Visa gani pombe ilikufanyia hutasahau?

mwakavuta

Member
Sep 22, 2020
99
302
Binafsi nakunywa pombe mara mojamoja, naweza kupitisha mwezi sijanywa ila nikinywa huwa nalipiza siku ambazo sikunywa kabisa. Hii imenikuta wiki chache zilizopita tulikuwa na event na marafiki tunaotoka sehemu moja, kwenye pombe mbuzi anahusika nilisimamia kitengo.

Nilikunywa mpaka K Vant nikaiona kama soda, nakuja kustuka pombe imenizidi kiasi hata kutembea ilikuwa noma. Sifanyi fujo nikilewa kila mtu alifurahi lakini balaa lipo kwa ndugu zangu kujua kuwa ninakunywa. Busara ilitumika simu yangu nikaicha kwa mtu niipate nikiwa fresh.

Ase nilifanya safari ya saa 1 na nusu peke yangu nikiwa nimelewa na sijui nilifikaje nyumbani, kuja kustuka ni asubuhi niko kitandani tatizo limebaki kwa ndugu zangu. Wakati nimeacha simu kwa rafiki nilipigiwa jamaa akapokea na kuwaambia niko kwenye matatizo ile kitu ilizua taharuki watu hawajalala kuulizia hali yangu maana mimi sikupatikana tena.

Hii kitu imeniweka sehemu mbaya sana hakuna mtu anataka kunielewa tena. Ukweli nimekwama nimeamua kuacha pombe maana naona itanigombanisha na ndugu.
 
Siku ambayo siwezi isahau ni siku nimekunywa pombe kisha nikaenda zangu home Ile nimeingia kulala mkojo ukanibana ikabidi nitoke chumbani nikakojoe baada ya kuenda chooni nikaenda jikoni kukojoa alafu nikaludi zangu kulala kesho yake asubuh ebanaeeeeee Sito sahau
Wewe pombe haikufai. Tuachie malegend.
 
Kuna pombe hio inaitwa 211 kule ughaibuni nilikunywa kopo mbili halafu nilikwenda club. Yaani nilikuwa najiona kama Superman mikono kama ndege inayotaka kuruka. Nikaingia club nikamchapa mzungu flani nikatolewa nje nikaanza kuwatukana mabausa sijui kilitokea nini ila niliishia hospital wiki 2 na miezi 6 home.😂😂

images.jpeg



Ndukiiiii 🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️
 
Siku ingine nilifakamia sana pombe mchanganyiko nilikuwa na binamu yangu wakati tunaondoka tupo ndani ya daladala mimi tu ndo nilikuwa muongeaji watu wote vicheko.

Tuliposhuka nikawa naenda njia ambayo sio binamu yangu akaniita.

Tulipofika nyumbani nikasema ngoja nikanywe ya mwisho wakati narudi nikapotea tena nyumbani nikashtuka kuwa nimepotea nyumba baada ya kuona sifunguliwi mlango.
 
Siku ingine nilifakamia sana pombe mchanganyiko nilikuwa na binamu yangu wakati tunaondoka tupo ndani ya daladala mimi tu ndo nilikuwa muongeaji watu wote vicheko. Tuliposhuka nikawa naenda njia ambayo sio binamu yangu akaniita.

Tulipofika nyumbani nikasema ngoja nikanywe ya mwisho wakati narudi nikapotea tena nyumbani nikashtuka kuwa nimepotea nyumba baada ya kuona sifunguliwi mlango.
😅😅😅😅😂😂😂
 
Siku ingine nilifakamia sana pombe mchanganyiko nilikuwa na binamu yangu wakati tunaondoka tupo ndani ya daladala mimi tu ndo nilikuwa muongeaji watu wote vicheko. Tuliposhuka nikawa naenda njia ambayo sio binamu yangu akaniita.

Tulipofika nyumbani nikasema ngoja nikanywe ya mwisho wakati narudi nikapotea tena nyumbani nikashtuka kuwa nimepotea nyumba baada ya kuona sifunguliwi mlango.
Kifo mkononi, bahati hukushukiwa wizi.
 
Mwaka 2008, Nilikuwa Mbeya Tukuyu Kikazi, Nilikuwa nimetokea Mbeya Mjini ambapo Kuna baridi, Dose yangu ilikuwa Tusker Kumi,
download (4).jpeg


Kwenda Tukuyu Nikaendelea na dose ileile bila kugundua kuwa Hali ya hewa ya Tukuyu Ni Tofauti na Mbeya Mjini. Na Pombe. Hukolea kwenye Joto, Tukuyu Kuna Joto.

Mzee Mzima Nikavesha Kama kawaida, mpaka saa tano FULANI hivi, Sasa kimbembe Nikasahau Guest, Nikaenda kugonga Nyumba ambayo Inaangaliana na Guest Huku Povu likinitoka kwanini wafunge na Mimi bado sijarudi.

Ebwana mlango ulifunguliwa na Mbaba mmoja akiwa na njemba tatu (Watoto wake) Nilichezea vitasa vyakutosha kila nikiweka Gurd wapi.

Niliokolewa na Staff wenzangu Baada ya kuhisi kuwa sijarudi na wanasikia kelele za sauti yangu.

Asee hiyo ilikuwa moja Ila Pombe kuacha bado nafikiria.
 
Back
Top Bottom