Vipigo vya Machinga Mwanza ni kama kwa Makaburu

Vipigo vya Machinga Mwanza ni kama kwa Makaburu

Kama wana jipanga barabarani wapigwe tuu Rais hakuwambia wakae barabarani.
Ukiwa unatoa tamko ... uwe na uhakika na unajua unachikitamkia ... Raisi mwenyewe kwa mdomo wake alitamka August 2016 huko Mwanza kwamba wasiondoke mjini na wala wasisumbuliwe na atakae wasumbua atadeal nao ...
 
Unawazungumzia hao machinga
wasio bebeka kama klabu ya yanga!!
mtu anakubeba jitulize na utumie nafasi hiyo vizuri
wao wanavuka mipaka
ulitegemea nini!!

wamefikia hatua yakupanga vitu kwenye vituo vya mabasi ya mwendokasi!!

Boda boda mmeambiwa msipakie mshikaki
na mvae kefia
Watu wana kaidi wewe unakuja na ngonjera zako polisi wafanyeje!?

Tena bado naona polisi wana udhaifu mkubwa
waongeze nguvu
 
Kwa hiyo ni ruksa kwa askari kulipa kisasi? Yule kijana anaonekana amepiga magoti kutii amri kwani apigwe namna ile?
Askari anayetumia weledi hawezi kulipa kisasi kwa mtu mwingine eti kwa vile kuna mtu kampiga mwenzie. Wale askari waliuwawa Mbagala ingekuwa hivyo si nao wangesimama barabarani na kuua raia kwani wenzao wameuwawa?
Ulinganisho wako hauko sawa mkuu
Suala la machinga ni suala la utalaamu, watu wa mipango miji ndo walitakiwa walishughulikie,lakini inavyoonekana limekuwa ni la kisiasa. Ni kweli kabisa,watanzania wanatakiwa wawe huru kwenye nchi yao,na wafanye biashara zao bila kubughuziwa lakini ni lazima kuwe na utaratibu.
operation machinga iliyoendeshwa mara ya kwanza ilifanikiwa ingawa ilisumbua machinga wenyewe.
Kuwarudisha tena,kiukweli hili tulilitarajia maana isingewezekana kuendelea na hali ilivyokuwa,machinga walijaa kila sehemu hata zile road reserves walipanga mali zao.
Tulilitarajia hili kwa maana machinga walikuwa na nguvu toka mamlaka ya juu kuwa ruhusa yao imetoka kwa mwenye nchi. Wenye wilaya na mikoa yao nao wanataka miji yao ipangike...hapa ndo ugomvi unaanzia.
Tumepiga kelele siku nyingi kuwa,watu wa mipango miji waachiwe waumize vichwa vyao,waje na jibu na si hizi zima moto za wanasiasa.
Machinga wataendelea kupigwa,askari kazi yake ni kutii amri. Akiambiwa piga na atapiga tu! Kwa mliopitia JKT mtanielewa,tunaweza kuwalaumu hawa watu lakini yeyote atakaefanya kazi hiyo atakuwa hivyo hivyo.
Tutafute suluhu ya machinga na tuondoe siasa katika hili.
 
NINAANDIKA HAYA KWA HERUFI KUBWA ILI KAMA HAO VIONGOZ HUWA WANAPITA JF WAFAHAMU UHALISIA,


MAJESHI YOTE YA TANZANIA HUTUMIA NGUVU KUBWA SANA KATIKA KUTULIZA GHASIA,UONEVU NA KUTOZINGATIA HAKI ZA BINADAM NDIYO WANAYOYAFANYA.HAKIKA MUNGU ANAWAONA,SIKU KIKIANZISHAPWA KIKUNDI KAMA ALSHABAB YA TANZANIA NITAKUWA WAKWNZA KUJIUNGA ILI KULIPA KISASI KWA SERIKARI,NIMESHASHUHUDIA UONEVU MWINGI SANA UNAOFANYA NA VYOMBO HIVI VYA USALAMA,NADHANI IPO SIKU FAMILIA ZENU ZITAKUWA NA VILIO.SHAME ON YOU....
Na wapigwe tu! Naelewa wasukuma wanadharau sana na lilipokuja swala la rais kuwa msukuma yaani ndo wamezidi wakijua rais ni wa kabila letu hawajui kuwa rais ni taasisi tu lakini serikali ipo wao wanajua ni magufuri tu, hatuwezi nchi ikaendeshwa kwa imani hizo wafanye wanavyotaka kwa kigezo cha rais ni msukuma mwenzetu pamoja na kulijua hilo na kuaminishwa hivyo na viongozi waandamizi lakini hawa ndugu zangu hawajui kiongozi mwingine ila ni magufuri tu, hatuwezi kukubali kuruhusu uzalishaji mkubwa wa uchafu tukauachia hivi hivi kwa imani rais ni wa nyumbani na pindi mlipuko wa maradhi ukitokea lawama kwa waziri wa afya! Lawama hizo hazikubaliki kwa ajili ya ubishi wa baadhi ya watu, nasema hivi afya ni jambo la msingi kabisa katika jamii wakiendelea kutotii mamlaka za miji na wapigwe tu!
WEWE ACHA UNAFIKI NA UCHOCHEZI WA KIKABILA,KWANI UNAJUA MAGUFUR ALIPITISHWA NA MAKABILA MANGAPI NA MIKOA MINGAPI,SHENZHEN TYPE KABISA,KUNA WACHAGA WALIOMPIGIA KURA NA KUNA KABILA NYINGI TU MBONA HUZIZUNGUMZII?alipokuwa RAIS KIKWETE MLISEMA HIVYO HIVYO KWAMBA KABILA LAO NI WATU WA SIFA,MAJIVUNO SANA,SASA MAGUFUR NDO MMEHAMIA KWAKE,,,


KABILA LA MTU SI KIGEZO CHA UTAWALA MBAYA BALI TABIA YA MTU NA AKILI YAKE,KUNA WANGAPI WASUKUMA NA WANAHEKIMA ZAIDI MAOFISINI?usitake kuDANGANYA UMMA WA WATANZNIA,WEWE MWENYEWE ULIMPA KURA LEO HII UNAANZA KUROPOKA UJINGA,SHAME ON YOU,,,,,,,,,
 
Piga tu na Mimi nasema wapigwe Mzee pinda muda wake umeisha saivi mkulima Wa dhabibu Dodoma huko.....
 
Wahangaike juani ili wewe ule kivulini...loo, ziko akili sitamani nizielewe.
Mkuu Mag3, hiyo ndio akili ya Watanzania wengi. Mtu anasema siasa mimi sitaki lakini anatamani mambo yabadilike. Hali hii ipo kwenye jumuiya zote hapa nchini,vyama vya siasa,vyama vya wafanyakazi ni mifano mizuri sana. Sasa ngoja utukute tukiimba "Solidarity Forever",utadhani kweli tunamaanisha,kumbe ni unafiki wa kiwango cha lami. Hii nchi ni yetu sote,tushirikiane wote ili tuijenge wote kwani hakuna mtu au kikundi cha watu wanaostahili wao tu kuijenga.
 
Mkuu wa kaya anatafuta kiki nyingine.Anawaacha wapigwe halafu yy anakuja kizombie zombie anatengua maamuzi ya wakuu wa mikoa then anashangiliwa.Ni upuuzi kiongozi kutaka kila siku uonekane kwenye media.
 
Mkuu wa kaya hapo atakua kafurahi bora wakoloni weupe kuliko weusi
 
Ngoja wapigwe watanzania tumezidi kwa upole ambao hauna maana unaonewa unashidwa kujibu kwa kisingizio cha Amani Tanzania ndo nchi pekee ambayo mtu anomba haki yake haki yako aitakiwi kuobwa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom