Visa gani pombe ilikufanyia hutasahau?

Visa gani pombe ilikufanyia hutasahau?

Visa vyangu ni lukuki, miaka ya 2000 nilisafiri toka mkoa niliokuwepo nikaenda Mkoa wa mara (Musoma mjini). Rafiki yangu wa karibu sana alikuwa anafunga ndoa, sherehe ikafanyika pale Musoma hotel.

Nilikunywa pombe nazinduka nimelala ufukweni mwa ziwa victoria tena asubuhi kabisa vitu vyangu vyote ninavyo. Usiku baada ya sherehe wamenitafuta wakashindwa kujua nilikokwenda.

Nikarudi nilikofikia bila kuwasimulia kilichonikuta
 
Visa vyangu ni lukuki, miaka ya 2000 nilisafiri toka mkoa niliokuwepo nikaenda Mkoa wa mara (Musoma mjini). Rafiki yangu wa karibu sana alikuwa anafunga ndoa, sherehe ikafanyika pale Musoma hotel. Nilikunywa pombe nazinduka nimelala ufukweni mwa ziwa victoria tena asubuhi kabisa vitu vyangu vyote ninavyo. Usiku baada ya sherehe wamenitafuta wakashindwa kujua nilikokwenda. Nikarudi nilikofikia bila kuwasimulia kilichonikuta
mzee kuwa makini usije ukawa umerogwa[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] huu uzi mikasa yako wewe ndo kiboko
 
Kama umewahi kunywa pombe ikakusababishia kufanya kitu chochote kesho yake ukajikuta umedhalilika au kujutia achana nayo fanya mambo mengine
 
Kama umewahi kunywa pombe ikakusababishia kufanya kitu chochote kesho yake ukajikuta umedhalilika au kujutia achana nayo fanya mambo mengine
Mimi binafsi napenda niiache jumla, ishaniletea mikasa lukuki mingine ni aibu kwa umri wangu, naweza kaa kwa muda nasahau narudi tena.

Kwa mtu ambaye hajawahi kuwa addicted ni ngumu sana kujua magumu niliyopitia na hatua ngapi imenirudisha nyuma. Niliwahi kuicha nikawa napata mauzauza (hallucinations) kwa siku kama 3 yaani naona watu wakiongea na kunisumbua nikufumbua macho siwaoni nabaki kusikia sauti za watu tu, naona vitu vya ajabu usiku silali wala mchana.

Namwambia wife umewaona watu au umesikia sauti anasema we lala hakuna chochote, wacha niishie hapa
 
Mimi binafsi napenda niiache jumla, ishaniletea mikasa lukuki mingine ni aibu kwa umri wangu, naweza kaa kwa muda nasahau narudi tena. Kwa mtu ambaye hajawahi kuwa addicted ni ngumu sana kujua magumu niliyopitia na hatua ngapi imenirudisha nyuma. Niliwahi kuicha nikawa napata mauzauza (hallucinations) kwa siku kama 3 yaani naona watu wakiongea na kunisumbua nikufumbua macho siwaoni nabaki kusikia sauti za watu tu, naona vitu vya ajabu usiku silali wala mchana. Namwambia wife umewaona watu au umesikia sauti anasema we lala hakuna chochote, wacha niishie hapa
Nadhani sababu huwa unaacha gafla. Labda ungekua unaenda unajipunguzia dozi mpaka unaacha kabisa. Na vizuri zaidi uwe unanywea home badala ya kwenda bar
 
Kipindi Niko chuo kikuu Cha Dar es Salaam miaka Ile. Tulikua tunakwenda kunywa wanzuki au mbege maeneo ya Riverside. Siku hiyo tulipata boom vzr Basi tukaona tukapate mbili tatu. Tukafika pale zilipo hostel za mabibo enzi hizo hazijajengwa kulikua na vibanda vya pombe za ovyo. Tukaanza kugida wanzuki. Wenzangu wakachoka wakaniacha na li barmeid Fulani umri umesogea. Kufika saa nne hivi nikaanza kuliona Ni beautiful Fulani. Basi nikalikokota Hadi hall one tower block kwa wale mliopitia shule za ukweli. Tukapanda mpaka kwa room na kufanya majambooz. Asubuhi naamka kwenda kukojoa nikaona ndala za yule mmama zilikua zimetoboka pale anapokanyagia na zimekarabatiwa na waya. Kumcheki kichwani ametia Ile kalkit ya muonekano Kama nywele zimetiwa maji au mafuta mengi. Kumbuka wanafunzi wameshaanza kukaa pale chini karibu na ofisi ya hall manager, wengine wanapiga stori wakitokea kafeteria kupata chai. Mimi Niko juu gorofani na msukule wangu unao dai lazima nimpeleke kituo Cha Basi. Madem wa chuo nao wapo pale stendi wanasubiri daladala. Mimi bado Nina msukule wangu anadai anataka kuwahi kutengeneza pombe mabibo. Aloo.
Nilimlaumu shetani na kazi zake zote. Nitampitishaje yule msukule mbele ya ma brazamen?
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji1][emoji1][emoji1]
 
Nadhani sababu huwa unaacha gafla. Labda ungekua unaenda unajipunguzia dozi mpaka unaacha kabisa. Na vizuri zaidi uwe unanywea home badala ya kwenda bar
Hata Daktari aliniambia hhivyo hivyo na ilinisaidia kwa kupunguza dozi kidogokidogo hallucinations haikunisumbua mara ya pili
 
Inaonekana ilipofika sa1 niliondoka bar kwa miguu kuelekea nyumbani, maana hapakuwa mbali sana.

Nilipofika, kwa kuwa nyumba zinafanana sana, nikakosea nikaingia nyumba kama yangu,lakini line ya mbele kabla sijafika kwangu.

Nilipofika nikaingia ndani na kupitiliza moja kwa moja chumbani kulala, wakati wenye nyumba wapo nje wanaongea!

Walipoingia wakakuta nimelala kitandani kwao na tayari 'shaharibu'.

Wakaenda kwa ghadhabu kumueleza 'wife' aje kunichukua, akakuta siamshiki wala sibebeki.

Njia iliyotumika kunitoa pale na kunipeleka kwangu pamoja na aibu yote niliyoifanya ndani ya nyumba hiyo na kwa familia hiyo, niliporudiwa fahamu na kusimuliwa, nilitamani dunia ipasuke inimeze!

Kwa unyenyekevu mkubwa, nikaiomba radhi familia hiyo na tangia hapo nikaacha pombe moja kwa moja mpaka takapokufa.
.


Sent using Jamii Forums mobile app
kuanzia hapo inapoonekana nimefurahi sana ama hakika ulikua hujitambui.
 
Kabisa mkuu! Darasa la saba hapo natoa pesa mfukoni nanunua vipombe vinaitwa power, ila pombe niliipenda tangia niko darasa la tano baada ya kuonja bia ya mzee
[emoji849][emoji1][emoji1][emoji1][emoji16]cha p uliyekubuhu
 
Iko hivi mkuu. Kitu chochote ambacho kimechachushwa ( fermented )kinakuwa na kiwango kikubwa cha acetic acids. Ini hubadirisha hizi chemical compound kuwa fatty acid, carbon dioxide na maji. Sasa ukiendelea kunywa kiwango ambacho ini litashindwa kuchakata hupelekea kiwango cha pombe kwenye damu kuongezeka. Pombe inapokuwa nyingi kwenye damu heart beats kuongezeka ili kuruhusu kiwango kingi cha oxygen kwenda kwenye moyo ili ijichanganye na damu yenye pombe kwa matumizi ya cells mwilini.

Hapa utumaji wa taarifa ( impulses) kwenda na kurudi kwenye ubongo hufanyika kwa speed kubwa kadri blood circulation inavyoongezeka kwa unywaji wako wa pombe. Taarifa ni hizo unazosikia hapo ulipo (stories zinazoendelea mahala unapokunywa) na taarifa nyingine ni hizo ambazo zipo kwenye store ya ubongo wako. Sasa mchakato wa kuzichakata ndipo hupelekea mwingine KUONGEA SANA[emoji3][emoji3]. Hapa ndipo huwa chanzo cha matusi, dharau na hali ya kutaka kusikilizwa wewe tu (conversational domination).

Process ya unywaji inapoendelea hufikia hatua kiwango cha blood alcohol huwa kikubwa sana nakupelekea utumaji na urudishaji wa taarifa kutoka kwenye ubongo kuzorota, hatua hii mtu huanza kuloose control na matokeo yake mdomo kuwa mzito, macho hulegea( Viungo vya mwili kuwa vizito). Kadri pombe inavyoongezeka kwenye damu Ubongo huamua kufanya maamuzi ya kuvizima sense organs (viungo pokea taarifa) ili ushugurike na kubalance kiwango cha pombe kwenye mwili.

Ubongo huamuru nephrones kwenye figo kuongeza kasi ya uchujaji bila kunyonya. Hapa kimkja hutokea kati ya vitu viwili ambavyo ni
1. Kama kiwango ni cha juu lakini ubongo unaweza tengeneza mazingira ukashtuka na kuhisi umebanwa na mkojo ukakojoa kwa hiari yako.

2. Kama kiwango ni cha juu ubongo huruhusu mkojo kutiririka toka kwenye figo, kjja kwenye bladder (kifuko) na kutoka nje moja kwa moja bila wewe kuwa na taarifa. Hatua hizi mbili zote tunasema mtu amezima[emoji23][emoji23][emoji23]

Nadhani nimejaribu kukujibu kadri ulivyotaka mkuu.
Mkuu heko kwako[emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122]

Makofi jamani eeh, umedadavua kiutamu mpaka nimerudia mara mbili mbili kusoma

Ila kama mambo yenyewe ni hayo, sitaki na wala sitamani ulabu tena

Kwaheri gambe[emoji119][emoji119][emoji2772]
 
Ndio maana kuna dogo mmoja dingi ake alikua ni mgonga nyagi hatari,siku hio dogo na mama ake wanapita mitaa ya pale Distilleries Chang'ombe dogo anamwambia maza ake nasikia harufu ya perfume ya baba.
Weeeeee[emoji16][emoji16][emoji1][emoji1]
 
Nikwambie kitu mkuu? Kwanza ujue mwili wenyewe unahitaji blood alcohol kwa kiwango flani ili metabolism and digestion zifanye kazi vizuri. Wenzetu wanaoelewa hata maofisini utakuta wameweka chupa za wiskey na glass na hunywa kabla hawajaingia kwenye mikutano au kabla ya presentations maofisini, kwenye mijadara mbalimbali kwasababu kwa kiwango kidogo huchangamsha mwili na akili.
Sisi tunakamia; kuna pombe za kunywa muda mrefu kama uko idle, kuna pombe ya kunywa kama una muda mchache pia kuna pombe zinatengenezwa na matumizi yake yanategemea na mazingira (hali ya hewa whether ni joto, baridi au moderate)
Unakuta pombe unayopaswa kunywa kipindi cha baridi we unaifakamia kwenye mazingira ya joto, unategemea nini? Lazima itakuperekesha au kukuzimisha tu.
Toa huo utofauti mkuu? Za iddle Ni zipi, za weather Ni zipi?
 
Kisa kikubwa cha pombe katika ujana huu ni kulewa alafu baada ya kufika home wakati nasubiria kufunguliwa geti niingize gari nikazima hapohapo. Chakushangaza toka kote huko nilipokuwa nimekuja vizuri tu mpaka getini, akili ikinituma nishapiga honi nasubiri kufunguliwa kumbe sikupiga. Nilikuja kushtuliwa saa kumi na moja asubuhi na mpangaji mwenzangu baada ya kuamka na kuona mwanga wa taa za gari zikipiga getini gari ikiwa inaunguruma mdogomdogo. Niliona aibu kwa mdada yule na tulivyokuwa tunaheshimiana haha. This issue opened a new page of us maana alianzishaga utani ambao baadae ulikiwa wa manufaa[emoji12][emoji12][emoji12]
Wacha wee pombe ikakupa na K kimasihara[emoji16][emoji16][emoji16][emoji1]
 
Hahaa pombe ikishakolea na pesa ipo huwa mtu hautaki kurudi home hata siku moja, najikutaga natumia laki mbili one night, roho inauma now naenda slow motion sanaa pole mkuu utasahau tu,

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna siku nilienda na 30k viwanja, ( yaan kula na kunywa chupa ya wine moja)

Baada ya ile wine kuisha, nilisaka ATM mpaka nikaipata nikachomoa laki, nikawanunulia mashost wine na Mimi mwenyewe

Asee kesho yake nilijuuuta balaa[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji1]
 
Kuna siku nilienda na 30k viwanja, ( yaan kula na kunywa chupa ya wine moja)

Baada ya ile wine kuisha, nilisaka ATM mpaka nikaipata nikachomoa laki, nikawanunulia mashost wine na Mimi mwenyewe

Asee kesho yake nilijuuuta balaa[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji1]
Kama unataka kujibana piga hesabu kabla hujafika mfano ukiona bia 4 efu 10 beba efu 10 tu kavu na kadi acha kitaaa mana ukienda na hela ukishaanza kuchangamka lazma utaanza kuzungusha mpe yule mruke chaap laki imekata

Sent from my TA-1004 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom