeana nakumbuka tulikunywa konyagi nyingi sana baadae tukasepa kila mtu kivyake njiani nikanunua chips+mishkaki ili nikalie geto kufika geto nikaanza kukata moto kiasi kwamba nilishindwa kuingiza funguo kwenye tundu la kofuli nikajisogeza pembeni Luna tofali nkakaa cha ajabu ambacho kilinishangaza alikuja mbwa sijui wa wapi akaninyang'anya mfuko wenye kiepe na mishkaki nilishindwa hata kumwambia shhh toka maana mdomo haufunguki,nikaamua kujilaza palepale hadi asubui..nikajifunza pombe bila msosi noma pia niligundua ukinywa nyagi na glass macho yanakufa
Hii kubwa kuliko [emoji23][emoji23]
 
Nimemaliza form six nimerudi home hyo week kulikua na harusi ya bro mmoja hivi jirani. So tukaenda harusini nikajifanya na mimi nimekua nikanywa castel 6 sio light. Aisee nilicheka kuanzia ukumbini,barabara nzimaaa nacheka nakuongea hovyo hovyo. Kesho yake nilipokea simu kila pande nalaumiwa nimekua mtoto gani nimejifunza tabia mbaya na mengine mengii, mbaya zaidi ni mama yangu aliekua ananiamini kwa kweli nilijiona kama nimemuabisha. Toka siku hyo sijawahi kurudia na wala sitarudia kunywa hiyo kitu. Kwanza hazina faida yyt niliambulia kuumwa tuu kichwa asubui. Ni miaka kumi na kitu ilopita
Ilikiwa mwaka gani mkuu?

Sent from my Infinix X680 using JamiiForums mobile app
 
Baada ya kupambazuka, ulijicheki? Ulikuwa salama sehemu za kukalia?
Binafsi nakunywa pombe mara mojamoja, naweza kupitisha mwezi sijanywa ila nikinywa huwa nalipiza siku ambazo sikunywa kabisa. Hii imenikuta wiki chache zilizopita tulikuwa na event na marafiki tunaotoka sehemu moja, kwenye pombe mbuzi anahusika nilisimamia kitengo.

Nilikunywa mpaka K Vant nikaiona kama soda, nakuja kustuka pombe imenizidi kiasi hata kutembea ilikuwa noma. Sifanyi fujo nikilewa kila mtu alifurahi lakini balaa lipo kwa ndugu zangu kujua kuwa ninakunywa. Busara ilitumika simu yangu nikaicha kwa mtu niipate nikiwa fresh.

Ase nilifanya safari ya saa 1 na nusu peke yangu nikiwa nimelewa na sijui nilifikaje nyumbani, kuja kustuka ni asubuhi niko kitandani tatizo limebaki kwa ndugu zangu. Wakati nimeacha simu kwa rafiki nilipigiwa jamaa akapokea na kuwaambia niko kwenye matatizo ile kitu ilizua taharuki watu hawajalala kuulizia hali yangu maana mimi sikupatikana tena.

Hii kitu imeniweka sehemu mbaya sana hakuna mtu anataka kunielewa tena. Ukweli nimekwama nimeamua kuacha pombe maana naona itanigombanisha na ndugu.
 
Dah!!!!,Weee sasa ulifika mbali sana.Hivi hadi mtu unachanganyikiwa hivyo unakuwa umekunywa kiasi gani?.Mbona mimi huwa nakunywa sana lkn sijawahi kufikia hatua hiyo?!!.
Jua tank lako kubwa mkuu, ujazo wa tank la starlet siyo sawa na tank la Verosa

Sent from my Infinix X680 using JamiiForums mobile app
 
Kuna pombe hio inaitwa 211 kule ughaibuni nilikunywa kopo mbili halafu nilikwenda club. Yaani nilikuwa najiona kama Superman mikono kama ndege inayotaka kuruka. Nikaingia club nikamchapa mzungu flani nikatolewa nje nikaanza kuwatukana mabausa sijui kilitokea nini ila niliishia hospital wiki 2 na miezi 6 home.[emoji23][emoji23]

View attachment 1576989


Ndukiiiii [emoji2089][emoji2089][emoji2089]
Pole sana.
Hii beer sio nzuri. Ukipata tena nafasi usinywe hii.
 
Mimi nilipata kazi 3, kisa nilikuwa napiga ile asubuhi kabla ya interview viroba vinne vya Konyagi nachanganya na sprite. Kuna sehemu nilifanyiwa interview na wazungu, ilikuwa Moshi kiwanda cha sukari, tukiwa njiani na wenzangu tunarudi Moshi mjini kabla hata hatujapata gari HR akanipigia kuwa nimepata kazi nisiondoke kesho nikasaini mkataba. Ila niliachana nao, mshahara kiduchu sana. Hata hii kazi ninayofanya sasa niliipata kwa nguvu za viroba.
Nipe maujanja ya interview brother.
 
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣

Jamaa umenikumbusha mbali matukio ni mengi ila moja ni hili:
Wakati nikiwa chuo mwaka wa mwisho tulikuwa tunafanya vikao vya tungi ,kama kawaida faru john mtu nne ila nilikua nachelewa kulewa tofauti na wenzangu kwa bahati mbaya Siku iyo nlikula slace mbili za mkate ,nikakaza kibingwa Hamna kutegeana nakumbuka tulikunywa konyagi nyingi sana baadae tukasepa kila mtu kivyake njiani nikanunua chips+mishkaki ili nikalie geto kufika geto nikaanza kukata moto kiasi kwamba nilishindwa kuingiza funguo kwenye tundu la kofuli nikajisogeza pembeni Luna tofali nkakaa cha ajabu ambacho kilinishangaza alikuja mbwa sijui wa wapi akaninyang'anya mfuko wenye kiepe na mishkaki nilishindwa hata kumwambia shhh toka maana mdomo haufunguki,nikaamua kujilaza palepale hadi asubui..nikajifunza pombe bila msosi noma pia niligundua ukinywa nyagi na glass macho yanakufa
 
Kali yangu moja ya tungi nipo bar na friends kula sana tungi hata siku mbuki idadi ya chupa mida ya kama saa saba ucku nikarudi zangu home fresh nacho kumbuka nilifungua geti fresh nika ingiza gari vizuri tu kumbe bhana nilipo fika nili park siku funga mlango wa gari na nika iacha ipo silence siku izima hii nilikuja kuambiwa asubuh.

Mbaya kuliko nika ingia ndani moja kwa moja mpaka kwenye chumba cha dada wa kazi nika lala naskia eti dada wa kazi kuona nime vamia chumba akaenda kulala sitting room ila wife hakuelewa kabisa ilo somo maana nakuja kushtuka asubuhi nipo chumba cha dada wa kazi ila baadae atakua ali elewa tu maana nili rudisha chenji kwenye shuka za dada wa kazi akajua huyu jamaa atakuwa alizidiwa na tungi

Ila ilinichukua siku nzima kumuelewesha ilo jambo.
 
Juzi juzi tu hapa nimepanda daladala sayansi kijitonyama na jamaa amelewa saa 6 mchana jua kali,
tumetoka pale tunaelekea mwenge tumefika adi mataa pale mwenge anamwambia konda amuache sayansi na wakati alipopandia gari ndo sayansi[emoji23][emoji23]
[emoji23][emoji23][emoji23]daah qmmk
 
Baada ya kuutwika kwenye sherehe ya kazini nilimtongoza mama mmoja mwenye cheo chake, nae akawa anacheka tu. Mimi ndio nazidi kumpa maneno mbele ya watu.

Party iliisha kila mtu akaenda zake. Jumaatatu yule mama akaniita na kuniambia Ni mwambie yale maneno niliyo muambia siku ya party halafu alikua serious.
 
Back
Top Bottom