Visa gani pombe ilikufanyia hutasahau?

Visa gani pombe ilikufanyia hutasahau?

Kuna jamaa yangu best sana. Alinitangulia kuoa kidogo Ila kazini tulikua pamoja na tulinunua viwanja sehemu moja Tabata na kuanza kujenga polis post wote. Kwa wale dotcom polis post Ni nyumba ya chumba sebule chumba choo na bafu nnje.

Ok. Tuendelee na Hadith. Christmas moja tulienda mkesha Kama kawaida, kutoka kanisani tukahamia bar enzi zile hakuna Makonda Wala Nini, kwenye grosare za mtaani bia mnapiga mpaka majogoo. Basi tukazianza Ile saa tano usiku, hapo ujue wanywaji wote Ni majirani na tunajuana, sasa unakuta mtu una beer tatu hazijafunguliwa, Ni mwendo wa kata mti panda miwili. Baas bwana, ilipofika majogoo mie na jamaa yangu na jirani yangu toka mkoani Geita tukaanza kurudi nyumbani.

Kufika jamaa kaingia kwake kwa mkewe na watoto wawili na mahaus geli wawili. Unajua siku ya Xmas kina mama hasa wanaokaa Tabata hupenda kupikia nje madishi kibao. Pale pilau, huku kitimoto, pale kuku, huku hausgel huyu anakata kachumbari, yule anawasha mkaa mama anasupavais na vijana wake wanacheza na baiskeli.

Kufika muda wa saa tatu watu wote wako nje. Jamaa yangu huyu ambae hajaenda jando mkojo ukambana. Pombe zikamtuma kwamba bado ni kuna giza hivyo anaweza kwenda kukojoa chap akiwa uchi na kurudi kuendelea na usingizi. Jamaa yangu akatoka nje Kama alivyozaliwa na kukojolea ukuta karibu na dirisha lake. Mke na mahausgel na watoto wameshikwa butwaa maana kidogo akojolee ungo uliokua na viungo.

Jamaa akaitingisha Kama kawaida ya wanaume na kuingia ndani kuendelea na usingizi. Jamaa kauchapa Ila kunako saa Saba harufu ya pilau ikamuamsha. Mke akamiwahi na kumwambia kabla hakatoka nje Tena na kumpasha.

ULICHOTENDA LEO HAKINA MFANO. UMERUDI ALFAJIRI UMEONA BADO HAITOSHI, UNAKUJA KUNIDHALILISHA MBELE YA HAUSEGELI NA MAJIRANI KWA KUTOKA NJE UCHI. Jamaa yangu kawa mkali na kusema hajatoka nje uchi. Bi mkubwa kaenda kumuonyesha ukutani jamaa yangu huyu mbabe alipokojolea maana japo mkojo ulishakauka lkn ramani ilikuwapo. Basi jamaa ilibidi awe mpole na kuapa pia alihamia makanisa ya walokole ambayo hayaruhusu pombe.
Daah hii kali wallah!
 
Acha tu. Sijui nani kanihujumu usingizi wangu na kunipa kazi ya ulinzi huku.
Haha umepatikana. Ila ukitaka uenjoy lindo vizuri nenda kule usiku wa manane. Ngoja nikawape hi maana ni muda sijawatembelea wale walinzi
 
Yaani mi binafsi sina wazo kabisa la kuiacha pamoja na yote inayonifanyiaga lakini haijanikomoa.
Ninakumbuka kiroba cha boss tangawizi hangover yake balaa,inafunga hamu ya kula,kunya mpaka kuoga na ukijilazimisha kunywa supu basi mchuzi mnaugawana na meza kwa jinsi mikono inavyotetemeka.
 
Kuna siku nikiwa bachela ndio nimeanza anza kazi Nina pea moja tu ya viatu vizuri vya kuendea mjini na kazini. Sasa Niko Sinza usiku nimeutwika Niko bwii narudi zangu home huku mvua imenyesha mchana na imeshaacha. Kuna ka mbalamwezi kwa mbali. Mbele yangu kukawa na bonge la dimbwi, Basi na zile pombe like dimbwi nikadhani ndio palipo kauka. Nikaliingia jumla na viatu na soksi na suruali.
Kesho yake sikutoka kwenda kazini maana sikua na viatu vingine nikashinda nimeanika viatu. KAbla havijakauka mvua ikashuka Tena. Na siku ya pili Tena sikwenda kazini nikiwa nakausha viatu..
Siku ya tatu nilipofika kazini mkwara niliowekewa ilibidi niache pombe.
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16] noma sanaaa man
 
Ngoja niweke mkasa wangu mwingine ulitokea 2004, Jamaa zangu walitoka mgodini wana hela ya maana wamekuja na mshikaji wao watupambanishe kunywa pombe wanajua mimi kichwa ngumu kwenye bia. Nikawapa masharti kuwa nakunywa bia na si pombe kali. Wakaleta kreti moja ya Tusker na jamaa akapewa yakwake hiyo ni saa mbili asubuhi tumeshakula ugali kwa supu ya samaki. Kufika saa saba nimemaliza kreti jamaa kachemsha. Nikaaga nikaenda kulala, nakuja kushtuka kesho yake mchana majirani wanabomoa mlango wakijua nimekufa. Walichungulia dirishani wanaona mtu kalala chini wakajua nishaenda kwa Sir God. Niliugua siku 3 sijiwezi kabisa.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787] umetishaa
 
Hatar
images-37.jpg
 
Yaani mi binafsi sina wazo kabisa la kuiacha pamoja na yote inayonifanyiaga lakini haijanikomoa.
Ninakumbuka kiroba cha boss tangawizi hangover yake balaa,inafunga hamu ya kula,kunya mpaka kuoga na ukijilazimisha kunywa supu basi mchuzi mnaugawana na meza kwa jinsi mikono inavyotetemeka.
Hii hali umeimiss kutoka kwa Boss?
Sijui ilitokomea wapi ile pombe, nilikuwa nashindwa kumaliza hata kiroba kimoja miaka ile ya 2006/7 kwa ile radha yaani for me it had unpleasant taste.
 
Hii hali umeimiss kutoka kwa Boss?
Sijui ilitokomea wapi ile pombe, nilikuwa nashindwa kumaliza hata kiroba kimoja miaka ile ya 2006/7 kwa ile radha yaani for me it had unpleasant taste.
Nimeimiss sana kiukweli,ila ilikua na madhara sana.
 
Back
Top Bottom