Vijana wa Dar na Vibegi mgongoni

Vijana wa Dar na Vibegi mgongoni

mwendokasi ya feri kwenda kimara ptuu,kidogo nitapike.full mindoo ya samaki abiria mmerundikana km meli ya utumwa.
nilikua najaribu tu kutumi huu usafiri unaoitwa wa kistaarabu ni balaa tupu.nikashuka hapo kisutu nikasongesha home na mashine.
 
wanakera kaka ujue changamoto nyingine ni za kutengenezwa mojawapo hii hapa
Usijifanye we mkamilifu ........na we unatukera kwa manukato yako na harufu ya minywele yako [emoji24] [emoji24]
 
Duhh aisee huko ndani ni balaaa kwanza wanaweka nguo,pili socks tatu zana za kazi....yani ni WIZI WIZI WIZI mtupu na hayo mabegi...coz kuna tukio nilishawai ona kbsa.
 
Siyo kwamba kuchungulia chungulia vibegi vya watu ndio ushamba?Halafu mtu akibeba kibegi mgongoni wewe inakuuma nini wakati hajakulazimisha na wewe kubeba?Town watu wanajali mambo yao na siyo kumind ya wengine mkuu.
 
Sijui wanaweka nini humo ndani, maana ni kama fashion kwa sasa.
Juzi wakati nipo Taifa kuna kijana nilikaa nae jirani wakati anafungua nikachungulia, Ajabu katoa headphone ya simu na hamkuemo na kitu kingine cha ziada ndani nilichoka sana.

Binafsi naona kama ni ushamba fulani hivi ambao vijana wanalimbukia bila kujielewa.
Mbona hushangai mwanamke kubeba mkoba?
 
Mi binafsi beg ni moja ya vazi langu ukiacha nguo za kawaida,unaweza nunua chochote ukaweka humo,nk! Kwanini wanaume Wa mikoani mnajifanya kila kitu mnakitia kasoro? Nyie mnabebe wapi vitu vyenu? Kwenye Rambo?
 
Mi binafsi beg ni moja ya vazi langu ukiacha nguo za kawaida,unaweza nunua chochote ukaweka humo,nk! Kwanini wanaume Wa mikoani mnajifanya kila kitu mnakitia kasoro? Nyie mnabebe wapi vitu vyenu? Kwenye Rambo?
 
Mimi beg loshagandia mgongoni,tangu enz za spoti spoti mpaka sasa natumia rainbow,wanaume wa mkoani ndo mnabeba Rambo
 
Begi mgongoni ni salama kwa wafanyakazi wenyewe PC binafsi kazini.

Begi mgongoni ni salama kwa wanafunzi wa vyuo vikuu wenyewe PC zao hapa Dar

Begi mgongoni ni salama kwa mafundi wa umeme na electronic wanapoenda kazini

Begi mgongoni ni salama kwa wanamichezo wanapoenda mazoezini

Begi mgongoni ni salama kwa wafanyabiashara wadogo na wa kati kuweka kumbukumbu zao

Begi mgongoni ni fashion kwa mabishoo
 
mkuu ogopa sana hao vijana...ni wezi sana hao..huku mtaani kwetu wapo kibao..wanaiba sana vitu vya watu...hasa kwa huku mtaani nguo zilizo anikwa..kwa huko posta wanaiba sana viatu kwenye nyumba za ibada....au wengine ni wezi wa mifukoni balaa ...sura za wanavyuo zinajulikana lakini wengi wao ni wezi wakubwa....tena wengine wako smart kama wanachuo au watu wenye mishe muhimu sana kumbe wezi wakubwa....Mkuu ukikutana nao au ukipishana nao uwe kimachale machale sana....
Hoja yako hain mashikooooo, try again
 
Katika siku za karibuni kumeibuka kitu kinachoitwa 'fasheni' ya vijana ya kubeba mabegi ya safari na kuzunguka nayo kwenye vyombo vya usafiri jijini Dar!

Unapowaona hao vijana walivyobeba mabegi yao ya safari unaweza kuhisi wanasafiri kwenda mikoani, kwa hiyo ukadhani wanaenda Ubungo Terminal kwenda kupanda mabasi ya kuelekea mikoani.

Kumbe katika uhalisia hao vijana wameichukulia hiyo hali ya kubeba hayo mabegi kuwa 'fasheni' na kuamua kuzurura nayo jijini Dar!

Hiyo inayoitwa 'fasheni' ya vijana imesababisha kero kubwa sana kwenye usafiri wa Umma hapa jijini Dar, hususani kwenye mabasi ya mwendo kasi, ambapo husababisha mabegi yao hayo wanayoyavaa mabegani, kuchukua nafasi kubwa kwenye hayo mabasi na hivyo kuwakosesha abiria wengi usafiri wa kwenda makazini na wanaporejea toka kwenye shughuli zao.

Nadhani ni muhimu kwa sasa wananchi wote tunaokerwa na hiyo hali inayosababisha kero kubwa sana kwenye usafiri wa Umma kutokana na 'fasheni' hiyo ya kipuuzi ya hao vijana, tuikemee kwa nguvu zote tabia hiyo ili hao vijana wakome kuendelea na hiyo 'fasheni' yao ya kipuuzi.
 
ila kuna pochi za wanaume siku hizi ,mtu ana simu tatu,wallet japo haina zaidi ya elf 2 ,unataka aweke wapi? mwingine ana laptop plus macharger ya simu.acha uzamani wewe
494df773d0729d1f21d7a93898887677.jpg
stock-photo-men-s-casual-outfits-standing-over-gray-grunge-background-with-space-beauty-and-fashion-concept-507406090.jpg
 
Back
Top Bottom