Vipigo vya Machinga Mwanza ni kama kwa Makaburu

Vipigo vya Machinga Mwanza ni kama kwa Makaburu

Eti CDF Wangekuja Lugalo Kukuimbia Kwaya Ungekubali, Jibu Hapana Mh Rais Na Salute Ikapigwa CDF Akakaa Chini.


Rais Akatamka Heshma Hii Hii Aliyosema CDF Ishuke Kwenye Vyombo Vyote Vya Dola Kuanzia Sasa. Msijifanye Hamvijui Vyombo Hivyo Ikumbukwe Ni Vingi Sana Ila Vinavyojulikana Ni Vichache Sana


Police Sasa Ni Kwenye Ubora MkubwA Yaani Yale Marungu Yanatoka Nchi/Pori Gani ?
 
Ukiwa unatoa tamko ... uwe na uhakika na unajua unachikitamkia ... Raisi mwenyewe kwa mdomo wake alitamka August 2016 huko Mwanza kwamba wasiondoke mjini na wala wasisumbuliwe na atakae wasumbua atadeal nao ...
Kama alisema ata deal nao anasubiri nn ss !?
 
Nawapongeza sana polisi... Piga malofa hao..hahahah namba lazima isimeke mpaka tuishi kama mashe.... Malizia
 
Unawazungumzia hao machinga
wasio bebeka kama klabu ya yanga!!
mtu anakubeba jitulize na utumie nafasi hiyo vizuri
wao wanavuka mipaka
ulitegemea nini!!

wamefikia hatua yakupanga vitu kwenye vituo vya mabasi ya mwendokasi!!

Boda boda mmeambiwa msipakie mshikaki
na mvae kefia
Watu wana kaidi wewe unakuja na ngonjera zako polisi wafanyeje!?

Tena bado naona polisi wana udhaifu mkubwa
waongeze nguvu
Kumbe Mwanza kuna njia za mwendokasi?
 
Alafu huyo jamaa alikuwa ametoka nje ya mji ajui ili wa lile ameshuka kwenye gari gafla anakutana na vichapo
 
Inachukiza na kusikitisha kuona wanamgambo wanampiga mtu teke la kichwa wakati ameishapiga magopi. Ningeelewa kidogo kama yule kijana angekuwa anakaidi amri.

Hawa wana mgambo hawana hata chembe ya ubinadamu achilia mbali maadili ya kazi.

Wao na Viongozi wao wamekalia kuti kavu.
Wanamgambo ni askari, na kwa kawaida askari hutii amri! walio juu wanapokuwa wababe hata pasipohitajika ubabe, kwanini wanamgambo nao wasiwe wababe hivyo hivyo ili kuendana na falsafa ya walioko juu? Kilichofanyika Mwanza hakina tofauti na kile kinachofanywa na polisi-kung'oa matairi ya magari! Kwanini tuone wanamgambo hao wanakosa ubinadamu lakini wale wanaofanya wanamgambo hao wawe kama walivyo wao tuwaone kuwa wana ubinadamu? Awamu hii ni ya "wapigwe tu"!
 
kwa kipigo hicho kwa mtu anaejitaftia riziki ya watoto wake nyumban tena kwa kuungua na jua siku nzima inatoa machozi kabisa aiseee. naijutia sana kura yangu 2015
 
Wananchi wa Mwanza hawapaswi kumlaumu yeyote. Ubwege wao wa kujifanya kuichagua ccm ndio utawagharimu miaka yote. Wacha wapigwe na ikifika 2020 watapewa pipi na jojo watasahau maumivu yao na watalichagua tena hilo zimwi lao. Kama binadamu nimehurumia sana huyo jamaa aliyekalishwa chini na kurukiwa teke usoni, hawa wapigaji nao watumie akili siyo kufata maagizo kama mbwa.
 
Halafu imeonyeshwa live na wananchi wanaona
Hii sidhan kama ni picha nzuri na outcome yake utaisikia tu very soon
 
Siasa za bongo bwana! Kwa sababu tu chama cha hakikuchaguliwa kushika dola basi raia wakiumia wala hujali. Una uhakika wote walioumia hakuna hata mmoja wa chama chako? Tutumie busara japo kidogo!
Mkuu kwani chama changu ni kipi?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom