Visa gani pombe ilikufanyia hutasahau?

Visa gani pombe ilikufanyia hutasahau?

Kuna siku nilikuwa napanda daladala naenda nyumbani, mwaka wa nne chuo kikuu. ile kufika kwenye daladala nikakuta kuna wanaume wawili wanapigana, kuangalia ni conductor na abiria. kumwangalia abiria ni mjomba wangu alikuwa na miaka kama 55 hivi, pande la mtu. kumbe mjomba alikuwa amekunywa pombe, zilimzidi na alijisaidia haja kubwa (ninasema hili kwa uchungu kwasababu nilipata aibu mno), suruali kwa nyuma ililowa kabisa naona mapombe yalitoka kama yalivyo, sasa alipokaa kwenye daladala abiria wakaanza kumkimbia, konda kumshusha wakaoshe gari kwa nguvu ndio ngumi zile nilizikuta, yeye anaona anaaibishwa, watu wamekusanyika wanamwangalia. niwe mkweli, nilijifanya simjui (nadhani ni utoto kwasababu nilikuwa mwanafunzi wa chuo bado na sikuwa na pesa ya kumchukulia taxi na kwasababu hakuniona na nilisimama distance, niliondoka eneo lile).

ajabu yake, hakuachaga pombe hadi anakufa pamoja na aibu kubwa namna hii. dereva kaondoa daladala kaenda kuiosha anapiga kelele ati daladala yangu yote inanuka choo. this is a true story.
Duuuh yani mtu anajinyea kabisa tena kwenye daladala hizi stori hua ni kweli lakini!! Napata tabu sana kuamini!!
Yani wanakua wanakunywaje mpaka kujinyea!!!
 
Nikwambie kitu mkuu? Kwanza ujue mwili wenyewe unahitaji blood alcohol kwa kiwango flani ili metabolism and digestion zifanye kazi vizuri. Wenzetu wanaoelewa hata maofisini utakuta wameweka chupa za wiskey na glass na hunywa kabla hawajaingia kwenye mikutano au kabla ya presentations maofisini, kwenye mijadara mbalimbali kwasababu kwa kiwango kidogo huchangamsha mwili na akili.

Sisi tunakamia; kuna pombe za kunywa muda mrefu kama uko idle, kuna pombe ya kunywa kama una muda mchache pia kuna pombe zinatengenezwa na matumizi yake yanategemea na mazingira (hali ya hewa whether ni joto, baridi au moderate)

Unakuta pombe unayopaswa kunywa kipindi cha baridi we unaifakamia kwenye mazingira ya joto, unategemea nini? Lazima itakuperekesha au kukuzimisha tu.
Mkuu hbeu nisaidie hapa Valuer iko kwneye kundi ghani?
 
Mkuu hbeu nisaidie hapa Valuer iko kwneye kundi ghani?
Ni aina ya Brandy mkuu
images.jpeg
 
Hapana, mwaka jana ilifanyika analysis ya pombe kali zote sokoni (Serikali ilihusika). Majibu yaliyotoka kwa hizi pombe zilizojizolea umaarufu kwa sababu ya bei, yanatisha sana. Baadhi zina methano ambayo hatutegemei kabisa iwepo. Pombe mojawapo ilikutwa na methanol content mpaka unaogopa.
Hadi leo nashangaa Serikali imepotezea kuchukua hatua dhidi ya janga kubwa kwa wananchi wake. Pombe hizi za 2,000/= nyingi ni hatari sana kwa afya, madhara yake tutayaona muda si mrefu, ni bomu hatari kwelikweli.
Duuh, sinwyi tena pombe. Ngoja ninywe juisi tuu.
 
Duuh, sinwyi tena pombe. Ngoja ninywe juisi tuu.
Pombe zenye viwango hazina shida kabisa ukizinywa kwa nidhamu. Hizi zinazochipukia kama uyoga huku zikiuzwa bei chee, ni hatari sana kwa figo, maini na hata afya ya ubongo. Hawa washenzi wanaongeza methanol kwa makusudi kabisa kupunguza gharama za uzalishaji ili kupata faida kubwa.
 
Nilikuwa nasafiri toka mwanza kwenda Dar usiku wa kuamkia safari nilipiga cocktail za maana Hadi saa Tisa usiku halafu safari ikaanza 11 alfajir dadadek kufika maeneo ya kibaigwa nilijinyea na kujikojolea nikawa nanuka Ile mbaya Hadi Kuna wakati konda aliitwa kiukweli pombe zilianza kupungua na mzigo ukaanza kushuka kwenye viatu ndipo nilipofikia dumila kwakuwa Giza lilikuwa limeingia nikashikia hapo yaani abiria walinizomea harufu nilikuwa naiacha yaani nikaenda kwenye ule mto wa dumila karibu na feli nikajitupa humo na nikampigia sim msela angu flani akaja na nguo zile nilizokuwa nazo nikajitupa mtoni ila hili tukio hakuna family member anajua
Mi mbona nilikuwa nafahamu ila niliamua kukunyamazia tu.
 
Hapa kama ninakiri!

Kitendo kilichonifanya kuacha kunywa pombe ni tukio la aibu nililolifanya miaka 30 iliyopita, lakini hadi leo bado linanibungua kichwa kwa aibu ile!

Miaka hiyo nilikuwa ninaishi 'kotaz' nyumba zenye kufanana kuanzia sura, rangi na mpaka mazingira ya nje.

Kimbembe kilipoanzia ni pale nilipotoka safari na kukuta 'ugeni' wa rafiki yangu wa siku nyingi kanitembelea hapo nyumbani.

Mahali gani pazuri pa kumpeleka 'outing' huyu ndugu akasuuze roho yake, hakuna pengine ni bar tu!

Sa9 alasiri tayari tupo kwenye meza ndefu tunakunywa, baada kama ya saa1 na nusu nikamuona mgeni wangu 'keshanitaimu' kalewa tayari mimi bado mkavu na bia hazinibambi, nikaona kama ananisanifu, sasa nifanyeje kufukia mashimo?

Wakati natafakari cha kufanya, nikaona mgeni wangu yupo chakari kabisa, nikaitisha tax ikampeleka nyumbani, mi nikabaki bar.

Bia zilivyoendelea kudunda nikaona niagize pombe kali nimix ili kupata ulabu kwa kasi, kumbe ninajitengenezea sumu!

Nikachukua viroba viwili vya 'power' (pombe ilikuwa inaingizwa toka Zambia)nikavimiminia kwenye chupa ya bia na kuanza kuifakamia.

Kumbukumbu zangu ndiyo zilipokomea hapo, yaliyofuata ni simulizi tu nilizokuja kusimuliwa bila mimi kukumbuka hata1.

Inaonekana ilipofika sa1 niliondoka bar kwa miguu kuelekea nyumbani, maana hapakuwa mbali sana.

Nilipofika, kwa kuwa nyumba zinafanana sana, nikakosea nikaingia nyumba kama yangu,lakini line ya mbele kabla sijafika kwangu.

Nilipofika nikaingia ndani na kupitiliza moja kwa moja chumbani kulala, wakati wenye nyumba wapo nje wanaongea!

Walipoingia wakakuta nimelala kitandani kwao na tayari 'shaharibu'.

Wakaenda kwa ghadhabu kumueleza 'wife' aje kunichukua, akakuta siamshiki wala sibebeki.

Njia iliyotumika kunitoa pale na kunipeleka kwangu pamoja na aibu yote niliyoifanya ndani ya nyumba hiyo na kwa familia hiyo, niliporudiwa fahamu na kusimuliwa, nilitamani dunia ipasuke inimeze!

Kwa unyenyekevu mkubwa, nikaiomba radhi familia hiyo na tangia hapo nikaacha pombe moja kwa moja na sitarudia kunywa mpaka takapokufa.
.


Sent using Jamii Forums mobile app
Nimecheka sana kwa kweli
 
Kipindi Niko chuo kikuu Cha Dar es Salaam miaka Ile. Tulikua tunakwenda kunywa wanzuki au mbege maeneo ya Riverside. Siku hiyo tulipata boom vzr Basi tukaona tukapate mbili tatu. Tukafika pale zilipo hostel za mabibo enzi hizo hazijajengwa kulikua na vibanda vya pombe za ovyo.

Tukaanza kugida wanzuki. Wenzangu wakachoka wakaniacha na li barmeid Fulani umri umesogea. Kufika saa nne hivi nikaanza kuliona Ni beautiful Fulani. Basi nikalikokota Hadi hall one tower block kwa wale mliopitia shule za ukweli. Tukapanda mpaka kwa room na kufanya majambooz.

Asubuhi naamka kwenda kukojoa nikaona ndala za yule mmama zilikua zimetoboka pale anapokanyagia na zimekarabatiwa na waya. Kumcheki kichwani ametia Ile kalkit ya muonekano Kama nywele zimetiwa maji au mafuta mengi. Kumbuka wanafunzi wameshaanza kukaa pale chini karibu na ofisi ya hall manager, wengine wanapiga stori wakitokea kafeteria kupata chai.

Mimi Niko juu gorofani na msukule wangu unao dai lazima nimpeleke kituo Cha Basi. Madem wa chuo nao wapo pale stendi wanasubiri daladala. Mimi bado Nina msukule wangu anadai anataka kuwahi kutengeneza pombe mabibo. Aloo.

Nilimlaumu shetani na kazi zake zote. Nitampitishaje yule msukule mbele ya ma brazamen?
Umesababisha nimecheka sana.
 
Kabisa!

Huwa namuonea wivu sana Abraham, yan alipata nafasi ya kipekee kwa Mwenyezi Mungu lkn alishindwa kuitumia[emoji848][emoji848][emoji849]

Mwenyezi Mungu alikuwa anampenda balaa, ila yy uwoga ulizidi ningekuwa mimi ningeitumia hiyo fursa balaa[emoji16][emoji16][emoji16][emoji28]
Ungefanyaje?
 
Binafsi nakunywa pombe mara mojamoja, naweza kupitisha mwezi sijanywa ila nikinywa huwa nalipiza siku ambazo sikunywa kabisa. Hii imenikuta wiki chache zilizopita tulikuwa na event na marafiki tunaotoka sehemu moja, kwenye pombe mbuzi anahusika nilisimamia kitengo.

Nilikunywa mpaka K Vant nikaiona kama soda, nakuja kustuka pombe imenizidi kiasi hata kutembea ilikuwa noma. Sifanyi fujo nikilewa kila mtu alifurahi lakini balaa lipo kwa ndugu zangu kujua kuwa ninakunywa. Busara ilitumika simu yangu nikaicha kwa mtu niipate nikiwa fresh.

Ase nilifanya safari ya saa 1 na nusu peke yangu nikiwa nimelewa na sijui nilifikaje nyumbani, kuja kustuka ni asubuhi niko kitandani tatizo limebaki kwa ndugu zangu. Wakati nimeacha simu kwa rafiki nilipigiwa jamaa akapokea na kuwaambia niko kwenye matatizo ile kitu ilizua taharuki watu hawajalala kuulizia hali yangu maana mimi sikupatikana tena.

Hii kitu imeniweka sehemu mbaya sana hakuna mtu anataka kunielewa tena. Ukweli nimekwama nimeamua kuacha pombe maana naona itanigombanisha na ndugu.
umesema unaishi wapi vile?
Isije ikawa ni wewe ambaye nilishuhudia umelala mtaroni vijana wakakuburuta mpaka chimbo wakapanga foleni😋
 
Siku ambayo siwezi isahau ni siku nimekunywa pombe kisha nikaenda zangu home Ile nimeingia kulala mkojo ukanibana ikabidi nitoke chumbani nikakojoe baada ya kuenda chooni nikaenda jikoni kukojoa alafu nikaludi zangu kulala kesho yake asubuh ebanaeeeeee Sito sahau
Hatari sana
 
Kuna kisa niliwahi kukiweka huku sikumbuki vizuri ile Uzi title yake ilikuwa inasemaje ila ilikuwa hivi:

Nilipata mshkaji mmoja kutoka Netherland akiwa anafanya research katika mambo ya kilimo nikawa nampa escort hadi akakamilisha tulikuwa moshi, baadae akataka kutembea mkoa mwingine nikamwambia mwanza pamekaa poa akataka nimpe kampani kwa kuwa nlikua likizo nikaona poa.

Basi safari ikawadia tukafika sasa kisa kilianza kesho yake baada ya kwenda bar moja ufukweni ziwa Victoria kama kawaida nikaagiza konyagi nikiwa na yule mzungu kidogo jamaa akaingia ziwani akanza kukata mawimbi hapo nakunywa kikonyagi nikaona huyu mgeni hawezi kushinda mwenyeji nikasaula nguo nikabaki na uboxa nikazama kwenye maji aisee ile naibuka wimbi likanichkua waaba! Eh nakanyaga chini miguu haifiki nikaanza kuita mzungu hello.

Nakunywa nguchu ....... Nikiibuka tena nguchu ,nikatamani Iwe ni ndoto kumbe in live likaja wimbi likanirudisha nilipotoka aisee nilitoka spidi break ya kwanza ni kaunta huku natetemeka ile mbaya na konyagi imeisha kichwani kwasababu ya lile wenge lililosababishwa na kiherehere chakushindana na mzungu bila kujuwa maji niliyokuwa naogelea mto karanga pale moshi ni tofauti kabisa na haya ya ziwa ,nikagundua maji sio kitu nzuri hata nikiingia bafuni maji ya ndooo sitaki nitumie muda mrefu dakika sifuri nimeshachomoka huko spidi ile kitu haipotei kwenye ubongo na maji nayaheshimu hadi Leo.
Dah nimecheka.
 
Back
Top Bottom