Viongozi wa Dini na Hatma ya Tanzania

Viongozi wa Dini na Hatma ya Tanzania

Hawa Maaskofu wao ni kila kitu at once, ni wanasiasa, wachumi, wahubiri, etc.

Nafikiri imefika wakati wakaongee na wale watu wa mafuta pia duniani...

Oil passes record $100 a barrel

NEW YORK (AP) -- Oil prices soared to $100 a barrel Wednesday for the first time ever, reaching that milestone amid an unshakeable view that global demand for oil and petroleum products will continue to outstrip supplies.

Oil finally passed $100 per barrel on Wednesday after violence in Nigeria triggered investor fears.

Surging economies in China and India fed by oil and gasoline have sent prices soaring over the past year, while tensions in oil producing nations like Nigeria and Iran have increasingly made investors nervous and invited speculators to drive prices even higher.

Violence in Nigeria helped give crude the final push over $100. Bands of armed men invaded Port Harcourt, the center of Nigeria's oil industry Tuesday, attacking two police stations and raiding the lobby of a major hotel.

Word that several Mexican oil export ports were closed due to rough weather added to the gains, as did a report that OPEC may not be able to meet its share of global oil demand by 2024.

Light, sweet crude for January delivery rose $4.02 to $100 a barrel on the New York Mercantile Exchange, according to Brenda Guzman, a Nymex spokeswoman, before slipping back to $99.48.

Crude prices, which have flirted with $100 for months, have risen in recent days on supply concerns exacerbated by Turkish attacks on Kurdish rebels in northern Iraq and falling domestic inventories.

However, post-holiday trading volumes were about 50 percent of normal Wednesday, meaning the price move was likely exaggerated by speculative buying.
"I would imagine the speculators are the biggest drivers today," said Phil Flynn, an analyst at Alaron Trading Corp., in Chicago.

It's hard to say whether prices would have risen as quickly on a normal trading day, Flynn said. While crude prices have soared on mounting supply concerns in recent months, speculators have often been cited as a reason for the swiftness of oil's climb.
Moreover, many of the concerns about supply disruptions have yet to materialize, but that hasn't stopped buyers from driving prices higher.

"Although the (Nigerian) violence has not impacted oil flow out of the country, it has reignited supply concerns as militant attacks have reduced Nigeria's crude output by roughly 20 percent since 2006," said John Gerdes, an analyst at SunTrust Robinson Humphrey in a research note. Nigeria is Africa's largest oil producer.

Separately, the Organization of Petroleum Exporting Countries said its member nations may not be able to meet demand as early as 2024, though OPEC also said that deadline could slide for decades if members increase production more quickly. Word that several Mexican oil export ports were closed due to rough weather added to the gains.

On top of those concerns, investors are anticipating that crude inventories fell by 1.8 million barrels last week, which would be the 7th weekly decline in a row.
"(A decline) is not anything unusual for this time of year, but when it happens for 7 weeks in a row, it starts to add up," said Amanda Kurzendoerfer, an analyst at Summit Energy Services Inc. in Louisville, Ky.

Oil prices are within the range of inflation-adjusted highs set in early 1980. Depending on how the adjustment is calculated, $38 a barrel then would be worth $96 to $103 or more today.

At the pump, meanwhile, gas prices rose 0.6 cent Wednesday to a national average of $3.049 a gallon, according to AAA and the Oil Price Information Service. Gas prices, which typically lag the futures market, have edged higher in recent days, following oil's approach to $100.

Gas prices peaked at $3.227 a gallon in May as refiners faced unprecedented maintenance issues and struggled to produce enough gasoline to meet demand. A similar scenario is expected this spring, when gas prices could peak above $3.40 a gallon, according to the Energy Department's Energy Information Administration.

The EIA's inventory report, delayed until Thursday this week due to the New Year's holiday, is also expected to show gains in gasoline supplies and refinery activity, and a decline in supplies of distillates, which include heating oil and diesel.

In other Nymex trading Wednesday, February heating oil futures rose 9.06 cents to $2.74 a gallon while February gasoline futures climbed 7.92 cents to $2.57 a gallon. February natural gas futures advanced 26.7 cents to $7.75 per 1,000 cubic feet.

In London, February Brent crude rose $3.11 to $97.58 a barrel on the ICE Futures exchange.


Copyright 2008 The Associated Press.
 
Mimi naungana nao katika kufikisha ujumbe kwa jamii.
Nchi haina dini lakini raia wake wana dini, naamini kama watakazana kuwahubiria wananchi ili wafunguke waone mbele katika kutetea maslahi yao, ni jambo zuri sana.

Kwa kila njia ni lazima rasilimali za Tanzania zitetewe.
 
MAASKOFU wamewataka viongozi wa serikali kuchukua hatua za haraka kunusuru hali ya kiuchumi mwaka huu wa 2008 ili kudhibiti mabadiliko yalisababisha uchumi wa nchi kupoteza mwelekeo mwaka jana.

Askofu Mokiwa aliitaka serikali kuchukuwa hatua za haraka mwaka huu wa 2008 dhidi ya mabadiliko makubwa ya uchumi yanaoyendelea kupoteza muelekeo wa watanzania kwa kujenga matabaka matatu ya matajiri, watu wenye hali nafuu na maskini ambao wanazidi kuongezeka kwa kasi.

Naye Kadinali Pengo wa Kanisa Katoliki alisema kuwa viongozi wasiowasaidia watu wao kuweza kujinasua kiuchumi ni viongozi wasiofaa, hivyo kuwataka wajichunguze upya.

Hatuwezi kuzungumzia taifa au dunia yenye amani bila kuwa na familia zenye upendo uliosimama, wazazi ambao ndiyo wajenzi wakuu wa upendo kwenye familia wanatakiwa wawezeshwe kiuchumi ili waweze kuonyesha upendo kwa kuendeleza familia zao," alisema na kuongeza kuwa viongozi wa watu au jumuia yoyote wasiyowawezesha watu wao kujinasua kiuchumi na kuzisaidia familia zao hawafai kuwa viongozi.


Naam, ukimya unaanza kutoweka, bubu wanaanza kusema!
Hii ndiyo inayo takiwa, waendelee kuelimisha jamii ya watz ili tujue kwamba tulipo siko tulipo paswa kuwa!, wapo walio tufikisha ambao hutumia kutojua kwetu kujineemesha, lakini kikubwa zaidi tunayo nguvu ya pekee juu yao, nayo ni sanduku la kura! Tukutane 2010.
 
Kanisa Katoliki laishukia serikali

na Edward Ibabila, Musoma
Tanzania Daima


KANISA Katoliki nchini limeelezea kukerwa kwake na hali ya mambo nchini hivi sasa, inayoonyesha kukithiri kwa vitendo vya rushwa, ufisadi na uroho wa madaraka, vinavyofanywa na baadhi ya viongozi serikalini.

Kwa upande mwingine, kanisa hilo limeelezea kusikitishwa kwake na mizigo anayobebeshwa mwananchi wa kawaida, kupitia gharama za maisha anazolazimika kuzilipia kama vile ankara za umeme na ada za leseni.

Hiyo ni kauli ya kwanza kutolewa na Kanisa Katoliki nchini, tangu kuibuka kwa kashfa za ufisadi, zilizohitimishwa hivi karibuni na kubainika kwa ubadhirifu wa mabilioni ya fedha kupitia akaunti ya kulipa madeni ya nje iliyoko Benki Kuu (BoT).

Kauli hiyo ilitolewa jana mjini hapa na Rais wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki nchini (TEC), Thadeus Lwaiche, ambaye ni askofi wa Kanisa Katoliki Jimbo la Dodoma, wakati wa ibada ya kuwekwa wakfu Askofu mpya wa Jimbo la Musoma, Michael Msonganzila, iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Maria Mama wa Mungu la mjini Musoma jana.

Bila kutafuna maneno mbele ya Waziri Mkuu, Edward Lowassa, aliyekuwa mgeni rasmi katika sherehe hizo, Askofu Lwaiche alisema matatizo ya rushwa na ufisadi yanayoikabili nchi kwa sasa yanatokana na baadhi ya viongozi serikalini kuwa wabinafsi na wasiowajibika, hali ambayo alisema inachochea umaskini miongoni mwa jamii na taifa kwa ujumla na kusababisha kaulimbiu ya maisha bora kwa kila Mtanzania ionekane haina maana yoyote.

“Nchi yetu inakabiliwa na matatizo ya rushwa na ufisadi, ambayo yanasababishwa na ubinafsi na kutowajibika kwa baadhi ya watu waliopewa majukumu ya kuwatumikia wananchi. Mambo haya machafu yanazidisha umaskini kwa jamii na taifa na kusababisha kaulimbiu ya maisha bora kwa kila Mtanzania isiwe na maana,” alisema.

Kwa upande mwingine, kiongozi huyo wa kidini alibainisha kuwa hatua ya serikali kupandisha gharama za leseni na umeme ni kukwepa hali halisi ya matatizo yaliyopo kwenye Shirika la Umeme nchini (Tanesco), na kuongeza kuwa hatua hiyo ni njia ya mkato ambayo kwa vyovyote vile inawaathiri zaidi wananchi wengi wenye vipato kidogo.

Kwa upande wa ubadhirifu wa Benki Kuu (BoT), ambapo imethibitishwa kuwa sh bilioni 133 zilifujwa, Rais huyo wa TEC aliwapongeza bila kuwataja majina, wale wote waliopaza sauti kuweka wazi uozo huo na kuwataka kuendelea kufanya hivyo, kwani ni njia sahihi ya kuonyesha utumishi wao kwa Watanzania.

Aidha, alimpongeza Rais Kikwete kwa hatua aliyochukua kutokana na ubadhirifu uliofanyika BoT.

Baada ya kukabidhiwa ripoti kuhusu akaunti hiyo na Kampuni ya kimataifa ya ukaguzi wa hesabu ya Ernst & Young, Rais Kikwete alitengua uteuzi wa aliyekuwa Gavana wa BoT, Daudi Ballali, na kuiagiza bodi ya benki hiyo kuwajadili wote waliohusika na kuwachukulia hatua stahili.

Aidha, alimuagiza Mwanasheria Mkuu wa Serikali, akishirikiana na Mkuu wa Jeshi la Polisi, Takukuru pamoja na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, kufanya uchunguzi dhidi ya wote waliotajwa kuhusika katika kashfa hiyo, na kuwachukulia hatua, ikiwamo ya kurudisha fedha zote ambazo zililipwa kimakosa.

“Hata hivyo kuna mambo mengi yanayohitaji majibu kutoka serikalini. Kuna baadhi ya mambo yanayohitaji majibu ya kina, lakini yanatolewa ufafanuzi na majibu mepesi, hali ambayo si nzuri kwa maendeleo ya taifa na kanisa,” alisema.

Kuhusu vurugu zinazoendelea nchini Kenya, Askofu Lwaiche aliwataka wanasiasa nchini humo kutafuta mizizi ya vurugu hizo na kuiondoa, kwa kuzingatia masilahi ya taifa lao na kuheshimu uhai wa Wakenya, ambao wanapoteza maisha na wengine kuyakimbia makazi yao.

Aliwataka waumini wa kanisa hilo nchini kutoa michango kwa ajili ya wananchi wa Kenya walioathiriwa na vurugu za kisiasa.

Kwa upande wake, Lowassa aliwaambia watu waliokusanyika kushuhudia tukio hilo kuwa jamii haiwezi kutenganisha dini na maendeleo ya watu, kama ambavyo dini haiwezi kutenganishwa na umaskini.

Akizungumza na maelfu ya watu waliofurika kwenye ibada hiyo, akitoa nasaha za kumpongeza Askofu Msonganzila, waziri mkuu alisema kwa kiasi fulani umaskini unaletwa na watu kutofanya kazi kwa bidii na maarifa, kutojituma na kutokuwa wabunifu.

“Tunahitaji kufanya kazi kwa bidii na maarifa ili kupata maisha bora. Hakuna njia fupi na rahisi ya kupata maisha bora… mtusaidie kuhimiza waumini wenu wajibidiishe katika kazi ili kuondokana na umaskini… wawe wavumilivu na wawe na subira ya mafanikio ambayo yatakuwa endelevu,” alisema.

Ibada hiyo ya kumweka wakfu na kumsimika Askofu Msonganzila ilihudhuriwa na Balozi wa Vatican Tanzania, Askofu Mkuu Joseph Chennoth, maaskofu 28 kutoka hapa nchini wakiwemo wawili wa kutoka Kenya na Uganda, pamoja na viongozi kadhaa wa serikali na chama.

Katika salamu zake, waziri mkuu alimwomba Askofu Msonganzila apambane na mmomonyoko wa maadili ambao umeikumba Tanzania na kusababisha matukio ya mimba kwa watoto wa shule, ubakaji wa watoto kama kinga ya maambukizi ya VVU, mauaji ya vikongwe na maalbino, kwa imani za ushirikina, ambayo alisema yameshamiri kwa kiwango kikubwa.

“Naiona kazi kubwa mbele yako ya kujenga imani thabiti ya Kikristu miongoni mwa waumini wako ili mauaji ya aina hii yasitokee jimboni mwako… naamini penye imani ya kweli ya kidini matukio haya hayawezi kutokea,” alisema.

Alisifu ushirikiano mzuri uliopo baina ya Kanisa Katoliki na serikali na jinsi kanisa hilo linavyojishirikisha kutoa huduma bora za afya, elimu na maji, tena bila ubaguzi wa aina yoyote.

Ili kukamilisha ujenzi wa Hospitali ya Kwangwa ya mkoa, alimwagiza Mkuu wa Mkoa wa Mara, Luteni Kanali (mstaafu) Issa Machibya, asimamie upatikanaji wa hati ya kumiliki ardhi ya eneo hilo.

Ombi la hati ya eneo hilo, lilitolewa na Askofu Mkuu Anthony Mayalla wa jimbo la Mwanza, ambaye alikuwa anasimamia Jimbo la Musoma tangu Askofu Justin Samba alipofariki dunia mwaka mmoja na nusu uliopita.

Kabla ya uteuzi huo, Askofu Msonganzila alikuwa Mkurugenzi wa Mashirika ya Kipapa.
 
Sina hakika kama maneno haya yalimfanya Pengo afurahi . Sina hakika kama wataendelea kutoa pongezi kwa wasemaji wa maovu nakuwaasa waumini wao kutowachagua mafisadi . Wakifikia hapo nitaamini kweli Kanisa langu Katoliki linasimamia haki nchini mwangu Tanzania .
 
Sina hakika kama maneno haya yalimfanya Pengo afurahi . Sina hakika kama wataendelea kutoa pongezi kwa wasemaji wa maovu nakuwaasa waumini wao kutowachagua mafisadi . Wakifikia hapo nitaamini kweli Kanisa langu Katoliki linasimamia haki nchini mwangu Tanzania .

Wanafiki tu siku zile walisema Muungwana ni zawadi toka kwa Mungu, mimi nitakubaliana nao ikiwa yeye Muungwana atasafisha na kufanikisha kurudi kwa mamilioni yaliyotumika katika kampeni za uchaguzi.
 
2008-01-27
Na Simon Mhina

Viongozi wa dini, wakiwemo maaskofu na mashekhe, wamelalamikia kitendo cha uongozi wa mgodi wa North Mara unaomilikiwa na kampuni ya BARRICK kuwalazimisha kuvua misalaba ya kichungaji, kuwafunua kanzu na kuwapekua hadi sehemu za siri.

Viongozi hao walifanya ziara kwenye mgodi huo, kwa nia ya kutaka kujionea wenyewe hali halisi ya mambo yanayojiri katika baadhi ya migodi, baada ya kusikia malalamiko mengi kutoka kwa wananchi.

Viongozi hao ni pamoja na Katibu Mkuu wa BAKWATA Alhaji Ally Mzee, Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kiluther Tanzania (KKKT), Alex Malasusa na Maaskofu wa Angalikana na Katoliki.

Wengine ni Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania CCT Mchungaji Dk. Leonard Mtaita na Mashekh wa mikoa ya Mara na Mwanza.

Alhaji Mzee alisema upekuzi waliofanyiwa na wawekezaji hao, umewadhalilisha.

Alisema alishangaa na kusikitika mno kuona kiongozi kama Askofu Malasusa anaamrishwa avue msalaba wake ili asachiwe.

Alisema mashekh wengine walilazimika kufunua kanzu zao, na kuingizwa mtambo wa upekuzi katikati ya miguu, hali iliyowadhalilisha mno.

``Hivi sisi viongozi wa dini tunaweza kwenda mgodini kuiba? Yaani hawa wawekezaji hawajui umuhimu wetu, hivi kama sisi viongozi wa dini wa ngazi za kitaifa tumedhalilishwa kiasi hicho hali ikoje kwa wananchi?``alihoji.

Alisema kilichosababisha yote ni hatua yao ya kukataa kupokea maelezo ya wamilikini kuhusu mgodi huo kwa maandishi.
Alisema nia ya viongozi wa dini ilikuwa ni kujadiliana na wenye mgodi kwa upendo ili kujua kinachoendelea.

Alisema ni wazi kwamba viongozi wa mgodi hawakutaka viongozi wa dini wazungumze na wananchi wanyonge, bali walitaka waishie kwenye ofisi zao.

``Hatukwenda kuwahukumu wala kuwalaumu, kama viongozi wa kiroho tulitaka kujua nini hasa kinafanyika, kwa vile tulidhani huenda mengine yanayozungumzwa dhidi ya wawekezaji hao ni uonevu,``alisema.

Alisisitiza kwamba jambo kubwa walilojifunza ni kwamba Watanzania hawajafaidi maliasili yao hususan madini.

Alisema kuna uwezekano mkubwa wawekezaji hao wanabebwa na wakubwa ndio maana wanakuwa na kiburi cha aina hiyo.

Akizungumza na Nipashe, Askofu Malasusa alisema licha ya shida na dharau walizopata, ziara hiyo ilikuwa ya manufaa.

Alisema manufaa waliyoyapata ni kwamba wamefahamu uhalisi wa matatizo ya wananchi hao, ambayo walikuwa wanayasoma tu kwenye vyombo vya habari.

Askofu Malasusa alikiri kwamba ilimbidi awe mkali, baada ya wamiliki wa mgodi huo kuonyesha dhahiri kwamba hawataki wajue kinachoendelea ndani ya mgodi.

Hata hivyo, alisema wao hawakuvamia mgodi huo, bali walifuata taratibu, ikiwa ni pamoja na kuandika barua na kuipitishia kwa Mkuu wa Wilaya.

Alhaji Ally Mzee alisema kama kuna Watanzania wanaoteseka nchini na kudhulumiwa kupita kiasi ni wale wanaoishi kwenye mgodi huo.

Hata hivyo, alisema kamati hiyo haikutumwa na serikali, bali wao kama viongozi wa dini, walisikia malalamiko ya muda mrefu kutoka kwa wananchi ambao ni waumini wao.

``Tulienda kujionea wenyewe kwa macho yetu ni kitu gani kinachoendelea huko, ili tusianze kulaumu kabla hatujaona, lakini tuliyoona huko na kuyasikia yametusikitisha,``alisema katibu huyo.

Bw. Mzee ambaye alifuatana na Dk.Mtaita alisema hata nyumba zinazodaiwa kujengwa na wamiliki wa mgodi kwa ajili ya wananchi walioporwa ardhi yao, si lolote si chochote.

Alisema wananchi hao wameporwa ekari nyingi na kupewa fedha kidogo mno.

Alisema hata baada ya kupewa nyumba hizo hazina msaada kwa wananchi hao, kwa vile hawana mashamba ya kulima.

Alisema kibaya zaidi wananchi hao inaonekana kabisa hawasikilizwi wala hakuna anayejali kilo chao.

``Walitueleza mambo mengi yakutisha yaliyotufanya tushangae kwamba kweli uonevu kama huu unafanyika kwenye Taifa la Tanzania,``alisema.

Akizungumza na Nipashe jana, Ofisa uhusiano wa mgodi huo, Bw. Nyasigo Cornel alisema upekuzi huo haukulenga kuwadhalilisha viongozi bali kulinda usalama wao.

Alisema hata maafisa wakuu wa mgodi hulazimika kusachiwa wanapoingia ndani.

``Ndani ya mgodi ni sehemu nyeti kuna vitu ambavyo huruhusiwi mtu kuingia navyo kwa usalama, ndio maana wakasachiwa,``alisema


* SOURCE: Nipashe

My Take:

Tulisema mmelala nao kitanda kimoja, na kujifunika mablanketi ya ufisadi sasa leo wamewageuka mnashangaa!!?
 
My Take:

Tulisema mmelala nao kitanda kimoja, na kujifunika mablanketi ya ufisadi sasa leo wamewageuka mnashangaa!!?


Agreed mkuu. Kwa nini wasingeamua kutoendelea na safari yao kama njia moja ya ku-protest. Wameshakubali kuvua kanzu na misalaba sasa wanacholalamikia nini na kwa nani huyo atakaye wasikiliza? Kesi ya nyani kwa tumbili!

Wanavuna walichokipanda.
 
`Kikwete chaguo la mungu`

2005-06-14 15:35:33
Na Daniel Mkate, Jijini

Bado malumbano kati ya watumishi wa Mungu na wanasiasa kuhusu mgombea wa CCM Jakaya Kikwete kuteuliwa kuwania nafasi hiyo yanaendelea, hivi karibuni Mwinjilisti wa Kanisa la Miracle Healing Ministry kutoka Gaborone Botswana, Alphonce Temba, amedai ana uhakika Kikwete amechaguliwa na Mungu kuongoza nchi ya Bongo!

Hayo yamesemwa na mwinjilisti huyo Mtanzania anayeishi kule Gaborone, walipozungumza na gazeti hili.


SOURCE: Alasiri

Maaskofu: Kikwete ni 'Nabii'
*Wasema hata manabii wa kweli walianza kwa matatizo
*Wadai hata shetani sasa amejenga hofu kubwa kwake
*Wawataka wananchi kuvumilia 'mitikisiko' inayotokea


Na Charles Mwakipesile, Mbeya

MAASKOFU wa Kanisa la Moravian Tanzania, wamesema matatizo yanayoikumba Serikali ya Awamu ya Nne, ni ishara kuwa Rais Jakaya Kikwete anakubalika mbele ya Mungu na ni kama manabii walivyopata shida katika ukombozi kabla ya mafanikio.

Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi jana katika makao makuu ya Kanisa hilo jimbo la Kusini Magharibi, walidai kuwa hakuna kitu cha ajabu kinachotokea katika utawala wa Rais Kikwete, zaidi ya kuwa ni ishara kuwa Mungu anatarajia kuinyeshea Tanzania 'mvua ya baraka' kupitia kwake.

Askofu Mkuu wa Jimbo la Kusini Magharibi, Mhashamu Alinikisa Cheyo, alisema katika vitabu vitakatifu, inaelezwa wazi, kuwa watu maarufu kama manabii wakiongozwa na Yesu, walipata matatizo makubwa kabla ya kupata mafanikio.


HIZI ni BAADHI YA NUKUU KUTOKA MIDOMONI MWA VIONGOZI WA DINI. SASA HIVI WAMEPIGWA NA BUTWAA KUONA UFISADI UNAVYOLIMOMONYOA TAIFA. WANSHINDWA KUMEZA MANENO YAO NA KUMKOSOA JK. WAKATI WA UCHAGUZI WALIWAAMINISHA WADANGANYIKA WENGI KUWA JK NIN CHAGUO LA MUNGU, SASA WANASHINDWA KUWA-FACE WAUMINI WALEWALE NA KUKANA KILE WALICHOKISEMA. KWA KASI YA UFISADI ULIVYO NCHINI, JK HAKUWA CHAGUO LA MUNGU. KIBAYA ZAIDI WAKATI HUO HATUKUONA "WAFUASI WATIIFU WA SISIEMU" WAKISEMA VIONGOZI WA DINI WANACHANGANYA DINI NA SIASA. ILA KWA VILE MKJJ LEO ANAWAKUMBUSHA WAJIBU WAO BAADHI YA WATU WASIOLEWA WANASEMA MKJJ ANACHANGANYA DINI NA SIASA, OLE WENU JK,EL, RZ, NA WAFUASI WENU.... "HAKI HUINUA TAIFA"
 
Hawa wachungaji wanatuona kondoo in the real sense wanadhani wao tu ndio wanajua kuisoma hiyo biblia:
My people are destroyed for lack of knowledge. Because you have rejected knowledge, I also will reject you from being My priest. Since you have forgotten the law of your God, I also will forget your children.
Kwanza linalotumaliza ni lack of knowledge, viongozi wanaambiwa kuna mafisadi, lakini hata kusikiliza hawako tayari, and yet the bible says:


Thieves must quit stealing and, instead, they must work hard. They should do something good with their hands so that they'll have something to share with those in need.

Mafisadi mnaambiwa mkome kuiba .... Mbona hawa wachungaji hawayasemi haya. Ndo maana mnavuliwa misalaba. Size yenu!
Pure and undefiled religion in the sight of our God and Father is this: to visit orphans and widows in their distress, and to keep oneself unstained by the world.

Badala ya kuwatetea masikini wao wana watetea wenye madaraka na matajiri.. halafu wana jidai watumishi wa Mungu, mbona Mungu anayosema ni tofauti na yao?

Mhhh... Hizo mvua za neema sijui zitakujaje huku wanaiba left right and center!
 
Wana JF, Jambo moja linalo sumbua Nchi yetu kwa Sasa Ni Ufisadi uliofanywa na unaofanywa na Viongozi Wetu, na Mojawapo ni hili la Raisi Mstaafu Benjamini Williami Mkapa.

Kwakuwa imekuwa ni vigumu kwa Kikwete na taasisi zingine za Serekali kumchukulia hatua, aidha kwa Kuogopa au kwa Madai ya Mapungufu ya Sheria au watu kuogopa kumwagiwa Tindikali au Polonium 210 (Hope Spelling za Polonium ziko Sawa).

Ningependa Si sote tuliopo hapa Jamvini/Kijiweni kuwaomba Viongozi wetu wa Dini Kuanzia Sheikh Mkuu Kassim Bin Simba , Muhashamu Kardinali Pengo na Msaidizi Wake Method Kilaini, Dr Alex Mtetemela na Bishop Mokiwa, wamfuate Mkapa kiutu uzima kumuomba hizo Mali alizo Iba au kuchukua kwa Njia zisizo faa, Awakabidhi ili wazirudishe Serekali, na Zile walizo chukua Marafiki, Mashemeji/ndugu nk kadhalika nazo Yeye Mkapa awaombe Mashemeji/Ndugu na Marafiki wakubali azirudishe ili kuliokoa taifa na Majanga kama ya Kenya, Somalia Nk.

Na pia kupunguza Mzigo kwa Tume kibao ambazo zina shindwa kuwasilisha Report zao maana System nzima wamezila hizo Pesa/Mali au wanaogopa kumfunga Paka Kengele.
 
..je,wana ushahidi au dhamira hiyo au sisi ndio tutawapa?

..halafu,tunajuaje kama nao hawakufaidika nazo?mi nadhani hilo jukumu litakuwa zito sana kiasi cha kubebeka!
 
August,

Dhamira- sidhani kama CCM kuna mtu ana dhamira kumsihi BWM arudishe mali. Na je kwa nini iwe BWM peke yake?

Ndo maana wizi upo na unaendelea -na umezoeleka tangu mda mrefu!

Je kuna dhamira ya kweli?

Wengi wa viongozi na wafanyakazi- wanatafuta namna ya kuiba na kupora!
 
hawajipendi? si walilala kitanda kimoja na ufisadi na kujifunika mablanket ya unafiki! Leo wakurupuke na kusema "kitanda kinachawa"?
 
..je,wana ushahidi au dhamira hiyo au sisi ndio tutawapa?

..halafu,tunajuaje kama nao hawakufaidika nazo?mi nadhani hilo jukumu litakuwa zito sana kiasi cha kubebeka!

Ushaidi naweza kusema wanao kutokana na kelele nyingi kutoka kwa wananchi, nyingine ni kutokana na report mbali mbali na nyingine ni matokeo ya uongozi mbaya kama kufirisika atcl, tanesco just mention a few. kuhusu dhamira , naona wanayo japo nusu nusu, kwa mfano wamediriki kutembelea mgodi huko musoma , wamekuwa wakitamka/ kukemea ufisadi. mwingine wanaweza kuupata kutoka serekalini na kwa wabunge. sema kitu kikubwa ni dhamira.
 
August,

Dhamira- sidhani kama CCM kuna mtu ana dhamira kumsihi BWM arudishe mali. Na je kwa nini iwe BWM peke yake?

Ndo maana wizi upo na unaendelea -na umezoeleka tangu mda mrefu!

Je kuna dhamira ya kweli?

Wengi wa viongozi na wafanyakazi- wanatafuta namna ya kuiba na kupora!

Pendekezo langu ni kuanzia BWM mkapa maana ndio kichwa, then nimesema marafiki/viongozi wenzake wengine, na Ndugu na Jamaa etc.

Kuhusu dhamira kwa ccm kwa kweli ni ndogo ndio maana nimeomba wawe viongozi wa Dini wenye kuchukua hiyo hatua.

Ndio maana kwenye thread mojawapo hapa jamvini kuna watu walipendekeza Kuundwa kwa Seneti ambayo itajumuisha Viongozi wa Dini na wazuoni wengine including wastaafu waliotukuka.
Lakini kwa sababu sasa hatuna hiyo Senati basi ni Juu yao Kuchukua Hatua Hiyo kwa Madaraka makubwa na Heshima walio kuwa nayo katika Jamii.

Lakini wakijiona hawana jukumu hilo au kupiga kelele za Danganya Toto basi wasubiri ya Rwanda ambapo Viongozi wengine wa Dini walionekana kuhusika.
 
August,

Tunaweza kuanzisha kampeni ili kanisa limtenge huyu mpaka azungumzie kashfa mbali mbali zinazomkabili. Hawezi kutudharau Watanzania kama vile yeye ni Mungu. Amefanya madhambi mengi sana huyu ya kutumia wadhifa wake kujitajirisha hii kampeni inaweza ikawa mwanzo wa kumfanya huyu fisadi ajue kwamba usemi wake wa, "Nimeshastaafu kwenye siasa" haukubaliki na Watanzania.
 
Hili suala la viongozi wa dini kuwatenga hawa mafisadi (Mkapa na wenzie wote, aliokua nao madarakani na waliopo madarakani sasa) ni muhimu sana. Nimebahatika kuwemo kwenye ibada na baadhi ya mafisadi. Nilishangaa jinsi wanavyojiposition kama vile wao ni wateule wa Mungu. Wanajikunja kama wako njiani kuelekea mbinguni.

Cha maana ni kwamba, kama kweli viongozi wetu wa dini wanafikiri kwamba amani ni kitu muhimu (wakitumia mfano wa majirani zetu wa Kenya), basi wakati umefika kwa wao kutowaruhusu mafisadi kuingia katika maeneo ya ibada.
 
Viongozi wa dini wasiwe tu wanakemea ufisadi lakini kuna umuhimu mkubwa kwa wao kuanza kuchukua hatua dhidi ya mafisadi kama vile kuwatenga na kanisa. The have the power to do something in order to get rid of ufisadi.
 
Kwenye dini tunasema "hate the sin but love the sinner". Hatujui kama Mkapa ana "dhambi" ya kuiba mali ya umma. We should not judge.

Uraiani, tunaweza kudai mali zilizoibiwa na viongozi zirudishwe. Lakini ni ndoto kudhani hilo linaweza kufanikiwa wakati chama cha viongozi hao hao bado kiko madarakani. Itabidi CCM ikae benchi kwanza, ndio viongozi wapya waweze kufuatilia mali zilizoibiwa na viongozi waliopita.

Kikanisa, wanatengwa tu wale wanaofundisha theolojia ya uasi. Hawatengwi wadhambi, kwani sote tu wadhambi.
 
Back
Top Bottom