Mshaurini Vicent Nyerere aachane na hizo siasa. Hoja kuu ambayo alitakiwa kuisimamia ni kwamba Vicent Nyerere hajawahi ku-claim mahali popote pale kwamba yeye ni mtoto wa Marehemu Mwalimu Nyerere. Kwa hiyo, claim ya Mkapa ilikuwa baseless na haiwezi ku-hold maji na hizo ndio siasa za maji taka, watu wanaacha hoja halafu wanakijita kwenye kuzua vijambo na vijimambo.
Discussion za chanzo cha kifo cha Mwalimu Nyerere kwa sasa haziwezi kuwasaidia CHADEMA ili washinde huko Arumeru Mashariki. Mjadala huo kwa sasa hauna msaada wowote kwa wananchi wa Arumeru ambao wana matatizo ya Ardhi na Maji, pamoja kukosekana kwa ajira kwa vijana.
Focus ya Kampeni ya CHADEMA iwe ni kwenye kero za wananchi wa Arumeru. Ili kumgonga vilivyo Mkapa na Chama chake, matatizo ya maji na ardhi hayajaanza leo wala juzi, yapo kwa miaka mingi sasa. Je, Mkapa akiwa Rais ina maana hakuyajua hayo matatizo, kama aliyajua, kwanini hakuyashughulikia? Kikwete yuko madarakani mwaka wa 7 sasa, je hajapelekewa hayo matatizo au hajui hayo matatizo? Je, wananchi watakuwaje na imani kwamba Mkapa akienda kumwambia Kikwete matatizo ya maji na adhi atayatatua na ilihali amekuwa madarakani kwa miaka 7 na matatizo yako pale pale?
Iwapo Mzee Sumari (RIP) alishindwa kusaidia kutatua matatizo ya Arumeru Mashariki akiwa Naibu Waziri wa Fedha (sehemu ya serikali ya chama tawala), je leo hii mwanae ndio ataweza kuyatatua? CCM kimebaki kuwa ni chama cha kuweka ahadi hewa bila kutimiza. Hapo ndio CHADEMA inatakiwa kusimamia kwa kuwa ndo ukweli wenyewe na wananchi wanajionea. Wakumbusheni kwamba hata Igunga ambako CCM walishinda uchaguzi mdogo, zile ahadi zote za CCM zilizotolewa kwa wana Igunga ikiwemo ya kujengewa daraja hazijatimizwa hata moja!