Kidogo tufanane mkuu pombe zilinitesa Sana,Kuna kipindi nilipiga valeur kubwa moja na vant ndogo na virikuu viwili!
Halafu asubuhi Nina kazi ya kupokea watalii nilijikuta asubuhi nimelala chini kwenye tiles milango ipo wazi,redio full mziki,taa zinawaka,Sina hata Mia mfukoni na simu
Uzuri geto hapakuibiwa chochote manake ninafuga mbwa wakali
Sijadhurika popote,sikumbuki nilifikaje Niko hangover hatari,tumbo linakwangua balaa,siwezi hata kushika glass ya maji
Nilivyokuwa fala nikajikokota mpaka dukani kwa mangi anipe kvant nizimue niende job!
Hapo ndio niliharibu!!
Nilivyozimua ile vant nilidata mazima 🤣
Kilichoniokoa mule ndani ni juice za machungwa na tangawizi
Nililala geto sio chini ya siku 3 nikaapa sinywi tena
Ila haikupita mwezi nikalisapraiz ini tena