Eng Nyahucho
JF-Expert Member
- Dec 18, 2016
- 688
- 1,156
Sasa ndugu, kazi ninayofanya inahitaji niwe laptop muda wote hivo ni lazima niwe na begi.Katika siku za karibuni kumeibuka kitu kinachoitwa 'fasheni' ya vijana ya kubeba mabegi ya safari na kuzunguka nayo kwenye vyombo vya usafiri jijini Dar!
Unapowaona hao vijana walivyobeba mabegi yao ya safari unaweza kuhisi wanasafiri kwenda mikoani, kwa hiyo ukadhani wanaenda Ubungo Terminal kwenda kupanda mabasi ya kuelekea mikoani.
Kumbe katika uhalisia hao vijana wameichukulia hiyo hali ya kubeba hayo mabegi kuwa 'fasheni' na kuamua kuzurura nayo jijini Dar!
Hiyo inayoitwa 'fasheni' ya vijana imesababisha kero kubwa sana kwenye usafiri wa Umma hapa jijini Dar, hususani kwenye mabasi ya mwendo kasi, ambapo husababisha mabegi yao hayo wanayoyavaa mabegani, kuchukua nafasi kubwa kwenye hayo mabasi na hivyo kuwakosesha abiria wengi usafiri wa kwenda makazini na wanaporejea toka kwenye shughuli zao.
Nadhani ni muhimu kwa sasa wananchi wote tunaokerwa na hiyo hali inayosababisha kero kubwa sana kwenye usafiri wa Umma kutokana na 'fasheni' hiyo ya kipuuzi ya hao vijana, tuikemee kwa nguvu zote tabia hiyo ili hao vijana wakome kuendelea na hiyo 'fasheni' yao ya kipuuzi.
Maisha ya sasa yanauhitaji mkubwa sana wa laptop kwa hiyo itakuwa ngumu kulikwepa hilo