Visa gani pombe ilikufanyia hutasahau?

Visa gani pombe ilikufanyia hutasahau?

Kuna pombe inaitwa "PINGU" hii ukiagiza tu, bila kujali kama wewe ni gangwe, kijogoo, kingunge, taita, mwamba au memba wa kudumu lazma mama muuza akufunge kwanza kamba upande wa chini wa suruali ndo mwende sawa.
Nilimuona mzee mmoja kajiharishia kweli kweli, walikuwa wanasema amekunywa hiyo hiyo Pingu huko Morogoro enzi hizo
 
Mwaka 2009 nilikwenda Tabora kikazi,sasa kwenye ofisi ya mo ule kuna jamaa akatokea kunizoea nikamuomba jioni anizungush zungushe kuifahamu mitaa,jioni ilivyofika akanipigia simu tukakutana na kuanza kupiga misele,nikamuuliza baa gani imechangamka akanipeleka kipindi hicho napiga sna mitungi sasa hivi nimeacha,kufika nikaagiza kilimanjaro yeye akaagiza konyagi basi piga vyombo sana tu.Ghafla mshikaji akaanza kulia bwana,lia vibaya mno nikapata kazi ya kuanza kubembeleza mtu mzima na mindevu yake anacholia sikijui na hadi leo sifahamu alikumbuka nini.
Uliingia mtumbwi wa Vibwengo hii siku [emoji23][emoji23][emoji23]

Sent from my 220333QAG using JamiiForums mobile app
 
Enzi za lango la jiji Magomeni nilikutana na mama mmoja. Nikamtania kwamba huo mwendo Ni barabarani tu au hata chumbani? Akajibu hata chumbani. Maza alikua na kalio balaa. Nikamwambia wapi akasema Buguruni. Tukapanda kipanya Hadi Buguruni tukaenda kwake. Nikakuta ana mabinti ambao ndio saizi yangu wako barazani. Tukaingia chumbani kwake direct. Akawaambia binti zake watoke hapo barazani kwani hakutaka wasikie nikipakua mzigo maana mimama ya enzi zile ukichomeka tu anaanza kulia utadhani umetonesha kidonda. Asubuhi ndio pombe zimetoka nakutana na binti zake. Hiyo aibu siwezi kuisahau.
Naye alikuwa amelewa? Yaani simple tu 'wapi, Buguruni' hata bila kutongoza!
 
Matukio mawili 1.Nilimtongoza mama mkwe infact sio mama wa mke wangu lakini ni mama mdogo wa mke wangu kwa kweli ni kifaa na tumelingana alishindwa nipa mchezo vile alimuheshimu tu mtoto wa dada yake 2.Nilitembea hadi asubuhi sifiki ninakokwenda. kufika asubuhi jamaa mmoja akanishtua hapo ndio nikajua kumbe nilipotea
 
img_70_1658867050309.jpg
MIMI SINYWI POMBE KABISA
 
Niliamka kwenda chooni usiku.. Niliporudi chumbani namsimulia mke wangu.. Baby leo nimeona maajabu.. Nimefungua tu mlango wa chooni taa ikawaka yenyewe.. Nilipomaliza ile nafunga mlango taa ikajizima yenyewe.. Wee..!!😃😃😃 Nilikula Bonge la bao.. Naskia Pumbavu umekojoa tena kwenye Friji.. 😃😃😃😃 Toka siku hiyo pombe siitaki tena..
 
Tarehe 20 nitatimiza miezi mitatu bila kunywa pombe....

Miezi mitatu bila kufanya ngono.
Miezi mitatu bila kula wanga (ugali na wali)

Itakua miezi mitatu natimiza kilo 75 kutoka kilo 96.....

Super....
Sasa ngono unamuachia nani mkuu
 
Mwaka 2008, Nilikuwa Mbeya Tukuyu Kikazi, Nilikuwa nimetokea Mbeya Mjini ambapo Kuna baridi, Dose yangu ilikuwa Tusker Kumi,
View attachment 1614054

Kwenda Tukuyu Nikaendelea na dose ileile bila kugundua kuwa Hali ya hewa ya Tukuyu Ni Tofauti na Mbeya Mjini. Na Pombe. Hukolea kwenye Joto, Tukuyu Kuna Joto.

Mzee Mzima Nikavesha Kama kawaida, mpaka saa tano FULANI hivi, Sasa kimbembe Nikasahau Guest, Nikaenda kugonga Nyumba ambayo Inaangaliana na Guest Huku Povu likinitoka kwanini wafunge na Mimi bado sijarudi.

Ebwana mlango ulifunguliwa na Mbaba mmoja akiwa na njemba tatu (Watoto wake) Nilichezea vitasa vyakutosha kila nikiweka Gurd wapi.

Niliokolewa na Staff wenzangu Baada ya kuhisi kuwa sijarudi na wanasikia kelele za sauti yangu.

Asee hiyo ilikuwa moja Ila Pombe kuacha bado nafikiria.
Uongo. Tukuyu kuna baridi zaidi kuliko Mbeya Mjini.
 
Nlienda mkoa flani kikazi. Jamaa yangu akanialika weekend kwake. Nikaenda akanitoa out tukapige maji. Nlikunywa karibia crate zima la beer safari. Baadaye anasema nikaanza kuongea kwa uchungu sana nikilia kwa kumuonea huruma kuwa jamaa hajajenga ila anakunywa beer daily. Nlimsema sana bahati mbaya tulipokuwa pale alileta na mchepuko wake na mchepuko akaja na rafiki yake. Jamaa alijisikia aibu sana.

Bahati mbaya alikuwa amenitaka siku hiyo nikalale kwake ilikuwa Ijumaa.tuliporudi kwake nikaitisha kikao. Nikamsema sana mbele ya mke wake kuwa hafanyi mambo ya maendeleo anaendekeza mademu tu na pombe. Nikamwambia nisimuone tena na wale mademu aliowaleta pale bar

Nikaanza kumsema na shemeji yangu kuwa naye amekuwa hatumii akili. Anawaza kujilemba tu muda wote. Badala wasave pesa wafanye maisha. Wanazaa kma mbwa....watoto watano na bado hawajasettle.

Kesho yake asubuhi jamaa aliomba anirudishe guest. Hatukuwahi wasiliana tena mpaka leo.
 
Yuko jamaa yangu mtu msomi vizuri tu tatizo anatokea kwenye kabila lenye misifa. Siku moja nilimkaribisha kinywaji pale 92 Sinza. Wakongwe mnapakumbuka miaka Ile palikua na gesti pia.
Tulianza vizuri tu Mara akaja mchekopuko wangu na rafiki yake(sasa hv mke wa mtu Tena mheshimiwa) baasi mie nikamchukua mchepuko wangu chobingo na kumpa laki na kumwambia pombe anunue yeye ili kulinda heshma yake kwa rafiki yake. Basi mchepuko wangu akaawaita wa jikoni na kuagiza mchemsho, mbuzi choma na kuku Kisha akalipa kabisa kumuonyesha jamaa yangu kuwa anazo. Kisha mvua ya bia ikaanza. Bwana misifa kila akitaka kuagiza ili kujitutumua mchepuko wangu anakua Kesha agiza bia. Sasa pale tuko wanne Mimi, mchepuko, misifa na rafiki wa mchepuko. Misifa akaona rafiki wa mchepuko Ni halali yake yaani alijimilikisha bila kutongoza kumbe anajipalilia Moto. Baada ya kula nyama nyingi, michemsho na mikuku mchepuko akasema twende kwake tukapate mbili mbili Kisha tuachane kila mtu aende kwake. Misifa hakupenda kuachwa nyuma alihisi labda anaweza kupata chance ya kununua bia ili amu impress rafiki wa mchepuko. Kufika nyumbani kwa mchepuko jirani kabisa na shule ya Mugabe mchepuko akawa amempa signal mama mwenye glossary ya jirani kwamba alete mvua ya bia. Zilipofika kabla misifa hajaingiza mkono mfukoni mchepuko akalipa kabisa. Basi kazi ikawa Ni moja tu. Kugida bia huku kila mtu amekaa sanjari kabisa na mwenza wake, Mimi na mchepuko na misifa na rafiki wa mchepuko, misifa alikua anajua lazima amvue nguo yule rafiki wa mchepuko. Punde si punde misifa akapitiwa na usingizi wa pombe na kulala kidogo kwenye Kochi. Rafiki wa mchepuko alivyoona jamaa amechoka nae huyoo akaondoka kwenda kwake huku misifa anakoroma kwenye Kochi ilhali ana mke aliyemuoa toka Kanda ya ziwa majuzi juzi tu. Mimi na mchepuko tukaingia chumbani na kujipunzisha huku kwenye Kochi misifa anangorota Kama trekta linalopukuchua mahindi. Kufika asubuhi nikamstua misifa aache ujinga, aamke awahi kwa mkewe mbichi mwenye miguu ya bia na lafudhi ya kamachumu.
Misifa kustuka akagundua amelala kwenye Kochi, rafiki wa mchepuko hakumpata na hakulala kwake. Kutoka pale misifa alipotoka kufika barabarani akaona gari ya polisi enzi zile tunayaita tetracycline. Akawaambia wale maaskari wajifanye wamemkamata halafu wampeleke kwake na wampige hata makofi mawili halafu wasachi nyumbani kwake Kama vile amefanya uhalifu fulani. Basi misifa akawakatia pochi polisi na kuwaambia wakifika home atawaongeza mbele ya mkewe. Polisi wetu wape dili la pesa na utajua wamepitia ccp Moshi. Misifa akapigwwa pingu na kupelekwa kwake muda huo yapata saa tatu asubuhi kumbuka enzi zile hakuna simu. Polisi wale kufika nyumbani kwa misifa wakamteremsha kwenye gari na kumwambia akawaonyeshe hiyo Mali ya magendo ilipo, mmoja akamlima Kofi mbili za keleb, misifa akajitetea Hana Mali ya magendo na polisi wakasachi uongo na kweli, Toto la kamachumu lilivyoona mumuwe aka misifa anazidi kudhalilika mbele ya majira akamuita polisi mmoja chocho na kumpa mlungula ili wamwache misifa. Basi pingu zikafunguliwa na misifa akaingia ndani na polisi kuondoka huku wakitabasamu na kijino pembe.
Itaendelea.......
Hadithi hii ishasimuliwa sana. We umeirudia kitoto hata haichekeshi.
 
Back
Top Bottom